Epuka utapeli wa mtandaoni unaoenea kwa kasi

Epuka utapeli wa mtandaoni unaoenea kwa kasi

Kuna mtu alinijia na sound takatifu nkasema hii sio kama D9 kweli... Hela zenyewe za mawazo
Hebu ona mmoja huyu

Good evening guys, I came to make a super ALERT against TRADE COIN CLUB, a multilevel system that is messing with the name of BITCOIN!
I was invited to invest in this "company", of course no one should invest in the dark, so I went to search for information, so I put it on Google, appeared sites talking badly about the company on the day marked where they would explain me better about TRADE COIN CLUB, they explained to me that I would get 50% of everything I came in (stirring up the profit of the crowd), I then asked why so many people complaining then I heard "If you only complain about blame!" Blockchaing¨ and use the name of bitcoin to promote themselves, the owner of TRADE COIN CLUB and DOVER BRAGA!
Searching the net I could find several processes, and complaints, and countless people deceived talking badly of Bitcoin, after all they were deceived, not even shot the reason of them! So people, let's denounce! Put your mouth on the trombone! LET'S NOT LET THE NAME OF OUR TAO BELOVED BITCOIN!
BITCOIN IS SOLUTION, NOT DESTRUCTION!
 
Hebu nitoeni tongo tongo juu ya hii kitu D9! Kuna MTU ameifagilia sana akidai inalipa vizuri kila wiki! Mwenye uelewa atujuze kama ni utapeli au LA!
 
Matapeli yana hoja za kufundishwa huko ili waweze kurudisha angalau nusu ya walizotapeliwa.
Watanzania fanyeni Kazi acheni kupenda urahisi hivi ushasikia nani katajirika kupitia upuuzi huu
 
Nimeona ipo haja ya kukujibu hatua kwa hatua, sio kwa maana ya ushindani, bali kufahamishana.

Nimeshatolea maelezo kuhusu kwa nini biashara hii sio ponzi lakini kwenye uzi wangu hapa nitarudia tena kutolea maelezo ya kina kukujibu.

Kwanza ponzi scheme kama vile DECI hazina biashara yoyote zinazozifanya kuzalisha. Zinatumia hela zilizolipwa na watu waliojiunga mwanzoni kulipia watu waliojiunga baadaye.

Ndicho kinachofanywa na tovuti hii pia. Ushahidi upo wazi kwa asiye mvivu kutafiti.

BtcClock ni tovuti inayoendeshwa na kampuni ya Lucky Times Ltd iliyosajiliwa Kemp House, 160 City Road, London, London, United Kingdom, EC1V 2NX mnamo 15th March, 2017.

Tupe majina ya board of directors na anuani zao halisi (sio virtual addresses).

Kampuni inatumia Bitcoin Technology kufanya biashara ya Bitcoin Mining kama ilivyoelezea kwenye mission statement yake. Shughuli zake zilizoorodheshwa kwenye Registration yake ni Computer facilites management activities, data processing, hosting and related services na web portals.

Bitcoin mining sio rocket science. Inahitaji uwekezaji kwenye vifaa kama powerful processors na umeme. Sasa hebu onesha hiyo kampuni imewekeza nini mpaka sasa. Hosting ipi wanayofanya hawa? Hebu tuoneshe kama kweli wanafanya web hosting.

Kwa hiyo utaona kwamba kampuni ina shughuli halali inazozifanya ikiwa ni pamoja na shughuli kuu ya kutumia Bitcoin Technology ili ku mine Bitcoins na cryptocurrenices zingine, shughuli ambayo inaiingizia pesa ambazo wanatumia pesa hizo kulipia gharama za uendeshaji biashara kama vile machine za ku mine cryptocurrencies, wafanyakazi, kuendesha tovuti (server costs, etc.), kulipia profit wanazotoa kwa wawekezaji wao ambapo wanalipa 3.84% kwa siku, kulipia matangazo ya biashara yao (kupitia 15% commission wanazotoa kwa affiliates wao) na kubakia na faida ya kampuni.

Affiliate commission ndio biashara kuu vinginevyo uthibitisje hayo hapo juu. Kwa kukusaidia tu, jaribu kutafuta Genesis bitcoin mining wakongwe wa biashara hii, uone ilivyo vigumu hata kurejesha tu mtaji wako. Hawa wanaotoa flat rate 3.84% hata wauza madawa ya kulevya hawawezi kukupa guarantee hiyo. Hiyo ni indicator ya fraud!

Mtaji wa kuendeshea biashara yao wanaupata kupitia hela zinazowekezwa na wanachama wao pamoja na hela zao wenyewe walizowekeza.

