SoC01 ERGONOMICS: Watu wengi wanaumia kwa kukosa Elimu hii

SoC01 ERGONOMICS: Watu wengi wanaumia kwa kukosa Elimu hii

Stories of Change - 2021 Competition

cilla

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2011
Posts
372
Reaction score
299


ergonomicOffice-1187582517-770x553-1-650x428.jpg


UTANGULIZI.

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na changamoto kubwa ya watu wengi kupata maumivu ya viungo sehemu mbalimbali za mwili. Zipo sababu nyingi zinazosababisha watu kupata matatizo ya kumwa viungo vya mwili lakini sababu moja wapo ni ukosefu wa elimu ya Ergonomics.Kwa bahati mbaya sijaweza kujua kwa Kiswahili neno hili linaitwaje.
ERGONOMICS NI NINI?

Ergonomics ni sayansi ya ubunifu wa namna ya ufanyaji kazi kwa kuzingatia usalama wa mfanyakazi unaoweza kusababishwa na mazingira ya kazi au vifaa anavyotumia.Ergonomic humsadia mfanya kazi kuwa confortable na kuongeza uzalishaji .

Neno 'ergonomics' lilibuniwa mnamo 1949 na K. F. H Murrell Neno 'ergonomics' liliundwa mnamo 1949 na K. F. H Murrell kwa kuunganisha maneno mawili ya Kiyunani, εργον (ergon), linalomaanisha 'kazi', na νομος (nomos) maana yake 'sheria'. Ergronomic lilikuja kuwa maarufu mnamo 1950 wakati lilipotumika kwenye jina la taasisi ya 'Ergonomics Research Society' (Kwa sasa inajulikana kama Chartered Institute of Ergonomics and Human Factors).

KWA NINI ELIMU YA ERGONOMICS NI MUHIMU?

Ergonomics ni muhimu kwa sababu ikiwa utafanya kazi na mwili wako uko stressed umechoshwa na mkao mbaya, joto kali, au matendo yanayojirudia rudia mfumo wa misuli(musculoskeletal system) huathirika. Mwili wako unaweza kuanza kuwa na dalili kama vile uchovu, kukosa utulivu, na maumivu, ambayo inaweza kuwa ishara za kwanza za ugonjwa wa maumivu ya misuli (musculoskeletal disorder).Ugonjwa wa shida za misuli au musculoskeletal disorder (MSDs) ni hali inayoweza kuathiri misuli ya mwili, viungo, tendon, mishipa, mifupa na neva.

Mara nyingi ugonjwa huu (MSD) huanza taratibu na kukua pole pole na husababishwa na kazi zenyewe au mazingira ya kazi
. Mtu mwenye tatizo hili anaweza kusababisha ajali, Mfano kuvunja au kuangusha kitu. Kwa kawaida, MSD huathiri mgongo, shingo, mabega na mikono; mara chache huathiri miguu(Leg}.

Mara nyingi ugonjwa huu wa shida ya misuli huwa na hatua tatu:

  1. kukosa utulivu (discomfort).unaweza ukajikuta ukikaa huoni kama uko sawa unajihisi viungo au sehemu ya maungio(joints) zinahitaji kunyooshwa nyooshwa.kama ni tatizo katika shingo unaweza kujikuta unaigeuza geuza yaani unaona kama misuli yake haiko sawa. Na kwa wakati mwingine unaweza kuhisi kupata ganzi kwenye maungio ya viungo vya kwenye mikono miguu au shingo.
  2. Maumivu madogo.( minor aches).Kwa mbali sana mtu huanza kuhisi maumivu kwenye sehemu za mwili uti wa mgongo, kiunoni, nyuma ya mabega, shingo n.k.
  3. Maumivu (pains) hadi hali mbaya zaidi za kiafya zinazohitaji muda wa kupumzika kazini na hata matibabu. Katika hali sugu zaidi, matibabu na urejesho mara nyingi hayaridhishi – matokeo, inaweza kuwa ulemavu wa kudumu na kupoteza ajira.

