Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Baada ya Mahakama Kuu Masjala ndogo Dar es Salaam kuifuta kesi ya mwanahabari Erick Kabendera, aliyokuwa ameifungulia kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Public Limited, ameibuka na kudai kuwa amepanga kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufani Tanzania baada ya kujadiliana na Wanasheria wake.
Kabendera akizungumza na vyombo vya habari, ameeleza jinsi alivyotekwa na kutaka kumuua, amesimulia matukio ya kutisha aliyopewa wakati wa kutekwa, akisisitiza umuhimu wa uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.
"Tutakata rufaa kwenye Mahakama ya Rufani Tanzania dhidi ya pingamizi lililowekwa dhidi yangu. Mimi na Wanasheria wangu tunaamini kesi yetu inamashiko na inastahili kusikilizwa ili tuweze kuwasilisha ushahidi wetu ambao tunaamini utatusaidia kutendeka kwa haki."
Kabendera ameyasema hayo leoJumanne Oktoba 1, 2024 alipokuwa akizungumza na wanahabari kutoka London, Uingereza
Pia, Soma:
=> Mwandishi Eric Kabendera aelezea jinsi Vodacom Tanzania ilivyomkamatisha kwa vyombo vya Usalama
=> Mahakama yaifuta kesi ya Kabendera dhidi ya Vodacom
=> Erick Kabendera aitaka Vodacom imlipe Dola Milioni 1 kwa kufanikisha kutekwa kwake 2019