Labda useme kwamba kwa sasa wako kwenye steji ya kutafuta mtaji kutoka kwa wanachama maana kampuni yao mpaka sasa imewekeza mtaji sifuri!

Hivyo huwezi kuiita kampuni hii kuwa ni Ponzi scheme kwa sababu haitumii hela za waliolipa mwishoni kuwalipa waliojiunga mwanzoni bali wanatumia hela za wawekezaji (investors) pamoja na hela zao kufanyia shughuli yao ya ku mine cryptocurrencies kisha wanarudisha hela za wawekezaji pamoja na faida yao pamoja na kulipia gharama za uendeshaji na kubakia na faida kutoka kwenye hela walizotengeneza kupitia shughuli ya ku mine Bitcoins pamoja na shughuli zingine.

upload_2017-7-1_9-51-4-png.533435


Tukija kwenye suala la HYIP ulilolitolea mfano hapo juu, kwanza huo mfano hauendani kabisa na biashara hii kwa sababu biashara hii hailipi faida kiasi hicho kama ulivyoelezea hivyo si sahihi kuilinganisha biashara hii na mfano wako.

HYIPs zinakuja kwa sura mbalimbali, haziji zikijitangaza kwa mba ni HYIPs. Fungua macho.
upload_2017-7-1_11-0-39.png



Pili linakuja suala la kujiuliza je faida ya 3.84% wanayotoa kwenye watu wanaowekeza biashara hii ni nyingi? Ukiangalia biashara tunazozifanya na tulizozizoea, jibu ni kwamba kweli faida ni nyingi mno wanayotoa kwa siku. Lakini ukiangalia kwa jicho la biashara inayofanyika ya ku mine cryptocurrencies, hiyo faida ni ya kawaida kwa sababu bado watu wengi duniani kote hawajaanza kuwekeza au kutumia hizi cryptocurrencies hivyo fursa (opportunity profile) bado zipo nyingi za kutengeneza faida kubwa unapofanya biashara ya mining. Kadri watu watakavyozidi kuongezeka kuzitumia na kuwekeza kwenye hizi cryptocurrencies basi ndivyo thamani ya hizi cryptocurrencies itakapoongezeka na wakati huo huo shuhguli ya ku mine itakavyozidi kuwa ngumu na hivyo kupunguza faida wanayopata wafanyabiashara wanao mine cryptocurrencies.

Umedanganywa kwelikweli. Cryptocurrency mining haijaanza jana. Lakini ni ngumu sana kupata faida kwa sababu ya gharama za uendeshaji.

Kwa hiyo kwa mtazamo wa kibiashara ni kwamba kampuni hii inatengeneza faida kubwa sasa hivi kwa sababu biashara inalipa hivyo watu wanaoichangamkia sasa hivi wakati bado inalipa ndio watakaovuna vya kutosha na kutumia mavuno yao kuwekeza kwenye miradi mingine ili faida itakaposhuka basi watafidia kushuka kwa faida ya biashara hii kwa kupata faida kutoka kwenye biashara zingine.

Nope. Wewe ndio biashara.

Hivyo watu ninawashauri kuhusu kufanya biashara hii siishii kuwaacha tu mara baada ya wao kuwekeza bali nasubiri wakishaanza kupata matunda ya biashara hii basi nawapa mkakati wa kutoa sehemu ya faida wanayopata kwenye mradi huu ili kuwekeza kwenye maeneo mengine.

At your own risk people. Unapowekeza kwenye HYIP wekeza kiasi ambacho uko radhhi kupoteza.

Mtazamo mwingine ni kwamba kweli hii ni kampuni ya kitapeli na itapotea mda si mrefu. Sikatai kwamba kampuni hii inaweza kuwa ya kitapeli. Lakini ninachosema ni kwamba hata kama ikiwa ni ya kitapeli, nilishafanya home work yangu kuichunguza kabla sijajiunga kama nilivyoelezea hapo awali nikaona kampuni haina jina baya lolote kutoka kwenye reviews zilizopo kwenye public domain baada ya ku search kwa kutumia Google. Hakuna hata reviewer mmoja aliyetoa ushahidi kwamba kampuni hii ni ya kitapeli. Wote wameelezea kwamba hakuna kitu walichokiona chenye kuashiria kwamba kampuni hii ni ya kitapeli ingawa baadhi yao wametoa wamesema kwamba ina dalili ya kuwa kampuni ya kitapeli.

Hujui jinsi ya kutambua hyips. Kila kitu kipo wazi.

