Eric Shigongo aingia mkataba na CRDB ili kuwakopesha Wajasiriamali wa Buchosha

Eric Shigongo aingia mkataba na CRDB ili kuwakopesha Wajasiriamali wa Buchosha

mkweliwatz

Member
Joined
Dec 6, 2025
Posts
8
Reaction score
11

Ofisi ya Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, imewakilishwa na Kerryn Mbatude katika kikao na Benki ya CRDB kilicholenga kuzindua rasmi ushirikiano wa kuwawezesha wananchi wa Buchosa kiuchumi kupitia mikopo kwa wajasiriamali.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge, Kerryn Mbatude amesema Shigongo ameingia makubaliano na Benki ya CRDB ili kuwezesha wananchi wa Buchosa kupata mikopo yenye riba nafuu kwa lengo la kukuza biashara zao, kuongeza kipato na kuimarisha uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.

Kwa upande wao, CRDB Foundation wameeleza kuwa sasa ni rasmi kuanza kwa programu hiyo ambayo imeambatana na utoaji wa elimu ya fedha kwa wananchi ili kuhakikisha wanatumia mikopo hiyo kwa tija na kufikia malengo yao ya kiuchumi.

Benki ya CRDB imetoa wito kwa wananchi wa Buchosa kujitokeza kwa wingi kunufaika na fursa hiyo, ikisisitiza kuwa dhamira yao ni kumgusa kila mwananchi kwa huduma za kifedha zitakazochochea maendeleo na ustawi wa jamii.
 
Shark loan
Itakuwa Kausha damu iliyohalalishwa
 
Back
Top Bottom