Esma Platnumz Afichua Tabia ya Zuchu Akigombana na Diamond: "Anablock Familia Nzima Ya Wasafi"

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Dada wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Esma Khan (Esma Platnumz), amefunguka kuhusu tabia ya msanii Zuchu pale anapokuwa na tofauti au migogoro ya kimapenzi na kaka yake, Diamond Platnumz.

Akizungumza kuhusu mahusiano ya wawili hao na jinsi yanavyoathiri watu wa karibu, Esma ameeleza kuwa Zuchu akiwa amekosana na Diamond, huwa hachagui wa kumzuia (kum-block) kwenye mitandao ya kijamii, bali anachukua maamuzi ya kuwablock ndugu na wanafamilia wote wa Wasafi bila kubakiza mtu.

Esma alibainisha kuwa hatua hiyo ya Zuchu huwa inawashangaza mara kwa mara, kwani ndugu hao huwa hawahusiki moja kwa moja na migogoro ya wawili hao ya kimahusiano.

Aliongeza kuwa hata wanapojaribu kufuatilia au kutaka kujua kilichoendelea, wanajikuta wote wamewekwa kwenye orodha ya watu waliozuiliwa (block list) kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, Esma alieleza kuwa hali hiyo imekuwa kama mzunguko wa kawaida kwao, kwani pindi mambo yanapotulia na wawili hao kupatana, mawasiliano hurejea kama kawaida na mambo mengine kuendelea.

Tabia hii ya Zuchu imezua gumzo mtandaoni, huku mashabiki wengi wakitoa maoni tofauti kuhusu namna hisia za mahusiano zinavyoingilia mahusiano yake na familia ya bosi wake huyo wa lebo ya WCB Wasafi.

1789377685683.png

​
 
Si mnaachana nae, kwani lazima kuwasiliana au mnampigaga mzinga kama mtu hataki shobo unamzimia taa tu kila mtu kimpango wake
 
Huyo sijui Esma Khan,Baba yake ni Shah rukh Khan?
Anahusika na nini huko Daslam?
 
Dada wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Esma Khan (Esma Platnumz), amefunguka kuhusu tabia ya msanii Zuchu pale anapokuwa na tofauti au migogoro ya kimapenzi na kaka yake, Diamond Platnumz.

Akizungumza kuhusu mahusiano ya wawili hao na jinsi yanavyoathiri watu wa karibu, Esma ameeleza kuwa Zuchu akiwa amekosana na Diamond, huwa hachagui wa kumzuia (kum-block) kwenye mitandao ya kijamii, bali anachukua maamuzi ya kuwablock ndugu na wanafamilia wote wa Wasafi bila kubakiza mtu.

Esma alibainisha kuwa hatua hiyo ya Zuchu huwa inawashangaza mara kwa mara, kwani ndugu hao huwa hawahusiki moja kwa moja na migogoro ya wawili hao ya kimahusiano.

Aliongeza kuwa hata wanapojaribu kufuatilia au kutaka kujua kilichoendelea, wanajikuta wote wamewekwa kwenye orodha ya watu waliozuiliwa (block list) kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, Esma alieleza kuwa hali hiyo imekuwa kama mzunguko wa kawaida kwao, kwani pindi mambo yanapotulia na wawili hao kupatana, mawasiliano hurejea kama kawaida na mambo mengine kuendelea.

Tabia hii ya Zuchu imezua gumzo mtandaoni, huku mashabiki wengi wakitoa maoni tofauti kuhusu namna hisia za mahusiano zinavyoingilia mahusiano yake na familia ya bosi wake huyo wa lebo ya WCB Wasafi.

Sura ya Zuchu inarudi kama alivyokuwa mwanzo siyo ile aliyetoka kujifungua aiseee.
 
Back
Top Bottom