Episode 1: Chama hatari cha Majesuit

Episode 1: Chama hatari cha Majesuit

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
LEO TUPATE ELIMU KUHUSU KUNDI LA JESUIT kundi la ‘Jesuit Society' maana wao ndio waliomfundisha Adam Weishaupt ambaye ni muasisi wa Illuminati. Shirika la Jesuits lilianzishwa na Ignatius Loyola aliyezaliwa mwaka 1491 na kufariki Julai 31, 1556. Sherehe ya Ignatius Loyola hufanyika kila ifikapo Julai 31 ya kila mwaka, siku aliyokufa. Mkuu wa shirika la Jesuit anaitwa "Black Pope" yaani "Papa Mweusi."

Hapa haimaanishi kuwa mkuu huyo anatakiwa awe wa rangi nyeusi yaani mwafrika bali neno ‘black' linamaanisha ‘asiyeonekana,' na kwa maana hiyo Jesuit Society wanafanya kazi za siri, zisizoonekana, tena za giza ambazo ni kinyume na nuru ya neno la Mungu. Shirika hili lilianzishwa ikiwa ni matokeo ya kanisa Katoliki kupiga vita uprotestant. Kujitoa kwa Loyola katika kulitumika kanisa kunaweza kuonekana kwenye kanuni 13 za shirika la Jesuits zinazolihusu kanisa; "Rules for thinking with the church" anaposema "I will believe that the white that I see is black if the hierarchical Church so defines it". Kwamba "nitaamini rangi nyeupe ninayoina kuwa ni nyeusi kama mfumo wa uongozi wa kanisa utatafsri hivyo."

Na ndivyo ilivyo katika shirika hili ya kwamba mtu anapaswa kuamini na kufanyia kazi kile anachofundishwana kanisa hata kama dhamira yake inamwambia kuwa hicho si sahihi. Hebu soma nukuu hizi ili tuone chanzo cha chama cha Jesuits: "Kuinuka kwa dhama za giza kulitokana na kuruhusu Biblia ipatikane kwa urahisi hata kwa watu wa kawaida na mafundisho ya waprotestant wanamatengenzo.

Mafundisho haya yalikuwa na msingi wa kutafsiri unabii kutokana na historia; yaani kuwakilisha siku 1260 za Danieli na Ufunuo kuwa miaka 1260. Viongozi wa matengenezo kama Luther, Calvin, Huss, Wycliff, Knox, Latimer, Cranmer, Ridley, Hooker, Newton na wengine waliamini hivyo na kufundisha." Ibid p 7. "Kwa kutumia mbinu hii ya kutafsiri unabii, kanisa la Roma lilionekana wazi kuhusika na unabii huu wa pembe ndogo katika Daniel 7, na mnyama wa Ufunuo 13:1, mwanamke wa Ufunuo 17, ikiwa ni pamoja na kichwa cha kanisa kuwakilisha Mtu wa Kuasi wa 2 Wathesalonike 2. Kadri mafundisho haya yalivyozidi, kanisa la Roma lililazimika kujilinda dhidi ya kuongezeka kwa ushahidi wa unabii wa Biblia kulihusisha kanisa hilo. Hivyo upapa ukaanza kuweka mipango ya kuwapinga waprotestant kwa kuanzisha ‘Jesuit society' ili kisaidie kufundisha mafundisho ya kanisa na kuharibu mafundisho na vitabu vyote vilivyokuwa kinyume na kanisa na kuanzisha "Holy Office of the Inquisition" maalumu kwa ajili ya kuwatesa hata kuwaua wapinzani wa kanisa." Ibid. pp 126, 127. Kati ya mwaka 1524 na mwaka 1537 Loyola alisomea Theology huko Hispania na Ufaransa.

Mwaka 1534 alifika Ufaransa wakati wa kipindi cha mapambano dhidi ya uprotestant, mapambano ambayo yalimfanya John Calvin akimbie kutoka Ufaransa. Mwaka 1539, Loyola akiwa na wenzake walifanikiwa kuanzisha muungano na kuuita ‘Society of Jesus'. Mwaka uliofuata yaani 1540 chama hicho kikapewa baraka na Papa Yohana III na ilipofika mwaka 1548 Papa huyo akatoa kibali kwa Society of Jesus ili kiweze kushughulika na maswala ya kiroho.