WATU AMBAO WAPO HATARINI KUPATA TATIZO HILI
  1. Madereva hasa wanaoendesha safari ndefu.Madereva wengi wanapata tatizo la kuumwa uti wa mgongo kwasababu ya mazingira yao ya kazi hasa viti.
  2. Wanaokaa ofisini muda mrefu.Kukaa muda mrefu bila kunyanyuka na kujinyoosha kidogo au kiti anacho kalia kutokuwa na sifa.
  3. Wanaokaa kwenye computer muda mrefu.Wanaokaa muda mrefu kwenye computer kama katibu mahususi(secretary).
  4. Wanaonyanyua vitu vizito.Wanaobeba mizigo ,mafundi na watu wa kawaida katika kuhamisha au kusogeza kitu kizito.
  5. Pia wanafunzi.
DONDOO CHACHE YA NAMNA YA NAMNA YA KUEPUKA TATIZO HILI
  1. Unyanyuapo kitu kizito usitumie uti wa mgongo kusapoti mikono (usinyanyue kwakubend mgongo).Tumia nguvu za miguu kwa kuchuchumaa kisha unyanyuke na mzigo.Vinginevyo unaweza kuumiza uti wa mgongo au kiuno.Wale ambao hupenda kunyanyua vitu vizito gym wanapaswa kunyanyua kwa mfano huu.
1627058187957.jpeg





2. Hakikisha kiti unachokalia kazini , ofisini, kwenye gari kina sapoti uti wa mgongo vizuri.Hasa juu kidogo ya kiuno.


1627058684967.gif
1627058809250.png

1627058958619.png

1627059085072.png
1627059168001.jpeg
1627059373598.jpeg




3. Unapotembea umebeba mzigo tembea kwa kunyooka.

1627059696068.jpeg



4. Unapotafuta kitu chini au unaposogeza kitu chini ogopa kupinda uti wa mgongo , njia nzuri ni kuchuchumaa au kutanua miguu wakati wakuokota au kusogeza. .
1627125286293.png
1627125565342.jpeg



5. Usilalie mto mgumu na mrefu kuepuka shingo yako kupata jeraha la misuli.

1627125851755.jpeg
1627125950262.jpeg
1627126134167.png



6. Kuepuka maumivu ya shingo uzitumie simu au laptop ukiwa katika mkao mbaya .

1627126480477.jpeg
1627126814399.jpeg
1627126986326.png
1627127367179.png



NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI YA ERGONOMIC YATAKAYOWEZA KUSAIDIA KUEPUKANA NA TATIZO LA MUSCULOSKELETAL DISORDER (MSDs) HASA WANAOKAA MUDA MREFU MAOFISINI, WANAFUNZI NA WALE WANAOFANYA KAZI YA KUBEBA VIFURUSHI AU MIZIGO.Nitakuonyesha kwa njia ya picha ili kupunguza maelezo na pia uweze kuelewa haraka.
YAFUATAYO NI MAZOEZI UNAYOWEZA KUFANYA NYUMBANI AU OFISI

1627128816658.jpeg
1627129382548.jpeg
1627128834608.jpeg

1627134080063.jpeg
1627134170677.jpeg

FAIDA YA KUTUMIA ERGONIMIC KATIKA SHUGHULI ZAKO

(1) Inaongeza morali/hari yakufanya kazi
(2) Inaongeza ufanisi wa kazi
(3) Inapunguza uwezekano wakupata maumivu ya viungo na misuli ya mwili
(4) Inapunguza uwezekano wakusababisha ajali
(5) Inapunguza uchovu na msongo usio wa lazima
(6) Inakuepusha na gharama za matibabu


KINGA NI BORA KULIKO TIBA TUCHUKUE HATUA





1627059218336.png


1627060123996.jpeg


1627126628386.jpeg


1627126757065.jpeg


1627127277533.png


1627129654988.jpeg


1627129696691.jpeg
 
Upvote 6
Very nice niliishawahi kuambiwa hata Wale wanaotumia kompyuta muda mrefu wanapaswa kuwa na short breaks away from the computer ili kupunguza effect kwenye macho; eye strain injuries,, you have my vote mkuu
 
Nipo natoa mafunzo ya Usalama Na Afya Mahali Pa Kazi na nimefundisha kuhusu vihatarishi vya Kierigonomia (Ergonomic Hazards).

Umefanya Vyem akuliangazia Suala hili na ni muhimu si kazini tuu Bali katika Maisha Yetu ya kila siku.

Chochote tufanyacho tuzingatie Erigonomia.

Erigonomia Ni Uhusiano wa Mtu na Kitendea kazi.
 
Shukrani
Nipo natoa mafunzo ya Usalama Na Afya Mahali Pa Kazi na nimefundisha kuhusu vihatarishi vya Kierigonomia (Ergonomic Hazards).

Umefanya Vyem akuliangazia Suala hili na ni muhimu si kazini tuu Bali katika Maisha Yetu ya kila siku.

Chochote tufanyacho tuzingatie Erigonomia.

Erigonomia Ni Uhusiano wa Mtu na Kitendea kazi.
 
Very nice niliishawahi kuambiwa hata Wale wanaotumia kompyuta muda mrefu wanapaswa kuwa na short breaks away from the computer ili kupunguza effect kwenye macho; eye strain injuries,, you have my vote mkuu
Shukrani
 
Back
Top Bottom