Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Bado mimi nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kama shida ni kocha, TEN HAG anaweza kuwa kuwa sehemu ndogo sana ya tatizo lililopo Old Trafford kwa sasa! David Moyes kapita hapo na alitoka Everton akiwa bora sana, Louis Van Gaal amepita hapo akiwa na Uholanzi tishio Duniani, Jose Mourinho ndio hakuna kitu cha kuongeza kisha Ole Gunnar na Ralf Rangnick
Hao Makocha wote walikuwa tatizo pale Man United? Sawa tukubali Ten Hag ni shida! Je wachezaji alionao unaona wana kitu cha ziada kwenda kushindana dhidi ya Man City, Arsenal na Liverpool kuwania Ubingwa wa EPL? Sawa tuache Ubingwa ni mbali sana! Je, Rashford, Garnacho, Zirkzee, Rasmus na wengineo kukosa nafasi za wazi mechi hadi mechi ni kosa la Ten Hag
Wachezaji wanalipwa pesa nyingi ila wengi hawapambani kwaajili ya jezi ya Man United, Wachezaji wanatembea uwanjani kama sio kufanya makosa wiki hadi wiki! Kabla ya kulaumu Benchi la Ufundi la Man United basi inapaswa wachezaji ndio iwe sehemu ya kwanza kisha falsafa ya Timu ambayo tunaishi kuanzia kuondoka kwa Sir Alex Ferguson! Sera ya Usajili mbovu, wachezaji wengi wanafeli na vijana kutoka academy wanaofanya vizuri wanauzwa kama sio kuondoka bure wenda Timu nyingine
Mkurugenzi wa Ufundi wa Man United, Dan Ashworth tayari hapo nyuma alishaeleza kuwa Timu inahitaji maboresho makubwa sana ndani ya uwanja, hapa akiwa na maana ya kuondoa baadhi ya wachezaji na kuleta wengine wapya ambao taratibu watairudisha Timu kwenye njia nzuri! Kumuondoa Ten Hag na kuja mtu mwingine ni kuanza upya tena kama hatuna falsafa nzuri ambayo tunaishi nayo kwa sasa
Man United inahitaji maboresho makubwa sana ya kikosi chake yaani wachezaji kabla ya kufika huko walipo kina Erik Ten Hag na wenzake! Timu inapaswa kuzalisha wachezaji wake kama ilivyokuwa utamaduni wao, ndio maana ni rahisi JOHN EVANS kupambana kwaajili ya jezi ya Man United kuliko hao wachezaji wengine ambao hawatambui historia na uchungu wa Old Trafford
Malengo ya Klabu ni KUCHUKUA UBINGWA WA EPL 2028 na ndio maana nasema kwa sasa ni mapema sana kuzungumza kuhusu Benchi la Ufundi, I Stand to be Corrected 💪
Itaendelea:..
Let's Goo!!.