Baada ya Mahakama Kuu Masjala ndogo Dar es Salaam kuifuta kesi ya mwanahabari Erick Kabendera, aliyokuwa ameifungulia kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Public Limited, ameibuka na kudai kuwa amepanga kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufani Tanzania baada ya kujadiliana na Wanasheria wake.
Your browser is not able to display this video.
Kabendera akizungumza na vyombo vya habari, ameeleza jinsi alivyotekwa na kutaka kumuua, amesimulia matukio ya kutisha aliyopewa wakati wa kutekwa, akisisitiza umuhimu wa uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.
"Tutakata rufaa kwenye Mahakama ya Rufani Tanzania dhidi ya pingamizi lililowekwa dhidi yangu. Mimi na Wanasheria wangu tunaamini kesi yetu inamashiko na inastahili kusikilizwa ili tuweze kuwasilisha ushahidi wetu ambao tunaamini utatusaidia kutendeka kwa haki."
Kabendera ameyasema hayo leoJumanne Oktoba 1, 2024 alipokuwa akizungumza na wanahabari kutoka London, Uingereza
Baada ya Mahakama Kuu Masjala ndogo Dar es Salaam kuifuta kesi ya mwanahabari Erick Kabendera, aliyokuwa ameifungulia kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Public Limited, ameibuka na kudai kuwa amepanga kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufani Tanzania baada ya kujadiliana na Wanasheria wake.
Kabendera akizungumza na vyombo vya habari, ameeleza jinsi alivyotekwa na kutaka kumuua, amesimulia matukio ya kutisha aliyopewa wakati wa kutekwa, akisisitiza umuhimu wa uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.
Baada ya Mahakama Kuu Masjala ndogo Dar es Salaam kuifuta kesi ya mwanahabari Erick Kabendera, aliyokuwa ameifungulia kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Public Limited, ameibuka na kudai kuwa amepanga kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufani Tanzania baada ya kujadiliana na Wanasheria wake.
Kabendera akizungumza na vyombo vya habari, ameeleza jinsi alivyotekwa na kutaka kumuua, amesimulia matukio ya kutisha aliyopewa wakati wa kutekwa, akisisitiza umuhimu wa uhuru wa kujieleza na haki za binadamu.
Kesi ilifutwa kabla hata ya kuanza kusikilizwa kwa kigezo cha muda kwamba alifungua mashtaka baada ya muda kupita .
Sijui ni muda gani unatakiwa usipite ukitaka kudai fidia wanasheria wanaweza kusaidia kwenye hili
2019 30 Julai
Polisi nchini Tanzania imesema kuwa mwanahabari wa Erick kabendera aliyedaiwa kutoweka hakutekwa bali alikamatwa.
Kukamatwa kwake kunatokana na mashaka katika uraia wake.Erick Kabendera ana andikia magazeti ya ndani na nje ya Tanzania View: https://m.youtube.com/watch?v=r9Gnnr-gx54 2020 2 January
DADA NA NDUGU WA KABENDERA WALIVYOLIA KWA UCHUNGU
View: https://m.youtube.com/watch?v=gDyB3M4uE7k Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemnyima mwandishi wa habari Erick Kabendera aliye rumande ruhusa ya kwenda kumuaga au kumzika mama yake.
Mama yake Kabendera, Bi Verdiana Mujwahuzi, alifariki dunia siku ya Jumanne tarehe 31 Desemba 2019 katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.
Akitoa uamuzi wa mahakama hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega alisema mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri ya Kabendera kusindikizwa chini ya ulinzi kwenda kutoa heshima za mwisho kwa marehemu mama yake mzazi.
Uamuzi huo ulikuja katika awamu ya pili ya usikilizwaji wa kesi hiyo baada ya upande wa mashitaka na utetezi, kubishana kwa hoja kwa saa kadhaa na baadae hakimu kuahirisha usikilizaji hadi baadae ambapo hakimu alikuwa tayari kutoa uamuzi wa mahakama.
Kuhusu mchakato wa 'plea bargain', upande wa mashtaka ulisema upande wa utetezi umekamilisha marekebisho katika maombi yao waliyotakiwa kufanya, hivyo mchakato huo unaendelea.
Kesi ya Kabendera imeahirishwa zaidi ya mara kumi, na leo pia imeahirishwa na kupangiwa kusikilizwa tena tarehe 13 January 2020.
View: https://m.youtube.com/watch?v=9-D281x4naI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemuhukumu Mwandishi wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera kulipa faini na fidia ya jumla ya Tsh. Milioni 273 baada ya kukiri makosa yaliyokuwa yakimkabili ya utakatishaji fedha na ukwepaji kodi huku akiondolewa shitaka la kuongoza genge la uhalifu.Mahakama imetoa uamuzi huo leo Jumatatu, Februari 24, 2020, baada ya mwenendo wa kesi iliyokuwa ikimkabili inafuatia kukamilika kwa mazungumzo na makubaliano baina yake na Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP).Kabendera amekiri shtaka la kukwepa kodi ya TZS milioni 173. Ameahidi kulipa kiasi hicho kwa mafungu ndani ya kipindi cha miezi 6. Kwa shtaka hilo, mahakama imeamuru alipe faini TZS 250,000 au kifungo cha miezi sita jela.Kabendera amekiri pia shtaka la utakatishaji fedha na mahakama imeelezwa kuwa mwandishi huyo maarufu wa habari za kiuchunguzi, tayari ameshalipa kiasi cha TZS milioni 100 kama faini ya shtaka.
Mwenyekiti wa makampuni ya Vodacom Afrika Bw. Sakumzi Macozoma akiwa katika ziara ya kikazi akutana na mabosi wa Vodacom Tanzania na pia akutana na viongozi wa serikali ya Tanzania
Vodacom Tanzania PLC we are honored to welcome and host Shameel Joosub, Vodacom Group CEO, and the Vodacom Group Board, led by the Chairman Sakumzi Macozoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania akimpokea mwenyekiti wa makampuni ya Vodacom Afrika Group, na pamoja wafanya mazungumzo Kushirikisha Serikali katika Mabadiliko ya Kidijitali
Vodacom Tanzania ilikutana na Waziri wa TEHAMA wa Tanzania kujadili ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi na kuendeleza mageuzi ya kidijitali nchini.
Katika ziara hiyo ujumbe wa Vodacom ulikutana na Mhe. Jerry Silaa, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia wa Tanzania. Majadiliano yalihusu mada kuu, ikijumuisha jukumu muhimu la ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) katika kuendesha maendeleo ya taifa, na njia ambazo Vodacom inaweza kuunga mkono dira ya serikali ya mabadiliko ya kidijitali. Mkutano huo ulisisitiza umakini wa Vodacom katika ushirikiano ili kuharakisha utumiaji wa teknolojia, na hivyo kusaidia kujenga mustakabali wenye uhusiano na ubunifu zaidi kwa Tanzania.
Vodacom Tanzania imesisitiza kujitolea kwake kufanya kazi kwa karibu na serikali ili kuleta maendeleo na kuwezesha kila Mtanzania kupitia teknolojia. Kampuni inalenga kupanua ufikiaji wa kidijitali, kuziba mapengo ya muunganisho, na kukuza siku zijazo ambapo teknolojia inasaidia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya kitaifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kundi la Makampuni ya Vodacom Bw. Sakumzi Macozoma pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.