Ifike hatua sasa tuanze kujulishwa kuhusu watu wote waliotekwa na kuwekwa ndani enzi za Magufuli ni walikua wamekosea nini? Walau Ben saa8 inajulikana, alikosoa phd ya Magufuli; huyu tunaweza kusema pasipo shaka kabisa kwamba alionewa, hope hata Magufuli huko aliko lazima atakua anajutia hilo cause ugomvi wao ulikua ni personal, hauna uhusiano wowote na urais au usalama wa nchi; kuna viongozi wengi tu, wanaitwa ma dokta while degree zao za kwanza tu ni questionable, King Msukuma nae ni Dr. Kwasasa, kapewa so ile ya JPM iwe ya kwelu au sio ya kweli haikua na issue yoyote kiurais so Ben saa nane hakuyakiwa kupotea kwasababu hizo. Lakini kuhusu makara za Kabendera, hivi kuna mwandishi wa say Uingereza au Marekani anaweza kuandika habari za siri za nchi yake halafu mwandishi huyo huyo akawa salama nchini mwake? Why yule shushushu wa USA anatafutwa hadi leo? Why kakimbilia nchi hasimu na USA? Kuhusu kuvuta bangi kwa Magufuli, hivi si kuna nchi zikowepo hizo ambazo Kabendera alikokimbilia zina ruhusu uvutaji wa bangi? Well, kati ya viongozi waliopo na waliopita, ukiwaweka kwenye mizani ya wananchi, unadhani Magufuli atashika nafasi ya ngapi? Twitter walikaribu kupigisha kura, Magufuli aliongoza; gazeti la Mwananchi pia walipigisha KURA, again marehemu aliongoza. So machoni pa watu wa kawaida, bado Magufuli anatazamwa kwa jicho tofauti na mitazamo ya kina Kabendera, tutafakari. Je wananchi hawana akili?