Espionage; How agents transmit findings

Espionage; How agents transmit findings

na ile ya kujifanya vichaa ni ya kweli?
Nilisoma kitabu fulani nikagundua hiyo kitu ni ya kweli,kichaa ni vigumun kumshitukia ,na pia sijui kama unajua jalala la nyumba fulani au taka zimebeba taarifa za nyumba husika.Kwa mfano kama jalala lenu lina vipisi vya sigara(wanaoisi wanavuta sigara),chupa za pombe za kopo, ni walevi na ainaya pombe wanayotumia itajulikana),jalala linaelezea uwezo wa kifedha wa familia husika.
Ni muhimu kwa spy kuwa mbunifu,kwani ukitumia hizi njia ambazo wote mnafundishwa kukamatwa ni rahisi.Ni kama Ninja hacking,technique inatumia mara moja tu.
 
Nilisoma kitabu fulani nikagundua hiyo kitu ni ya kweli,kichaa ni vigumun kumshitukia ,na pia sijui kama unajua jalala la nyumba fulani au taka zimebeba taarifa za nyumba husika.Kwa mfano kama jalala lenu lina vipisi vya sigara(wanaoisi wanavuta sigara),chupa za pombe za kopo, ni walevi na ainaya pombe wanayotumia itajulikana),jalala linaelezea uwezo wa kifedha wa familia husika.
Ni muimu kwa spy kuwa mbunifu,kwani ukitumia hizi njia ambazo wote mnafundishwa kukamatwa ni rahisi.Ni kama Ninja hacking,technique inatumia mara moja tu.
kwa kuongezea tu yeye kama ni mpenzi wa muvi akacheki muvi yaitwa elysium kuna jamaa kacheza kama kichaa ila vifaa vya mawasiliano alivyo kuwa navyo ni hatari.
 
Mkuu hivi huu Uzi una neno TISS kweli? ivi unadhani mambo ya intelligence ni kwa ajili ya Umma tu? Hujui kuna private people wana ajiri Mashushu kwa ajili ya kukusanyiwa taarifa zao either za kampuni au taasisi kwanini unahisi tunawaanika TISS kwanza hatuijui wala hatujui mfumo wake huu uzi umechambua general method not tiss method
asante kwa kunielimisha mkuu!!!!!!!!!
 
Ongezea mkuu
wakuu wa kazi, taaluma ya ujasusi ni taaluma ya watu wenye mashaka sana (profession of skeptics) ujasiri na umakini wa hali ya juu sana. spy hapaswi kuamini kiumbe hai chochote kwa 100% hususani binadamu. kwa kuzingatia weledi wa kazi yake, spy anapaswa kujiuliza lolote linalotokea mchoni pake ama kwenye masikio yake kuwa ina athari gani katika usalama wa nchi, hivyo watu wa namna hii wanapaswa kuwa makini kwa zaidi ya 2000%..........
 
Habari wakuu, natumai wote ni wazima. Napenda kuwaletea thread kuhusu Espionage au Intelligence. Espionage ni nini? Espionage ni kitendo cha kukusanya taarifa au nyaraka muhimu za nchi/taifa au taasisi kubwa. Taarifa hizo zaweza kua za biashara, siasa au nguvu ya jeshi la taifa jingine nk na kuzihamisha au peleka sehemu zinapotakiwa kwenda.

Kumbuka kuwa, taarifa hizi hupatikana kupitia njia za kwa siri kwahiyo lazima zifichwe ili yule anayechunguzwa asiweze gundua kile kinachoendelea, na vile vile ni kwa ajili ya kulinda usalama wa taarifa zenyewe, yaani taarifa zifike zikiwa katika ubora unaohitajika.

Thread hii inalenga kuzitaja njia zitumikazo kuhamisha {transmit or communicate} taarifa za kijasusi. Taarifa zikishapatikana zinahitaji kufanyiwa kazi au kuchunguzwa, sasa taarifa haiwezi chunguzwa kama haijafika pale panapostahili.

· Kwa kutumia geresha ya sigara au kiko

Hii njia hupendwa kwasababu si rahisi, katika hali ya kawaida mtu kufikiri kuwa, ndani ya sigara anayovuta spy kunaweza kuwa na ujumbe wa kiintelejinsia. Pia ni njia rahisi kwa usalama wa spy huyo maana kama akigundulika au akishukiwa, basi huweza poteza ushahidi kwa kuuchoma kama vile anavuta sigara.

