N'gwanantugwa
JF-Expert Member
- Apr 25, 2015
- 347
- 345
Mwaka 2005 lilifanyika shindano kubwa lililobatizwa jina la Mfalme wa Rhymes chini ya mdau, mmiliki na Mkurugenzi wa magazeti ya Global Bwana Shigongo. Shindano liliendeshwa na magazeti kwa kuweka picha za wasanii wengi kisha wasomaji na mashabiki kuchagua nani anatakiwa kuingia hatua ya kumi bora. Hatua hii ilikuwa ndio fainali. Wasanii 10 walifanya onyesho kwa pamoja na mshindi wa kwanza hadi watatu walipatikana siku hiyo ya onyesho. Ukiacha malalamiko yaliyotokea baada ya Suleiman Msindi kupewa taji, shindano hilo lilikuwa la kizushi haswaa.
Mwaka uliofuata yaani 2006 shindano halikufanyika japo maandalizi ya kijizi yalikuwa yashakamilika. Wawekezaji wakubwa walikuwa washadhamini na hatua ya kumi bora ilikuwa ishafikiwa.
Wasanii waliopendekezwa ni; Wagosi wa Kaya, Prof. Jay, Jay Moe, Hayati Mangwear, Ferouz, Fid Q, D. Knob, Ditto, Mike Tee na Dataz.
NINI KILIKWAMISHA ONYESHO NA SHINDANO HILO?
Ubabaishaji wa mdau ndo ulisababisha shindano hilo kuvunjika. Ili apate faida kubwa akaandaa zawadi ya mshindi wa kwanza Sh. Milioni 8, Mshindi wa pili milioni 3.5 na mshindi wa tatu milioni 1.5. Waliobaki ilitakiwa wapewe Sh. laki 2.5 kama kifuta jasho na maandalizi ya onyesho. Pengo hili la mgawanyo wa zawadi lilifanya wasanii waweke kikao peke yao bila kuwashirikisha wadau waandaaji. Walifikia uazi kuwaandikia barua wadau hao ili wabadili vipengele vya shindano hilo.
Ili kwenda sawa na hali halisi waliamua waongezewe pesa kutoka laki 2.5 kifuta jasho hadi milioni 2.5 kitu ambacho kilikuwa kinawezekana kwa udhamini mkubwa waliokuwa nao waandaaji. Hisia za kuandaliwa washindi kabla ya shindano pia ilijidhihirisha pale baadhi ya wasanii watatu (inasemekana waliandaliwa ushindi) hawakuonekana kutoa mchango wao kwenye harakati za kuomba maslahi yaongezeke.
Ni dhahiri shindano hili halikuwa na nia ya kuwafaidisha wasanii bali lilimfaidisha Shigongo na wadau wake wa pembeni. Shindano lilifanikiwa kuzima sauti za wanaharakati waliokuwa wameandaliwa ushindi ila ukweli ukabaki palepale. Hasara aliyoipata Shigongo ilihamia kwa wasanii waliokuwa wametangaza kufa au kupona kusimamia misimamo yao. Shigongo aliyewapa kick watangazaji na matamasha ya Radio flani gazetini alianza kuacha kuandika harakati za wana na wana wakabaniwa Radioni huku wasanii wasiojua kuimba wala kughani wakawa ndo kivutio kwa mdau huyu. Kuanzia miaka hiyo
Mziki wetu mpendwa wa hip hop ukakosa rafiki, ukaongeza idadi ya maadui hasa watu walipozidi kueleza ukweli na uhalisia wa maisha yao katika tungo zao.
Ukweli unachukiwa, ndo maana vyombo vya habari vinalazimisha watu watoke kwenye misingi waimbe starehe, mapenzi na anasa.. ADUI wa kwanza katika harakati hizi za kueneza ukweli ni huyu Msukuma mwenzangu, Shigongo. CCM wanampoteza, Wananchi anawapoteza ila Hip Hop hawezi kuipoteza japo anataka iwe hivyo...
Kila siku anaandika habari za mashoga na kuandika habari mbaya tu za wanaharakati ila nzuri haandiki......