Mwisho ningependa kuchukua fursa hii kukushauri Nyenyere kwamba unapokuja na hoja ya kudai kwamba kampuni fulani ni ya Ponzi scheme basi jikite kujenga hoja kitaalam kwa nini unadhani kampuni hiyo ni ya ki Ponzi. Unapotumia mfano wa kampuni nyingine na kuacha kutumia mifano ya kampuni unayoishambulia kwamba ni Ponzi scheme huo ni utoto.

Asante kwa maoni yangu. Ila ukweli umeupata. Kama wewe sio mtoto njoo sasa na constructive criticism hapa. I rest my case.
 

Attachments

  • upload_2017-7-1_11-1-7.png
    upload_2017-7-1_11-1-7.png
    49 KB · Views: 52
Siyo kila kitu mtandaoni ni utapeli, kuna mengi sana ya ukweli na mengi sana ya uongo.
Na ukitaka kujua kuwa ni uongo ni pale unapoambiwa eti ufanye investment ya wiki moja na kisha utavuna pesa nyingi Sana.
Hakuna investment ya wiki au mwezi mmoja tu na ukapata pesa nyingi.
Tatizo hata wewe unaonekana kabisa kuwa hujui ulichoandika, umekimbilia tu kusema utapeli bila kusema Kama na ukweli huwa upo pia .
sidhani Kama Unajua lolote kuhusu cryptocurrency business au digital coins.
Kwanza lazima ujue kuwa, siye watanzania bado tunaishi karne ya 18 wakati wenzetu wapo karne ya 21.
Ngoja nikusubirie ulete mada Kwa kina ili na Mimi nikukosoe Kwa kina tena na ushahidi ,sidhani Kama utaweza kuleta ushahidi wa kutosha japokuwa ni kweli ponzi Zipo ila umechemka kuegemea upande mmoja tu.
Nasubiri hekima zako wiseboy.
 
aisee,,mi nimekuelewa vyema mkuu Nyenyere tatizo watu wanapenda sana easy money while there is no easy money in this world,,kuna matapeli wengine wanajiita biko wapo wanawapiga tu wajinga wajina
 
na hawa wanaojiita H2I Helping handsinternational international na wenyewe sio matapeli kweli!
 
Ni lazima uite matakataka Kwa Sababu, umezaliwa Tanzania, umekulia Tanzania, umesoma Shule zilizopitwa na wakati Tanzania.
Dunia ipo karne ya 21 ,wewe unaishi maisha ya karne ya 18.
Dunia ina mambo mengi sana usiyoyajua lakini wewe umekariri kilimo na ufugaji, sasa mambo ya cryptocurrency utayajulia wapi wewe?
Na ni bora ukae hivyo hivyo maana mkijanjanjaruka wote tutatoa wapi wafanyakazi siye mabilionea tujao?
Hahaaa dah mkuu taratibu bwana dah nimecheka sana aisee. For sure asiye ijua cryptocurency kwa ulimwengu huu ni ngumu kukuelewa na ndiyo maana hata mabank yamekuwa yakianza kujikanyaga kanyaga baada ya watu kugundua chimbo la cryptocurency. Maana hii ni njia ya kuua mabank kama ambavyo mabadiriko ya internet juu ya email kulivyo ua shirika la posta. Ni vile tu bado watz akili zimo kwe chungu ila wenzetu mbele bank zao zimeaccept bitcoin na wana ATM zake kabisa.
 
Hebu ona mmoja huyu

Good evening guys, I came to make a super ALERT against TRADE COIN CLUB, a multilevel system that is messing with the name of BITCOIN!
I was invited to invest in this "company", of course no one should invest in the dark, so I went to search for information, so I put it on Google, appeared sites talking badly about the company on the day marked where they would explain me better about TRADE COIN CLUB, they explained to me that I would get 50% of everything I came in (stirring up the profit of the crowd), I then asked why so many people complaining then I heard "If you only complain about blame!" Blockchaing¨ and use the name of bitcoin to promote themselves, the owner of TRADE COIN CLUB and DOVER BRAGA!
Searching the net I could find several processes, and complaints, and countless people deceived talking badly of Bitcoin, after all they were deceived, not even shot the reason of them! So people, let's denounce! Put your mouth on the trombone! LET'S NOT LET THE NAME OF OUR TAO BELOVED BITCOIN!
BITCOIN IS SOLUTION, NOT DESTRUCTION!
Mmmmhhh sasa kwanini wanasema watrade bitcoin.

Heri kuwa mkulima tuuu upatu kila siku majanga
 
Jaman nialipia hashflare.io kwa kutumia visa card yng lkn kule hashflare.io wanasema invalid purchase nan anajua njia ingene ya kulipa au mtu anaeweza tukakutana nkampa cash anilipie
 
Back
Top Bottom