Epuka mtego wa shetani, kuwa makini sana

Epuka mtego wa shetani, kuwa makini sana

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
Punda mmoja alikuwa amefungwa kwenye mti.

Shetani (Pepo) akaja akaifungua ile kamba. Punda baada ya kujiona yuko huru, akaingia kwenye shamba na kuanza kula kila kitu.

Mke wa mwenye Shamba (Mke wa mkulima) akahofia Punda anataharibu kila kitu, hivyo akachukua bunduki, akamuua yule Punda.

Mwenye Punda akaja, akaona Punda wake ameuwawa; akashikwa na hasira, akachukua bunduki yake na kumuua mke wa mkulima.

Mkulima aliporudi nyumbani, na kukuta mke wake ameuwawa, akaenda kumuua Mmiliki (mwenye) wa Punda.

Watoto (wengi) wa mmiliki wa Punda kuona baba yao ameuwawa, wakashikwa na hasira na ghadhabu, wakaenda kuchoma shamba lote la mkulima. Mkulima naye kuona hivyo, kwa hasira akawaua watoto wale wote.

Shetani alipoulizwa amefanya nini, akajibu: “Sijafanya lolote, mimi nimemfungulia Punda tu.”

Umeelewa? Shetani hana nguvu ya kufanya mengi, ila machache tu ambayo yanaweza kuchokonoa na kuamsha roho ya kikatili iliyomo ndani ya mwanadamu.

Hivyo tutafakari kabla ya kutaka kulipiza kisasi! Kuwa mwangalifu na nafsi yako, kwa kuwa mara nyingi, Shetani ambayo hufanya ni "kufungulia tu Punda"

Uwe na tafakuri na mapumziko mema ya mwisho wa wiki. Punda wengi wamefunguliwa tayari. Tahadhari.
 
Nasikia huu mpango wa kumpoteza mwenyekiti uliandaliwa kwa ustadi mkubwa na mwendazake
Wakati mwingine anasingiziwa tu. Ukweli ni kuwa mama ni tofauti kabisa na mwendazake kwa nyanja zote. Hivyo mwenyekiti kusota mwendazake aachwe apumzike.
 
Wakati mwingine anasingiziwa tu. Ukweli ni kuwa mama ni tofauti kabisa na mwendazake kwa nyanja zote. Hivyo mwenyekiti kusota mwendazake aachwe apumzike.
Kwa hili hapa legacy inasingiziwa hili la madame speaker
 
Huyo shetani aliyemfungua punda alitumia njia gani kumfungua na anafananaje kumfungua. Na ili tukio lilitokea wapi?
 
Hakika, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom