bhageshi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2010
- 264
- 101
Hello wanafamilia wa JF, naomba msaada wenu juu ya shule hiilevel ya Primary School au wengine huita Junior School. Mie nipo nje ya nchi yetu pendwa natafuta shule kwa ajili ya mwanangu. Rafiki yangu mmoja ameniambia juu ya shule hii lakini hakuwa na takwimu zozote juu ya ufanisi wa elimu itolewayo hapo zaidi ya kunielekeza mahali ilipo. Hivyo basi naomba kwenu mwenye taarifa zozote juu ya ubora wa elimu inayopatika hapo anipatie taarifa hizo na hata mazingira ya shule kwa ujumla, kwani asilimia kubwa muda mwingi mtoto huwa shuleni na hivyo makuzi na malezi ya mtoto kwa asilimia kubwa tabia za waalimu na mazingira ya shule kwa ujumla ya athari kwa mtoto. Kwa yeyote mwenye chochote anipatie ili niweze kufikia maamuzi, hata picha sawa tu kwani naweza pata chochote from photograph interpretation.