Loyola alikufa mnamo Julai 31, 1556 na akabarikiwa na Papa Paul V mwaka Julai 27, 1609, akapewa hadhi ya utakatifu Machi 12, 1622 na Papa Gregory XV na akatangazwa kuwa kiongozi wa maswala la kiroho mwaka 1922 na Papa Pius XI. Jina kamili la Loyola lilikuwa ni Íñigo akiwa ni mtoto wa mwisho kati ya watoto 13. Baada ya kifo cha mama yake mwaka 1506 Íñigo alichukua jina la mwisho "de Loyola" kutokana na jina la mji ulioitwa Loyola ambako alizaliwa.

Akaamua kutumia jina la "Ignatius of Loyola" yaani Ignatius anayetokea mji wa Loyola. Mwaka 1534 aliwakusanya marafiki zake sita ambao alikutana nao chuo kikuu wakiwa ni wanafunzi wenzake ambao ni Francis Xavier, Alfonso Salmeron, Diego Laynez na Nicholas Bobadilla wote wakiwa ni Wahispania; Peter Faber akiwa ni Mfaransa; na Simao Rodrigues aliyekuwa Mreno. Asubuhi ya tarehe 15 Agust 1534, katika kanisa la Our Lady of the Martyrs huko Montmartre, Loyola akiwa na wenzake sita ambapo mmoja wa marafiki hao alikuwa ni padre, waliapa kutumika maisha yao yote. Ignatius akawa ndiye kiongozi mkuu (Superior General) wa chama cha Yesu – Society of Jesus. Yeye ndiye aliyetunga katiba ya chama hicho mwaka 1540

. . . . . . ITAENDELEA . . . . . .
 
uprotestant ulipoteza wengi laiti idadi ingalianikwa,enzi za kina Calvin na Luther ni uozo mkubwa uliofichwa nyuma ya pazia la dini
 
Hata yule Jorge Mario Bergoglio ni kiongozi kwanza wa dini/rais wa ka nchi kenye vilima saba naye kutoka jamii ya jesuit.
 
Mkuu naomba uwe unanitag katika muendelezo wa hii thread...

Kuna kitu cha muhimu ntakipata hapa
 
uprotestant ulipoteza wengi laiti idadi ingalianikwa,enzi za kina Calvin na Luther ni uozo mkubwa uliofichwa nyuma ya pazia la dini

uprotestant ulipotezaje wengi mkuu? mana kwa jinsi nlivyofatilia uzi nimeona hao jesuits walikua against protestants.. kwanini?
 
mkuu Aaron naomba unitag na mm episode 2 mana napenda kuyajua kwa undani
 
Last edited by a moderator:
Harufu ya Uchinja chinja wa kanisaaa unanukia ila watu hawajui tu!!!!!

yaaani!!! Mbweha ndani ya ngozi ya Mwanambuzi!!
 
Naomba uni tag episode 2 pia ndugu msabato...mpoteza watu..na hasira za kupokonywa bara la amerika mlokuwa mmewadanganya watu kwa mafundisho yenu ya uongo na vitisho..ili nikujibu
 
hakuna taarifa ngeni inayo husu jesuits ambayo mleta mada kaileta.nimekuja mbio kwa kuhisi labda nitakutana na habari mpya kuwahusu.kichache alicho share hapa,kinapatikana kwa wingi sana mitandaoni(ingawa kwa lugha ya kingereza),hasa ktk ile mitandao inayojihusisha na conspiracy theories.alicho fanya mleta mada,ni ku-copy na kutafsiri machache aliyo yaelewa toka kingereza kuja kiswahili na kuya-paste JF.anyway,nasubiri episode 2 kwa shauku kubwa.

NB : gwiji wa conspiracy theories david icke,ameeleza vizuri sana kuhusu Jesuit,mcheki hapo ktk video.
 
Last edited by a moderator:
Baadhi ya maandishi ni kweli, ila hawa jamaa wapo kulinda na kutetea imani ya kanisa katoliki. Swali sio uhatari wake ila ukweli ni kwamba haya majamaa yanasoma sana na elimu zote sio tu mambo ya dini bali pia elimu zingine. Kwa hawa jamaa kuwa na doctrate tatu au hata zaidi za mambo tofauti ni kawaida. Wasioamini waende pale Loyola Kigogo uwaone baadhi ya waalimu pale ambao ni wanashirika hilo alafu ulizia cv zao utachoka. Kwa muonekano wengi ni kama machizi ila kichwani ni balaa.
Lazima kuelewa pia kitaaluma inaweza kuwa ndio taasisi ambayo iko safi karibu kila nyanja. Vyuo vingi vyenye sifa na umaarufu duniani hawa jamaa wako nyuma yake kama waanzilishi.
 
Episode 2 tayari nimeshaiweka, nimeshindwa kuwatag wote
 
Back
Top Bottom