Escrow: Mahakama Imedhalilishwa! Imedharauliwa! Imefedheheshwa!- Ili Kulinda Heshima Yake

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Najua wengi wetu, tumehamanika na mjadala wa Escrow na Ripoti ya PAC, kwetu sisi wengine wenu, ile Ripoti ya PAC ya jana, tunaiona hakina kitu wala haina jipya bali ni sehemu tuu ya mihemuko ile ile kuhusu sakata hili tangu mwanzo.

Escrow ni matokeo tuu, watu humu wanashangilia matokeo tuu, nikadhani ripoti hiyo ingetupeleka kwenye chanzo cha jinamizi hili la IPTL ili tung'oe tangu mizizi!, IPTL ni rushwa mwanzo mwizo!, hivi mnamjua ni nani aliyewaleta?!.

Hayo ya Ripoti ya PAC ni cha mtoto, kikubwa kwangu Escrow: Mahakama Imedhalilishwa!. Imedharauliwa!, Imefedheheshwa!-Ili Kulinda Heshima Yake inabidi Mahakama itoe statement, kwanza kukitafsiri Ibara ya 100 ya Katiba ya JMT, kuhusu nani yuko right kati ya Mahakama kutoa amri halali kulizuia Bunge kujadili issue iliyoko mahakamani, au mahakama ndio iliyokosea kutoa amri kwa Bunge, uwezo ambao mahakama haina.

Na ili kuilinda heshima yake, kama ni Jaji alikurupuka, then mahakama itamke wazi kwa kumvua ujaji jaji huyo aliyopelekea Mhimili wa Mahakama kudhalilishwa!, kudharauliwa! na kufedheheshwa!, hali itakayopelekea stop orders za mahakama zitakuwa zinadharauliwa kila siku. Vinginevyo wakitamka zuio lile lilikuwa ni amri halali, then Mahakama italifanya nini Bunge kwa kuidhalilishwa!, kuidharauliwa! na kuifedhehesha Mahakama?!.

Kwa watu wote wanaojua utawala wa sheria, "the doctrine of separations powers!", kati ya mihimili hii mitatu ya dola, hawawezi kuiacha hali hii ikapita tuu hivi hivi!.

Paskali

NB-Mode, hii mada inahusu hoja za kisheria na sio hoja za kisiasa!.
 
A rubbish not to talk, as it is against but the way to quench your thirst of self egoistic and money chasing, even Charles De Montesque wouldn't allow this ----, if he would to be alive up to date.......
 
Wewe mwenyewe hujaongea kisheria umeongea kisiasa halafu unataka watu wapoteze muda wao kuongea kisheria. Nenda kwanza ukasome constitutional na administrative law ndio uje tuongee kisheria
 
Huu ni mwendelezo wa kile walichoanzisha.

Walishindwa kutoa amri wakati wa bunge la katiba. Eti lipo kisiasa zaidi!

Sasa, hata hili la Escrow lipo kisiasa/maisha ya watanzania. Bora wakae kimya!
 
Tatizo lako Pasco unataka kututoa kwenye mstari.Subiri basi tumalize issue moja ya sakata hili tutarejea na uchambuzi wako.

wakati nikihaidi kutorejea katika thread yako na kuomba tusiijadili zaidi nakuomba unitafute kifungu katika katiba kinachopingana na hiki hapa chini -Nasisitiza kwenye katiba siyo kwenye sheria.tunaanza na katiba kabla ya sheria.

Ibara ya 100.-(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika
Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema
au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo
 
Last edited by a moderator:
Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika!.

Jee unazizua hizo sheria nyingine zozote zinazohusika?, jee unayajua masharti yake?!.

Pasco
 
Nakupongeza mkuu Pasco kwa kusimamia ukweli juu ya jambo hili tangu mwanzo
 
Ile ripoti ya PAC ni ripoti ya kihuni tu ambayo haina chembe ya ukweli hata kidogo ni ripoti ya kihuni kabisa.
 
 
Mgogoro wa kisheria kati ya mahakama na mihimiri mingine, mtoa tafsiri ya kisheria awe tena mahakama- huu ni ujinga.
Hekima lzm itumike the way i see leo mahakama itatoa maamuzi ya kujibeba, kesho bunge litabadilisha sheria ili kuibana mahakama.

NCHI IMEKOSA MTU WA KUTUONGOZA NA KUTUUNGANISHA
KILA MMOJA ANA NDEVU SIKU HIZI HAIJULIKANI BABA NANI, MAMA NANI, NA MTOTO NANI, WOTE WAMEFANANA.
SHAME
 
Niliipenda sana statement ya Spika juzi kwamba itafikia mahali kila mtu akifanya uchafu wake anakimbilia Mahamani kwenda kuweka zuilio. Hivi mambo yako bungeni unawezaje kukimbilia Mahakamani halafu unatafuta watu wasapoti...
 
Rejea miaka ya huko nyuma 1992. Valambia aliishitaki serikali. Valambia alishinda kesi na serikali iliamuriwa kumlipa Valambia $70 milioni. Serikali ilikaidi kulipa pamoja na juhudi zote alizofanya Valambia kupitia mahakama, serikali ilikaidi na mpaka Valambia alikutwa na umauti bila ya kulipwa pesa zake. Ukaidi umeanza siku nyingi. Tuone hili hatua gani itachukuliwa ili kuweka sawa haya mambo katika siku zijazo.
 
Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika!.

Jee unazizua hizo sheria nyingine zozote zinazohusika?, jee unayajua masharti yake?!.

Pasco

Pasco iyo phrase unaitoa wapi? Icho unachogang'ania 'bila kuathiri katiba hoi au sheria yoyote' kipo ibara ndogo ya pili inayohusu mbunge kutoshitakiwa, usipotoshe umma!!
 
Ivi mleta mada ulimsikiliza mwanasheria ...waziri wa katiba na sheria alivoclear hii ishu? Mbona hautaki? Ulimsikiliza spika? Au wazo lako ndio kuu tu???
 

Naomba kueleweshwa subsection 2 inaendana vipi na Escrow? was it hoja, muswada ama wizi wa fedha za Umma?
Confusion, pls help.
 
Last edited by a moderator:



Mkuu Pasco umeona Mafisadi wanaendelea na mkakati wao.


 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…