SI KWELI Ernest Mgawe amesema alitumwa na Heche na Mange kuratibu vurugu mwendokasi

SI KWELI Ernest Mgawe amesema alitumwa na Heche na Mange kuratibu vurugu mwendokasi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
photo_2025-10-07_16-22-08.jpg
photo_2025-10-07_16-22-17.jpg
photo_2025-10-07_16-22-26.jpg
 
Tunachokijua
Ernest Mgawe ni Mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilaya ya Kibamba, ambaye Oktoba 04, 2025 chama chake kilitoa wito wa kutaka kuachiwa huru au kufikishwa mahakamani baada ya mwenyekiti huyo kukamatwa kwa tuhuma za kuhamasisha fujo kwenye magari ya Mwendokasi na kuhamasisha maandamano.

Madai
Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni kwa kutumia grafiki zenye utambulisho wa vyombo mbalimbali vya habari na kudai kuwa Ernest Mgawe alisema Heche, Mange walimtuma kuratibu vurugu mwendokasi. Rejea hapa, na hapa.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani hakuna chanzo cha kuaminika kilichoripoti kauli hiyo zaidi ya kusambazwa na wapotoshaji.

Vilevile grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo zimeghushiwa na wapotoshaji kwani hazijachapishwa na vyanzo hivyo (Jambo Tv, Mwananchi, na Clouds Media) kama inavyoonekana.

Aidha grafiki hizo zimebainika kuwa na mapungufu kadhaa ikiwemo kutumia aina tofauti ya mwandiko (Font) ukilinganisha na grafiki halisi za vyombo hivyo.​
Back
Top Bottom