Esacs international academy kulikoni?

bhageshi

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2010
Posts
264
Reaction score
101
Hello wanafamilia wa JF, naomba msaada wenu juu ya shule hiilevel ya Primary School au wengine huita Junior School. Mie nipo nje ya nchi yetu pendwa natafuta shule kwa ajili ya mwanangu. Rafiki yangu mmoja ameniambia juu ya shule hii lakini hakuwa na takwimu zozote juu ya ufanisi wa elimu itolewayo hapo zaidi ya kunielekeza mahali ilipo. Hivyo basi naomba kwenu mwenye taarifa zozote juu ya ubora wa elimu inayopatika hapo anipatie taarifa hizo na hata mazingira ya shule kwa ujumla, kwani asilimia kubwa muda mwingi mtoto huwa shuleni na hivyo makuzi na malezi ya mtoto kwa asilimia kubwa tabia za waalimu na mazingira ya shule kwa ujumla ya athari kwa mtoto. Kwa yeyote mwenye chochote anipatie ili niweze kufikia maamuzi, hata picha sawa tu kwani naweza pata chochote from photograph interpretation.
 
<br />
<br />
Hakuna shule mbaya yategemea ww kama mzazi. Wamsimaje mwanao? Hata ukimpelekea makuburi primary atachomoka tu kama wengine
 
Unless na wewe unarudi ukae nae ila kama unampeleka kwa bibi yake hapo unaharibu. Kama mchangiaji hapo juu msingi ni usimamizi tena wa karibu kwelikweli ILA HILO LA MAKUBURI SINA UHAKIKA NALO. Shule nzuri wanafundisha vizuri sana na elimu yao inafuata mfumo wa Kiingereza kwa makuburi sijui, mazingira poa, usafiri na Kiingereza ni kipaumbele. Ila mwandalie na tuition ina saidia kwelikweli (From experience)

Elimu ya msingi shule za serikali ( Makuburi)imetelekezwa mfano viongozi gani wanasomeshea watoto wao katika shule hizo? Wachache sana na ni wazalendo kwelikweli.
Good luck.
 
asante kwa ushauri na nitauzingatia
 

Shukrani kwa taarifa na ushauri wako utazingatiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…