Ni sera mbovu za serikali kuu na zile za Halmashauri/TAMISEMI kujaza mabango ya biashara, promotion, siasa ,waganga wa kienyeji n.k huku ni kuchafua mazingira ya barabara majengo na maghorofa.
Matangazo hayo juu badala ya kuyaanika ktk mabango serikali kuu / serikali za halmashauri mitaa wangeweka sera magazeti, majarida na stesheni za televisheni pia radio iwe ni maeneo ya rasmi mahususi na pekee kutangaza biashara, promotion, uganga n.k hivyo vyombo vya habari kuvuna matangazo pia mazingira yetu kuondokana na uchafuzi wa mabango na matambara ya matangazo.
Hii ni dunia ya kidijitali tuondokane na mbinu za kijima za matangazo.