Halmashauri zina mafungu ya kuwasomesha watumishi wao, ni kweli! Hata hivyo watumishi wanaohitaji kujiendeleza kimasomo ni wengi sana na ni katika ngazi tofauti tofauti.
Wapo wanaojiendeleza katika ngazi ya shahada, ambao hawana 'sifa' za kupata mkopo wa Bodi. Zaidi ya hao, wapo wale ambao wanajiendeleza katika ngazi za Stashahada na cheti, hawa wote hawana chao toka Bodi. Kwa ufupi, hawa ndiyo hasa walengwa wa mafungu ya Halmashauri wanazozitumikia!
Kwa maelezo haya mafupi, naungana na wale wanaopinga Bodi kuwanyima mkopo watumishi. Sababu zangu ni hiz zifuatazo:-
1. Watumishi wanaokopeshwa na Bodi hawana haki ya kupata msaada wowote wa kimasomo toka Halmashauri (kwa mujibu wa sheria)
2. Tamko la Halamashauri kutakiwa kuwakopesha watumishi wanaojiendeleza limetolewa kwa kuchelewa sana (mimi nimelisikia mwezi wa nane, na hata hivyo halikuwa rasmi). Bajeti za Halmashauri zinapaswa kuwa zimekamilika na kupitishwa mwezi Machi!
3. Watumishi hawa ni walipa kodi kama walivyo watanzania wengine!
Kwa mtazamo wangu, huu ni mkakati maalumu (haramu) wa baadhi ya wenye madaraka kuwazuia watumishi wa umma wasipate nafasi ya kujiendeleza ki masomo! Wasipofanikiwa katika hili, watakuja na mkakati mwingine, yangu macho!