ERYTHROPOETIN 4000IU SC Dawa ya FIGO

Yo Yo

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2008
Posts
11,210
Reaction score
1,720
Wakuu naitafuta popote ilipo hii dawa nina mgonjwa anahitajika kutumia hii dawa....wapi naweza ipata?
 
wakuu msaada please
 
Pole YoYo....hiyo si dawa ya figo per se. Kwa kawaida mafigo hutoa kichocheo hicho cha erythropoietin ambacho kazi yake ni kustimulate bone marrow itengeneze chembe chembe nyekundu za damu (red blood cells). Mafigo yanapokuwa magonjwa yanashindwa kutoa erythropoitin na hivyo mgonjwa kupata upungufu mkubwa wa damu (severe anaemia). Sasa hiyo erythropoietin haitibu figo, ila inaenda kufanya kazi ya kustimulate bone marrow kuzalisha red blood cells figo zinaposhindwa kufanya hivyo.

Mara ya mwisho niliona mgonjwa akihitaji hiyo mwaka 2007, na tuliagiza toka Nairobi. Nilidhani mpaka sasa itakuwepo, ni aibu kama bado hatuna. Tafadhali check kwanza na maduka makubwa ya dawa mfano JD Pharmacy, Okinawa Pharmacy, Philips...kabla huaagiza Nairobi.
 
Hello... hiyo ni dawa ya kumsaidia mtu mwenye renal failure wakati anafanyiwa dialysis... erthropoietin katika mwili inahusika katika formation of red blood cells... Nenda OKINAWA PHARMACY .. Ipo Jirani Jirani na Askari Monument..au Salama Pharmacy Kariakoo... au Dawa Pharmacy Benjamini Mkapa Pension Tower.... JD Pharmacy Mlimani City au JD Pharmacy jirani na round about ya Askari Monument

Nawasilisha
 
ahsanteni wakuu imeshapatikana.....mbarikiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…