EPL - Ligi bora zaidi duniani ona takwimu zake ukiilinganisha na la liga

Historia kama ipi? Nguvu ya pesa la liga Ipo kwa barca na Madrid epl nguvu ya pesa ipo kwa chelsea man utd na man city huoni bado EPL inatumia nguvu ya pesa zaidi?

Namaanisha, hizo cluba bora kabisa La liga, bila pesa zisingekuwa bora. Ukiangalia kama hizo ulizozitaja ndizo zinazonunua wachezaji kwa ada ya record za dunia, wachezaji wenye majina makubwa. Na ndio club pekee zinazotokea kwenye club tajiri 20 duniani kutokea La liga.

EPL zina club nyingi kwenye listi ya club tajiri 20 duniani. Lakini umeweza kuona, Leceister wamebeba ndoo bila kuwa kwenye hiyo listi, Spurs kang'ang'ana top four ilihali club tajiri kabisa duniani iko nafasi ya 5.

Kwahiyo, kwa lugha nyepesi, La liga ni pesa tu ndo itakuweka juu, tofauti na EPL ingawa ndio, kwa namna moja au nyingine, ligi zote, ili ufanye vizuri saaana, unahitaji pesa.

La liga, kwa miaka zaidi ya 10 sasa ni Madrid au Barca tu pale juu.
 
Kama ni bora Kwanini huo ubora wao hauonekani UEFA au EUROPA? tuacheni itani La liga ndiyo bora muda wote.

Ebu tafuta records uone, kwa miaka mingapi EPL imetoa club bora duniani kabla Sir Alex hajastaafu, na wakati huo ni club gani ilikuwa tajiri kabisa! Kisha unambie, nini kiliwashinda La liga kuwa pale juu kabisa kwa kila kitu!!!
 

Plan A, B na C. Ukishindwa zote hizo umeshindwa tu, hakuna mfumo mpya wa kisoka duniani, soja ni pamoja na maarifa, na ushindi ni kumzidi mpinzani wako mbinu. Sasa ulitaka timu zote duniani zicheze mpira wa aina moja, ni nani angekuwa anafurahia hizo game?

Kwa kauli yako, ni kuwa, Laliga wamekariri mchezo mmoja, wakibadilishiwa pattern wanambwela.

Kama wakibaki basi, wakibutua, wakikanyaga ndo wanashinda na timu pinzani isilalamike wala mamlaka za mpira wa miguu zisione tatizo, maana yake hiyo ni sehemu ya mbinu zikubalikazo.

Bundesliga, wana aina ya mpira wao, pasi ngumu, vipi hawa nao hawachezi soka? Serie A je, wanakaba sana, hairuhusiwi? US nao ni mibio, si mpira ule?

Timu kama Chelsea wamecheza karibu pattern zote kwa vipindi mbali mbali, anzia enzi za akina Darmian DUFF.
 
Mfano wako ni irrelevant
 
Kama unapenda sifa za kijinga, butuabutua, blablaaa kibao - EPL ni sehemu sahihi sana kwako

Kama unapenda Kandanda safi, sanaa ya mpira, burudani murua, vipaji halisi vya mpira, chenga kali zitakazokuacha mdomo wazi, magoli makali -La liga ndiyo sehemu yake

Chaguo ni lako
 
naona unaruka point, ngoja basi tufananishe ligi za mabara, we si umesema ligi inatakiwa kuwa ya kishindani ili iwe bora na kuvutia. unasemaje kuwa UCL 2014 alichukua Madrid, 2015 Barca na 2016 Madrid. na wakati huo huo africa vimechukua vilabu toka nchi tatu tofauti. je klabu bingwa Africa ni bora kuliko ya ulaya?
 
Watu wanatesa UCL, europa, club world cup na hata timu ya taifa inasumbua unafananisha na timu za ligi ambayo hata robo fainali timu zake hazifiki, epl wana hela mpaka timu ndogo ila kiwango ni zero!
 
Vipi na Sevilla anaeshika nafasi ya nne kutolewa na kibondo anaetaka kushuka daraja EPL.. Hii imekaaje?
kipindi hichohicho huyo kibonde alitoka kumfunga liver aliyekuwa nafasi ya 3 goli tatu. kwahiyo nayo EPL ni mbovu kisa anayekaribia kushuka kamfunga mtu wa 3?
 
Hii paragraph ya mwisho imehitimisha kwa kuonyesha ni kwanini EPL itaendelea kuwa ligi baba kuliko zote. Wewe mtu yuko red zone ila lakini kwenye michuano ya nje anakimbizana na akina Madrid hadi Leo hii.
Kuna mpira gani Leicester kaonesha hadi umfagilie hivyo? Kafika pale kibahati bahati tu au hukuona game na sevilla alivyobutua butua na kukaa langoni muda wote?
 
Epl ni kama shule ya kata tu....ushndan mkuubwa ila marks zao ni 40,39,38,41,40,40,39....nk...sasa ikija necta shulen wakwanza ana dev four,nothing ushndan wakifala usio na mpango...viwango vdogo ata mshndane vp hamfik mbali coz kila mmojq anaona anamuweza mwenzake kumbe wote wabovu tu
 
Kuna mpira gani Leicester kaonesha hadi umfagilie hivyo? Kafika pale kibahati bahati tu au hukuona game na sevilla alivyobutua butua na kukaa langoni muda wote?
Kinachotafutwa kwenye mpira ni matokeo haijalishi umecheza vipi.

Na matokeo ndio yanayoleta mafanikio ambayo upelekea timu kuonekana bora.

Kwani Leicester kuna sheria yoyote ya mpira aliyovunja kwa approach aliyitumia kumtoa Sevilla?
 
kwa muda mrefu kumekuwa na malumbano juu ya ipi ni ligi bora duniani
kwa takwimu hapo chini nazani tunaweza kuumalza ubishi kam sio kuupunguza

tafadhari tazama katika link hapo chini

TAKWIMU - Epl ligi bora duniani ikifuatiwa na la liga
takwimu zinaonyesha la liga ina team tatu tu bora ndizo zinazosumbua UEFA na zilizobakia ni team ndogo zinazosindikiza hizo tatu kutafuta ubingwa wa ligi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…