Eric Shigongo, adui mkubwa wa Hiphop Bongo

Eric Shigongo, adui mkubwa wa Hiphop Bongo

N'gwanantugwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2015
Posts
347
Reaction score
345
Mwaka 2005 lilifanyika shindano kubwa lililobatizwa jina la Mfalme wa Rhymes chini ya mdau, mmiliki na Mkurugenzi wa magazeti ya Global Bwana Shigongo. Shindano liliendeshwa na magazeti kwa kuweka picha za wasanii wengi kisha wasomaji na mashabiki kuchagua nani anatakiwa kuingia hatua ya kumi bora. Hatua hii ilikuwa ndio fainali. Wasanii 10 walifanya onyesho kwa pamoja na mshindi wa kwanza hadi watatu walipatikana siku hiyo ya onyesho. Ukiacha malalamiko yaliyotokea baada ya Suleiman Msindi kupewa taji, shindano hilo lilikuwa la kizushi haswaa.

Mwaka uliofuata yaani 2006 shindano halikufanyika japo maandalizi ya kijizi yalikuwa yashakamilika. Wawekezaji wakubwa walikuwa washadhamini na hatua ya kumi bora ilikuwa ishafikiwa.

Wasanii waliopendekezwa ni; Wagosi wa Kaya, Prof. Jay, Jay Moe, Hayati Mangwear, Ferouz, Fid Q, D. Knob, Ditto, Mike Tee na Dataz.

NINI KILIKWAMISHA ONYESHO NA SHINDANO HILO?

Ubabaishaji wa mdau ndo ulisababisha shindano hilo kuvunjika. Ili apate faida kubwa akaandaa zawadi ya mshindi wa kwanza Sh. Milioni 8, Mshindi wa pili milioni 3.5 na mshindi wa tatu milioni 1.5. Waliobaki ilitakiwa wapewe Sh. laki 2.5 kama kifuta jasho na maandalizi ya onyesho. Pengo hili la mgawanyo wa zawadi lilifanya wasanii waweke kikao peke yao bila kuwashirikisha wadau waandaaji. Walifikia uazi kuwaandikia barua wadau hao ili wabadili vipengele vya shindano hilo.

Ili kwenda sawa na hali halisi waliamua waongezewe pesa kutoka laki 2.5 kifuta jasho hadi milioni 2.5 kitu ambacho kilikuwa kinawezekana kwa udhamini mkubwa waliokuwa nao waandaaji. Hisia za kuandaliwa washindi kabla ya shindano pia ilijidhihirisha pale baadhi ya wasanii watatu (inasemekana waliandaliwa ushindi) hawakuonekana kutoa mchango wao kwenye harakati za kuomba maslahi yaongezeke.

Ni dhahiri shindano hili halikuwa na nia ya kuwafaidisha wasanii bali lilimfaidisha Shigongo na wadau wake wa pembeni. Shindano lilifanikiwa kuzima sauti za wanaharakati waliokuwa wameandaliwa ushindi ila ukweli ukabaki palepale. Hasara aliyoipata Shigongo ilihamia kwa wasanii waliokuwa wametangaza kufa au kupona kusimamia misimamo yao. Shigongo aliyewapa kick watangazaji na matamasha ya Radio flani gazetini alianza kuacha kuandika harakati za wana na wana wakabaniwa Radioni huku wasanii wasiojua kuimba wala kughani wakawa ndo kivutio kwa mdau huyu. Kuanzia miaka hiyo

Mziki wetu mpendwa wa hip hop ukakosa rafiki, ukaongeza idadi ya maadui hasa watu walipozidi kueleza ukweli na uhalisia wa maisha yao katika tungo zao.

Ukweli unachukiwa, ndo maana vyombo vya habari vinalazimisha watu watoke kwenye misingi waimbe starehe, mapenzi na anasa.. ADUI wa kwanza katika harakati hizi za kueneza ukweli ni huyu Msukuma mwenzangu, Shigongo. CCM wanampoteza, Wananchi anawapoteza ila Hip Hop hawezi kuipoteza japo anataka iwe hivyo...

Kila siku anaandika habari za mashoga na kuandika habari mbaya tu za wanaharakati ila nzuri haandiki......
 

Attachments

  • 1430051678253.jpg
    1430051678253.jpg
    15.5 KB · Views: 462
Ushindi wake ulizua mjadala hadi kaka mkubwa SOLO THANG akahisi anagundu kwenye nyimbo ya KILIO​ CHANGU
 
Nilishawahi kusema hapa shigongo ni mnafki tena mnafki mno...muongo na uongo wake wakuwadanganya watanzania eti Mungu kampa mali.ha ha ha ha ha...eti namafunzo ya ujasiriamali anatoa kwa wajasiriamali watanzania....pole shigongo,kamdanganye mjinga asiyejua misingi ya vyanzo vyako...
 
