Eric Shigongo na Global publishers hii dhambi ya kumfarakanisha Baba Diamond na wanae amto ikwepa.Acheni huu upuuzi mnabomoa

Eric Shigongo na Global publishers hii dhambi ya kumfarakanisha Baba Diamond na wanae amto ikwepa.Acheni huu upuuzi mnabomoa

Busara ni shani aliyotujaalia manani. Ni juu yetu kuitumia au kutoitumia ila inabidi tufahamu kuwa tunamkosea mungu kwa kufarakisha waja.
HAKIKA
 
Hebu ngoja nikuulize ndugu! Magazeti ya Shigongo yanakuwaga wapi hadi yafahamu kwamba Mzee Abdul anaenda kwa mwanae? Kwa mfano, walifahamu vp kuhusu hiii hapa ambayo Mzee Abudl ameishia mlangoni kama sio kwamba timu ya Shigongo walimpa vipesa ili waende nae?
View attachment 1027018

Hapa chini Shigongo alifahamuje kwamba Baba Diamond alikuwa anataka kwenda hospitali hadi wakapata hizi picha?View attachment 1027006

Anaachokisema mleta mada, ningekushauri tazama hii video hususani kuanzia dakika 3:05


Alichokisema Diamond na Mleta Mada kuhusu Mzee Abdul, ni hiki hapa:-



Unaona hapo Mzee Abdul akiwa ametandika suti baada ya kufahamu kwamba anataka kuongea na magazeti ya Shigongo huku akiwa na mwanae wa hiari ambae hata lafudhi ya Kitanzania ameisahau!!! Dada na mwenyewe, na yeye anatumia njia zile zile za Mzee Abdul, kwamba kuongea na Diamond kupitia magazeti ya Shigongo ambayo hata hivyo hawana terms mzuri kati yao!!

My take ni kwamba, anachotakiwa kufanya huyu mzee ni kuachana na hivi vigazeti vya udaku na atumie watu wenye adabu zao kupatanishwa na mwanae!

Huyu mzee anazo shida na ana hitaji msaada lakini kukubali kutumiwa na Shigongo kumchafua mwanae ndilo kosa alilo fanya
 
Wasalaam wana jamvi..

Kila mtanzania anajua fika kabisa kuwa hakuna mawasiliano mazuri kati ya Baba Diamond na wanae wakina Diamond na Queen Doreen na hakuna anayejua kilichotokea hadi wakafikia kutokuwa karibu au kuwa na maelewano kati yao.

Bahati mbaya tumezungukwa na jamii ambayo inapenda kutoa hukumu na kuchochea mambo kama si kuchonganisha,,,,Matatizo kati ya Baba Diamond na wanae yalikuwa yamemalizwa lakini bahati mbaya zaidi Baba Diamond amekuwa akitumiwa na vyombo vya habari vya shingongo bila kujijua kwa mgongo wa kumsaidia...
Huyu baba ana hitaji sana msaada wa Diamond lakini lazima tukubali kabisa kuwa ifike wakati Shigongo na Global publisher wamuache huyu Baba amalize matatizo yake na wanae bila wao kuingia kati kwa lengo la kuwadhalilisha watoto wa huyu Baba.....

Lengo la Shigongo si kumsaidia huyu Baba bali nikapata pesa kupitia huyu Baba...ni ukweli uliowazi kabisa huyu baba anaweza akatumia njia nzuri tuu kupatana na mwanae na si kukubali kutumiwa na shigongo kupata pesa ili kumshawishi mwane amsaidie,,,,,

Shigongo kama angekuwea na nia ya kumsaidia huyu Baba angelikuwa amelifanya hivyo zamani sana....ni miaka mitatu sasa Shigongo na Global publishers wamekuwa wakichochea huu mtafaruku kwa kumrekodi huyu mzee maneno mabaya dhidi ya wanae na kuyaweka kwenye miatandao....
Nafikiri Shigongo kama kweli ana nia njema na huyu baba basi angempeleka kwanza huyo baba hospitali akapate matibabu kuliko kumzungushia makamera hili kupata pesa....

Shigongo anatakiwa ajue hii dhambi ya kuchonganisha watu haiwezi kumuacha salama maana ana chochea chuki mabya sana ....
Nina hakika hawa watu wangelikuwa katika maelewano mazuri sana baini yao kama sio hii mitando na magazeti ....kwani kwa kiasi kikubwa yamechangia kuongezeka chuki baini yao.

Nichukue fursa hii kumuomba Ndugu Shigongo kuachana na Baba Diamond au mshauri atafute njia nyingine ya kuongea na watoto wake,, Ni vyema Shigongo ukawa mpatanishi mwema tena kwa njia nzuri lakini si hiz ambazo zinakuza chuki na kuchochea uhasama....

Shigongo utapata faida gani au furaha gani hawa watu wakishindwa kuzikana au kusaidiana wakiwa hai? au unasubiri kuandika na kuuza nakala "Baba Diamond afariki kwa kukosa hela ya matibabu ya Miguu", "

Huyu mzee kwaajili ya camera zako shigongo ameshatoa laana na amesha wanenea vibaya sana watoto wake na kuwakana pia....kweli una jenga au una bomoa? unategemea nini?

