EPUKA KUWA WA MTUMWA WA HISIA ZAKO KWENYE MAPENZI..JTATU NJEMA

EPUKA KUWA WA MTUMWA WA HISIA ZAKO KWENYE MAPENZI..JTATU NJEMA

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
EPUKA KUWA MTUMWA WA HISIA ZAKO MWENYEWE📌📌

Watu wengi leo wana ongozwa na hisia kuliko akili. Ukikasirika unafanya maamuzi ya haraka, ukiumizwa una jihukumu, ukifurahi unatoa ahadi usizo weza kutimiza. Mwisho wa siku unajikuta umeharibu mahusiano, kazi, au heshima yako mwenyewe.

Kumbuka hili👇
Hisia ni sehemu ya maisha, lakini hazipaswi kuwa dereva wa maisha yako.
👉 Jifunze kujitawala
👉 Jipe muda kabla ya kuamua
👉 Tambua thamani yako
👉 Linda mahusiano yako
👉 Kuwa mtu wa kanuni, sio mihemko

Mwisho wa yote, mtu mwenye nguvu sio yule anaye shinda wengine, bali ni yule anaye weza kujishinda yeye mwenyewe.

Chagua leo kuwa bosi wa hisia zako, sio mtumwa wa kujitumikisha mwenyewe ✨
 
🌅 HABARI YA ASUBUHI KAKA… 🌅

Kuna mahali unaweza kutoa moyo wako wote, juhudi zako zote, muda wako wote… lakini bado usithaminiwe. 💔
Na ukweli mchungu ni huu—si kila mahali panastahili nguvu yako.

mahali ulipo kosa kuthaminiwa kwa juhudi zako, usipigane kubaki kwa nguvu. Jiepushe kwa heshima, jitenge kwa utulivu, na jithamini kwa vitendo.
Usilazimishe thamani yako kwa mtu asiye ona ulicho nacho.

👉 Jifunze hili leo:
Thamani yako haipungui kwa sababu mtu fulani hakuiona.
Heshima yako inaanza na wewe mwenyewe.
Na nguvu ya mwanaume ni kujua lini aondoke bila kelele.

Kuna sehemu utaenda, utaonekana.
Kuna watu utakutana nao, watathamini uwepo wako.
Kuna maisha yana kusubiri nje ya maumivu uliyo yazoea.
Chagua amani yako.
Chagua heshima yako.
Chagua kujithamini.

Asubuhi hii, simama kifua mbele na ujikumbushe:
“Mimi ni wa thamani, na nitachagua mahali panapo nithamini.”

🔥 Ubarikiwe katika siku yako ya leo kaka!
Usikate tamaa… bora yako bado ipo mbele
 
“Dada, unaweza kuwajali wote… lakini jifunze kumtofautisha mume wako na mtu mwingine yeyote.
Kuna heshima, nafasi na upendo ambao ni wake peke yake❤️”
 
Sio kila mwanaume anahitaji maneno mengi…
Wengine wanahitaji utulivu, heshima na faraja ili waoneshe ubora wao 💪
Kelele hupunguza nguvu zao, amani huongeza uwezo wao 💯🔥
 
KAKA YANGU AMBAYE WEEKEND HII UKO BAR MUDA HUU UNAKULA RAHA NA WAREMBO… 🍻💔

Nakukumbusha tu kuwa watoto wako na mke wako wanatamani uwepo wako nyumbani.

Usifikiri kila kilio cha mke wako ni kelele zisizo na maana…
Mara nyingi ni uchovu wa kubeba majukumu peke yake
Ni haja ya upendo wako
Ni tamaa ya kuona familia yenu inasimama pamoja.

Kuna wanaume wengi wanakimbia nyumbani kwa kisingizio cha “kelele za mke”
lakini hawajui kuwa wanakimbia wajibu wao.

👉 Kumbuka:
Mtoto wako anahitaji uwepo wako kuliko pesa zako
Mke wako anahitaji muda wako kuliko zawadi zako
Familia yako inahitaji upendo wako kuliko anasa za nje

Leo kabla hujachelewa sana…
Simama, jirudi, rudi nyumbani. ❤️
Usije siku moja ukatamani kurudi…
lakini ukakuta moyo wa mke wako umechoka na watoto wamezoea kuishi bila wewe😥
 
Back
Top Bottom