Pole YoYo....hiyo si dawa ya figo per se. Kwa kawaida mafigo hutoa kichocheo hicho cha erythropoietin ambacho kazi yake ni kustimulate bone marrow itengeneze chembe chembe nyekundu za damu (red blood cells). Mafigo yanapokuwa magonjwa yanashindwa kutoa erythropoitin na hivyo mgonjwa kupata upungufu mkubwa wa damu (severe anaemia). Sasa hiyo erythropoietin haitibu figo, ila inaenda kufanya kazi ya kustimulate bone marrow kuzalisha red blood cells figo zinaposhindwa kufanya hivyo.
Mara ya mwisho niliona mgonjwa akihitaji hiyo mwaka 2007, na tuliagiza toka Nairobi. Nilidhani mpaka sasa itakuwepo, ni aibu kama bado hatuna. Tafadhali check kwanza na maduka makubwa ya dawa mfano JD Pharmacy, Okinawa Pharmacy, Philips...kabla huaagiza Nairobi.