Shigongo tunaomba umpumzishe Mzee Abduli na umuache atatue matatizo yake mwenyewe bila wewe kuingia kati.

Wasalaam
katika watu wanao zidi kunichukiza tz hawa waandishi wa habari wakutafuta watamazaji youtube,trafic web yani mpaka wanaboa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mtu unaosomaje au kununua magazeti Haya? Daah kweli tunatofautiana
Shigongo ameona fursa na ameitumia effectively, kuna mwandishi wa habari aliwahi nieleza kwamba magazeti ya udaku yanaongoza kwa sales kwa zaidi ya 60%.... Kipindi mitandao haijachanganya wenye magazeti ya udaku kwenye printing house walikuwa wanaogopeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endeleeni kumjaza ujinga tuu.... Thamani ya kuwa na mikono miwili hujulikana pale mkono mmoja unapokatika....
Kwani kuna ulazima wa mond kwenda mumzika mtu alomkana kwamba sio mwanae? Huku kutakuwa ni kunipendekeza tu... mond bado anamtafuta baba ake halisi na sio huyu mzee wa kufikia.... kwa sababu ye alishajitoaga kwny malezi ya mwanae kwa kusema hamtambui km mwanae... sasa mond afanyaje kwa mfano? Cha kufanya huyo mzee atafute njia nzuri ya kumuomba msamaha na si kumchafua mitandaoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
katika watu wanao zidi kunichukiza tz hawa waandishi wa habari wakutafuta watamazaji youtube,trafic web yani mpaka wanaboa

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee! We acha tu! Kwanza majority ya hawa wala sio waandishi wa habari, ni wakanga njaa tu wanaotumia blogging kupata pesa ya kula! Hawa washenzi ndo wanazidi kukera kwa kusambaza videos zisizo na kichwa wala miguu!
 
Endeleeni kumjaza ujinga tuu.... Thamani ya kuwa na mikono miwili hujulikana pale mkono mmoja unapokatika....

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo mkono wa pili ni upi?! Ukweli mchungu ni kwamba, ingawaje mbegu inatoka kwa sie wanaume kiasi cha mtoto kufahamika kama ni wa baba lakini MAJUKUMU HALISI ya baba ni malezi ya mtoto na wala sio kwenye kuchangia mbegu ambazo kila siku wanaume wanazitoa kupitia punyeto! Huwezi kuwa sparm dona usiye na msaada wowote kwa watoto halafu eti ujiite mkono wa pili kisa tu ulikojoa shahawa kwa raha zako na matokeo ya shawaha hizo akatokea mtoto ambae wala ukuhangaika nae!! Leo hii Mzee Abdul analia lia kwa sababu tu Diamond ana pesa vinginevyo, si ajabu vilio vyake angekuwa anavipeleka kwingine kama ambavyo hatumsikii akiwalilia watoto wake wengine!!! Kwahiyo unakuwa mkono wa pili kwa mtoto simply because ana pesa?!

Of course, ningekuwa Diamond ningemsaidia Mzee Abdul kwa sababu za kibinadamu lakini siwezi kumlaumu wakati sifahamu how he feels! Binafsi nina mdogo wangu ambae na mwenyewe kakataa mtoto na hadi sasa huwa anajileta pale home lakini dogo anasema hamtambui! Halafu siku ya siku dogo atoboe aanze kumfungia vioo "baba" ake halafu eti mie nimuone dogo ni roho mbaya na hajui umuhimu wa mikono miwili wakati mkono wa pili wenyewe haukuwahi kutambua uwepo wake?!

Ngoja nikuambie! Thamani ya mkono wa pili utaifahamu pale utakapokatika baada ya kuanza kukikosa kile kilichokuwa kinatokana na huo mkono wa pili! Na hicho ninachosema "kukikosa" not necessarily kiwe materia stuff lakini hata kile kinachotokana na emotion!
 
Huyu mzee anazo shida na ana hitaji msaada lakini kukubali kutumiwa na Shigongo kumchafua mwanae ndilo kosa alilo fanya
Sana, anahitaji msaada kwa kweli lakini asipobadilika, watu wataendelea kumfanyia makusudi hivyo hivyo! Diamond mwenyewe keshazoea kusemwa vibaya kwahiyo anakosea sana anapodhani kumshitakia kwenye magazeti ya udaku na hatimae kuonyooshewa zaidi vidole kunaweza kuwa ndo aolution badala ya kutumia njia za busara kumaliza sintofahamu yao! Hivi unakumbuka kama sio 2018 basi 2017, Diamond alisham-post babake kwenye siku ya Father's Day! Ile ilikuwa ni hatua kubwa sana ambayo Mzee Abdul alitakiwa kufahamu kwamba mwanae kaamua kujirudi! Lakini kabla hajajirudi kwa asilimia zote, mara tena huyo kwenye magazeti ya Shigongo! Very stupid!
 
Back
Top Bottom