· Kwa kutumia soli za viatu

Kwenye soli ya kiatu kunakuwa na nafasi ndogo ambayo imetengenezwa (chamber) ili kuweza kuhifadhi taarifa ndogo ndogo. Mfano memory cards zinaweza fichwa hapo. Njia hii ilipendwa sana na warusi maana ilikuwa, japokuwa inaonekana ndogo lakini ina uwezo mkubwa. Memory card iliyofichwa kwenye soli inaweza kuwa na mafile ya picha hadi 500–10000. Au mafaili ya audio records 1000 kutegemea na ukubwa wa device.

· Kwa kutumia michoro (tattoo) kwenye visogo, kisha kuotesha nywele kwenye maeneo hayo ya kisogo upya

Njia hii inatumika kwasababu ya usiri wake. Si rahisi mtu kumshuku spy kama anaweza kua ameficha taarifa kwenye kisogo chake kwa kutumia michoro. Kwaiyo ujumbe au taarifa zinaweza kuonekana pale tu baada ya Spy huyo kunyolewa nywele na kupaka kimiminika ( chemical ) sahihi kisogoni kwake.

· Kwa kutumia macho feki

Hii njia inatumika kwa kuchukua kipande cha kioo ( lenzi ) na kuweka kwenye macho, ila nyuma ya lenzi iyo kuna kua na nafasi ndogo ya kuweza kuhifadhi devices ndogo kama micro chips ambazo zinakua zimehifadhi taarifa muhimu.

· Kwa kutumia sarafu au shillingi

Hii shillingi huonekana kuwa ni ndogo kwa mtazamo, ila zinakuwa na katundu kadogo kadogo ambacho hakaonekani kirahisi, ambacho ukichukua pini na kuipenyeza kwenye ako katundu basi shillingi hiyoinajifungua kati kati au nusu kwa nusu. Katikati unaweza tunza micro chips au memory cards ambayo inaweza kua na taarifa yenye hata kurasa 50 au zaidi.

· Kwa kutumia karatasi maalumu

Hii ni karatasi ambayo, kwa mtazamo inakua tupu yaani haina maandishi kwaiyo sio rahisi kwa mtu kuishuku. Ila ukweli ni kuwa, karatasi hii inakuwa imebeba ujumbe ndani yake. Ujumbe huu huweza kuonekana kwa kuchemsha iyo karatasi kwenye vimiminika vya kemikali sahihi, au maji nk

· Kwa kutumia dead drop

Hapa taarifa hufichwa kwenye eneo ambalo linajulikana kabla au mapema, na baada ya muda mfupi, mtu mwingine anaenda kuzichukua. Njia hii ni maarafu sana na inatumika sana, ni kama zile the most celebrated kamasutra positions hahaha. Faida yake ni kuwa, inazuia nafasi za yule anayeficha taarifa na mpokeaji kukutana uso kwa uso au kuwa wote pamoja kwa wakati mmoja katika eneo husika. Hivyo basi, hata ikitokea muhusika anafuatilia (kama ni double agent ) anaweza akajitetea, na hasa kama eneo lenyewe ni kama kwenye garden, anaweza sema kuwa ameenda kupunga upepo nk.

Taarifa inaweza wekwa kwenye mfuko wa takataka, kinyesi cha ng’ombe au sehemu yeyote ile ambayo itamfanya mpita njia akiona asiweze kupata kishawishi cha kutaka kuchukua au kudadisi hizo taarifa.

· Kwa kutumia mizoga ya wanyama

Mnyama ( panya, paka, sungura nk ) mwenye umbo dogo, ambae yupo hai, anauawa, kisha taarifa za siri zinawekwa ndani yake, anashonwa kwa operation. Baada ya hapo hatua inayofutia ndo muhimu zaidi na ndiyo inayoleta tofauti ( usiri ).

Mnyama huyo hunyunyuziwa vimiminika vya kemikali ambavyo hufanya aoze na kutoa harufu mbaya ambayo ni kero kwa watu na hata wanyama ambao katika hali ya kawaida huwa wanakula jamii iyo ya wanyama (mzoga) kuchukizwa na hyo harufu na kupuuzia huo mzoga, kisha hutupwa kwenye eneo husika au lililokusudiwa ili muhuika wa upande mwingine aweze kuona na kuchukua taarifa hizo.

