Katibu Mkuu wa CCM (Kinana) ana kampuni ya ISP - internet service provider kwa jina la WIA, Eric Mwenda yupo pale kama CEO na inasemekana amepewa shares. Ni kijana very sharp na aliye elimika vizuri nje (canada). Amejifunza aina hii ya biashara kupitia kwa rafiki yake wa karibu aitwaye rashid shamte, CEO wa sixtelecoms. Rashid aliporudi kutoka nje masomoni alibahatika kukutana na peter noni (DAP wa BOT wakati wa balali, hivi sasa CEO wa Tanzania Investment Bank). Shamte akafanikiwa kumshawishi peter noni kufungua biashara ya telcoms na baadae eric mwenda aliporudi kutoka canada akaajiriwa na shamte kwa muda mrefu kabla ya yeye pia kumpata peter noni wake (kinana).
Vijana hawa wawili kwa sasa wana mafanikio makubwa sana kifedha. Fursa kama zao bado zipo hasa pale vijana wanapopata bahati ya kuwa karibu na pia kuaminiwa na vigogo wa CCM wenye fedha lakini ambao hawana idea on how to invest it in today's knowledge driven global economy.