Masahihisho kodogo. Hip-hop sio muziki, hili kosa wengi tunalifanya sana. Ni utamaduni unahusisha vitu kadhaa, kati ya hivyo ni Rap ambayo ndio muziki.
 
ndo fitna za mziki zilivyo
ni
mziki ni kazi na watu wamepoteza vingi kwa sababu ya wito waliovuviwa na mungu....mziki bila fitna mafanikio huwepo.....tofauti na hapo wasanii wachache watafaidika ila wengi watatabika
 
masahihisho kodogo. Hip-hop sio muziki, hili kosa wengi tunalifanya sana. Ni utamaduni unahusisha vitu kadhaa, kati ya hivyo ni rap ambayo ndio muziki.
nguzo ya mc huwezi kuitenga na muziki........hata asili ya utamaduni ulianza na dj ku loop muzik,ndipo mc,michoro na wavunjanji wakafuata.....
 
nilishawahi kusema hapa shigongo ni mnafki tena mnafki mno...muongo na uongo wake wakuwadanganya watanzania eti mungu kampa mali.ha ha ha ha ha...eti namafunzo ya ujasiriali anatoa kwa wajasiriamali....pole shigongo,kamdanganye mjinga asiyejua chanzo....
mungu anajua ukweli wote....hata akivaa ngozi ya kondoo hataondoa ukweli kuwa yeye ni chui mwenye makali ya simba........
 
nguzo ya mc huwezi kuitenga na muziki........hata asili ya utamaduni ulianza na dj ku loop muzik,ndipo mc,michoro na wavunjanji wakafuata.....
Hip-hop inaundwa na nguzo kuu 4; Emceeing, Break-dancing, Deejaying, pamoja na Graffiting. Je, graffiti ni aina ya muziki?
 
hip-hop inaundwa na nguzo kuu 4; emceeing, break-dancing, deejaying, pamoja na graffiting. Je, graffiti ni aina ya muziki?
hip hop ni dhana pana sana ,michoro ilikuwepo hata kipindi cha babu zetu....kumbuka kila nguzo inakazi yake katika ushereheshaji....leo hii tusingekuwa tunaongelea hip hop kama dj,mc na wavunjaji ukiwatoa.....hata jina la hip hop limetoka kwa ma mc au waghanaji kwa kiswahili.....chata inakazi yake na mic ina kazi yake....huwez kuvitofautisha kwenye kufikisha ujumbe uliokusudiwa.....wapo wanamapinduzi hawakufanya muziki ila wanaheshimika kwa zao itikadi
 
Wengine wananirubuni eti nashindania gari...
Kumbe wameshapanga wampe nani toka awali...
Sitorudia kosa hata zawadi waweke meli waongeze ghorofa mbili wanikabidhi na shell...!
 
hip hop ni dhana pana sana ,michoro ilikuwepo hata kipindi cha babu zetu....kumbuka kila nguzo inakazi yake katika ushereheshaji....leo hii tusingekuwa tunaongelea hip hop kama dj,mc na wavunjaji ukiwatoa.....hata jina la hip hop limetoka kwa ma mc au waghanaji kwa kiswahili.....chata inakazi yake na mic ina kazi yake....huwez kuvitofautisha kwenye kufikisha ujumbe uliokusudiwa.....wapo wanamapinduzi hawakufanya muziki ila wanaheshimika kwa zao itikadi
Ndio nachosema pia brother. Kimsingi, hip-hop ni utamaduni unaohusisha sanaa mbali mbali, kama tulivyokwisha-zitaja mara kadhaa hapo.

Point yangu ni, si sahihi kusema Hip-hop ni muziki, kwa sababu wapo watu mbali mbali ambao hawajawahi kujihusisha na muziki ila wanatambulika kama wana-hip-hop, kwa sababu wanafanya sanaa zingine zinazokamilisha hip-hop.
 
Ndio nachosema pia brother. Kimsingi, hip-hop ni utamaduni unaohusisha sanaa mbali mbali, kama tulivyokwisha-zitaja mara kadhaa hapo.

Point yangu ni, si sahihi kusema Hip-hop ni muziki, kwa sababu wapo watu mbali mbali ambao hawajawahi kujihusisha na muziki ila wanatambulika kama wana-hip-hop, kwa sababu wanafanya sanaa zingine zinazokamilisha hip-hop.
uko sawa kabisa kaka,HUU Mjala wa dhana ya nguzo za hip hop tutauchambua zaidi siku zijazo,tujadili maadui wa harakati hizi zenye msingi wa kusema kweli kwa kutumia uwezo wa Mungu
 
Adui wa hip hop ni mashabiki na wana muziki wenyewe.
Mashabiki ni kuwasingizia....ndio maana kwenye show hujawahi kusikia mtu wa HIP HOP kazomewa....wasanii wanakutana na changamoto ambazo kuongea wanashindwa kwa kuhofia kukosa hata kile kimkate kinachowapeleka haja....wamefungwa midomo na wadau wenye kiu ya kujitajirisha TOFAUTI NA HAPO NI HABARI ZA MAPAMBO......OOH!!!!! HUYU TAJIRI...... HUKU VITEGA UCHUMI HAVIJULIKANI.......BONGO
 
Back
Top Bottom