Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Beki wa kati wa Simba SC Erasto Nyoni baada ya Timu ya Majimaji ya Songea kukwama jijini Dar es Salaam kwa kukosa pesa ya nauli na deni la Hoteli juzi alifanikiwa kuwasaidia kulipa na kuwapa Tsh. Milioni moja ambayo wamefanya nauli ya kurejea Songea.
Erasto ni Mwenyeji wa Songea na ameongea na Ayo Tv kwa njia ya simu na kueleza kuwa amewahi kupita hali kama hiyo, hivyo ameamua kuwapa support ili kuwatia moyo.
“Sisi kama Kaka zao tunatakiwa tuwaoneshe na tuwape moyo ili waweze kupambana maana kazi yetu ya mpira ni kazi ngumu sana unatakiwa usikate tamaa uwe Mvumilivu sasa uvumili hauji tu hivihivi lazima kuna Watu wawe wanakupa hiyo nguvu”
“Nimeshawahi kupitia hii hali ndio maana ilipotokea ikanisukuma ikanisukuma kufanya hivi kwasababu imeshwhi kunitokea”
Chanzo: Millard Ayo