Erasto Nyoni asaidia kuwalipia nauli MajiMaji ya Songea

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Beki wa kati wa Simba SC Erasto Nyoni baada ya Timu ya Majimaji ya Songea kukwama jijini Dar es Salaam kwa kukosa pesa ya nauli na deni la Hoteli juzi alifanikiwa kuwasaidia kulipa na kuwapa Tsh. Milioni moja ambayo wamefanya nauli ya kurejea Songea.


Erasto ni Mwenyeji wa Songea na ameongea na Ayo Tv kwa njia ya simu na kueleza kuwa amewahi kupita hali kama hiyo, hivyo ameamua kuwapa support ili kuwatia moyo.

“Sisi kama Kaka zao tunatakiwa tuwaoneshe na tuwape moyo ili waweze kupambana maana kazi yetu ya mpira ni kazi ngumu sana unatakiwa usikate tamaa uwe Mvumilivu sasa uvumili hauji tu hivihivi lazima kuna Watu wawe wanakupa hiyo nguvu”

“Nimeshawahi kupitia hii hali ndio maana ilipotokea ikanisukuma ikanisukuma kufanya hivi kwasababu imeshwhi kunitokea”

Chanzo: Millard Ayo
 
Hongera sana legend ila ligi yetu kazi bado ipo kwanza nikiangaliaga tu ofisi za TFF moyoni najisemea bora kumpeleka shule mwanao kuliko academy za mpira hapa bongo
 
Hongera sana legend ila ligi yetu kazi bado ipo kwanza nikiangaliaga tu ofisi za TFF moyoni najisemea bora kumpeleka shule mwanao kuliko academy za mpira hapa bongo
Kiujumla huko kote kwenye michezo na sanaa tunapuyanga tu. Kama nchi hatujafanya maamuzi ya dhati kuinua hiyo sekta na nadhani najua kwa nini. Ni juhudi za watu binafsi tu ndiyo zimesukuma hadi hapa tulipo.
 
Na hii timu imezid Sasa

Hi n Mara ya pili kuchangiwa na wahisani hapa.mjini

Kuna mwaka kipind wapo daraja la kwanza basi lao.lilikamatwa na wachezaj mabeg yao yalidakwa na mwenye hoteli had walipe bills zote
 
Mbunge wao si huyu somebody Ndumbalo,huyu jamaa ni kanji balaa,hanaga time,Ndumbalo aibu hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…