Kama unafahamu njia zingine, pls share..

Link iyo hapo chini, BBC waki-report maisha ya double agent wao toka anajua recruited mpaka ana deflect. Ni Tanzania tu ambapo inaonekana sio sahihi ila sio uko walipoendelea
Kim Philby, British double agent, reveals all in secret video - BBC News
alafu ya kiaskari, hii taaluma inahitaji vijana ambao ni sharp-minded, agile and too swift kwa kiasi kwanza vijana wanakuwa wabunifu wa mbinu mbalimbali za kuweza kufanikisha kazi zao na si lazima kukazania kile walichofundishwa na chuoni kwao, ili mradi hawakiuki kanuni na misingi ya majukumu yao. nakumbuka kwa mfano mossad, huwa hawaruhusu assassination method moja, kutumika katika mission zingine zote zitakazofuata ili kuepuka kwa agents kukamatwa kwa maana kwa kila tukio la kihalifu katika hostile country, vyombo vya usalama hufanya assessment ya kuangali wapi kulinkuwa na loopholes zilizowezesha mission ya maadui kukamilika.
yangu hayo tu kwa leo.
 
mossad wapo vizuri katika mfumo wa @espionage,wakati wa tukio la kigaidi sept. 11,2001 waisrael waliokua ndani ya @WTC walipewa taarifa ya kuondoka mapema kabla ya tukio,hapo inadhihirisha kiasi wametapakaa dunia nzima
 
kuna mada iliyokuwa na kichwa TISS wanatumia vyombo Gani vya mawasiliano? ilianzaishwa siku kama tatu zilizopita ila naona ilikwisha fungiwa. kwa sasa naona umeamua kuja kwa style nyingine tofauti kabisa. rai yangu kubwa kwetu sote ni kwamba naomba tusipende kuwachimba sana hawa ndugu zetu wa TISS kwa kuwa wanayoyafanya ni kwa maslahi ya taifa zima la Tanzania pasipo kujalia itikadi zetu. kuelimishana kuhusu taaluma hii kongwe ya ujajusi si vibaya sana lakini naomba tujiwekee mipaka ya vitu vya kuuliza.
Long live Tanzania.
"Das Billige ist immer das Teuerste"

Mkuu unayosema Ni kweli kabisa.Lakini ndugu zetu wazalendo Ni vizuri kujua sisi wananchi tunajua nini ili waweze kuunda mipango mipya ya kulinda hadhi ya taasisi Na Kwa usalama wa nchi kwa ujumla.Leo Hii ukiingia YouTube unaona kila kitu kuhusu ujasusi uliobobea.
Kwa Mfano hackers wanaingia kwenye mitandao ya majeshi,makampuni Na mabenki Kwa hiyo hizo taasisi zinajihami kila kukicha.
Vile vile kuna taasisi zinaomba mahackers wawajaribu.
Kwa maoni yangu tuuelimishane Na kuwaelimisha Ndugu zetu wazalendo ili wawe wakali zaidi.
 
mkuu, asante sana, na bila shaka wahusika wenyewe watakuwa wamekuelewa vizuri mno
 
wakuu de'levis Yericko Nyerere na Freelancer and the rest, kwa namna dola la kiislam la Iran lilivyo fully alert kiusalama kwa kujua fika ya kwamba nchi za ulaya na marekani zinataka kuisambaratisha kama walivyoitafuna na kuichanachana taifa la Iraq ya Saddam Hussein, mnafikiri ni umakini mkubwa kiasi gani "intelligence officers" wa mossad, cia, MI6 na idara zingine za kijasusi za kimagharibi zinatumia kukusanya taarifa ndani ya Iran via human means (achilia mbali satellite surveillance)? ama tuseme the west no longer run human spy rings in persian soil???!!!!!!!!!!
 
Mambo yote juu ya ujasusi yamo katika kitabu changu kiitwacho ujasusi wa kidola na kiuchumi...

Kipakue hapa mkuu.

Amazon product ASIN B01GPXFDB6
 
Pia, nasikia pana njia ya kuhama makazi kutoka mji mmoja hadi mwingine huku taarifa zikichukuliwa wakati wanafanya mishe mishe za kuhama mji au nyumba .

