Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akichangia Bungeni, Shigongo ameeleza kuwa mchango wa mapato ya kodi kwenye pato la Taifa bado ni mdogo, jambo linalohitaji Serikali kuweka mazingira rafiki yatakayowezesha wananchi wengi zaidi kuingia kwenye mfumo rasmi wa ulipaji kodi.
Amesisitiza kuwa ni muhimu kujenga mfumo unaovutia walipa kodi kujitokeza wenyewe kwa hiari, ili kuongeza mapato ya ndani na kuimarisha uchumi wa nchi.
Kuhusu suala la mikopo, Shigongo amesema ni vigumu kwa Taifa kuacha kukopa kabisa, lakini amesisitiza kuwa mikopo ichukuliwe kwa tahadhari na pale tu inapokuwa ni ya lazima ili kuchochea maendeleo.
Amehitimisha kwa kusisitiza kuwa kwa kuongeza wigo wa walipa kodi na kusimamia vizuri matumizi ya rasilimali, Tanzania inaweza kufikia uchumi imara na kujitegemea kikamilifu.