HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
Rais wa Uturuki, RecepTayyip Erdogan amefanya mazungumzo na Rais wa Urusi Vladmir Putin na kujadili namna ya kuboresha mahusiano kati ya mataifa yao
Katika mazungumzo yao ya Jumamosi, yaliyofanyika kwa njia ya simu, viongozi hao wamejadili pia juu ya yanayoendelea katika vita nchini Ukraine.
Rais Erdogan katika mazungumzo hayo ameelezea umuhimu wa kuumaliza mzozo kati ya Urusi na Ukraine kwa njia ya mazungumzo haraka iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Uturuki, Erdogan amemshukuru pia Rais Putin kwa mtazamo wake chanya katika kuurefusha mkataba wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi.
Chanzo: RTRE