Yaani, aliyefata taarifa anakuwa ndiye anayehamisha vyombo au mzigo kwa kuelekezwa na mtoa taarifa . kwa hiyo muda huo unatumika kuchukua taarifa wakati wako katika mizunguko hiyo ya kuhama aidha nyumba, chumba au mji.na kwenda kwengine kuliko andaliwa.

Japo, hii ni rahisi sana kufanikiwa kwa sababu ya tamaduni zetu waafrika kusaidiana wakati wa tukio kama hilo la kuhama.

Pia, ili kuwachanganya watu zaidi,.wanabeba vitu vyote wakivipeleka mahala palipoandaliwa kisha wanavirudisha kwa kutoa kisingizio kuwa nyumba au chumba ni kidogo au siyo pazuri ili katika hizo purukushani Yale.mabadilisho ya taarifa yaweza kufana na kutotiliwa shaka.

Au hata hao wawili kubadilishana nyumba ama vyumba, huwa nayo ni njia moja wapo na rahisi sana tena haina utiliwaji mashaka na.mtu au vyombo vya usalama vya sehemu au nchi husika!

Nyingine zipo nyingi, nazi-upload kutoka moyoni kuja hapa JF nitaendelea.....
 
Habari wakuu, natumai wote ni wazima. Napenda kuwaletea thread kuhusu Espionage au Intelligence. Espionage ni nini? Espionage ni kitendo cha kukusanya taarifa au nyaraka muhimu za nchi/taifa au taasisi kubwa. Taarifa hizo zaweza kua za biashara, siasa au nguvu ya jeshi la taifa jingine nk na kuzihamisha au peleka sehemu zinapotakiwa kwenda.

Kumbuka kuwa, taarifa hizi hupatikana kupitia njia za kwa siri kwahiyo lazima zifichwe ili yule anayechunguzwa asiweze gundua kile kinachoendelea, na vile vile ni kwa ajili ya kulinda usalama wa taarifa zenyewe, yaani taarifa zifike zikiwa katika ubora unaohitajika.

Thread hii inalenga kuzitaja njia zitumikazo kuhamisha {transmit or communicate} taarifa za kijasusi. Taarifa zikishapatikana zinahitaji kufanyiwa kazi au kuchunguzwa, sasa taarifa haiwezi chunguzwa kama haijafika pale panapostahili.

· Kwa kutumia geresha ya sigara au kiko

Hii njia hupendwa kwasababu si rahisi, katika hali ya kawaida mtu kufikiri kuwa, ndani ya sigara anayovuta spy kunaweza kuwa na ujumbe wa kiintelejinsia. Pia ni njia rahisi kwa usalama wa spy huyo maana kama akigundulika au akishukiwa, basi huweza poteza ushahidi kwa kuuchoma kama vile anavuta sigara.

· Kwa kutumia soli za viatu

Kwenye soli ya kiatu kunakuwa na nafasi ndogo ambayo imetengenezwa (chamber) ili kuweza kuhifadhi taarifa ndogo ndogo. Mfano memory cards zinaweza fichwa hapo. Njia hii ilipendwa sana na warusi maana ilikuwa, japokuwa inaonekana ndogo lakini ina uwezo mkubwa. Memory card iliyofichwa kwenye soli inaweza kuwa na mafile ya picha hadi 500–10000. Au mafaili ya audio records 1000 kutegemea na ukubwa wa device.

· Kwa kutumia michoro (tattoo) kwenye visogo, kisha kuotesha nywele kwenye maeneo hayo ya kisogo upya

Njia hii inatumika kwasababu ya usiri wake. Si rahisi mtu kumshuku spy kama anaweza kua ameficha taarifa kwenye kisogo chake kwa kutumia michoro. Kwaiyo ujumbe au taarifa zinaweza kuonekana pale tu baada ya Spy huyo kunyolewa nywele na kupaka kimiminika ( chemical ) sahihi kisogoni kwake.

· Kwa kutumia macho feki

Hii njia inatumika kwa kuchukua kipande cha kioo ( lenzi ) na kuweka kwenye macho, ila nyuma ya lenzi iyo kuna kua na nafasi ndogo ya kuweza kuhifadhi devices ndogo kama micro chips ambazo zinakua zimehifadhi taarifa muhimu.

· Kwa kutumia sarafu au shillingi

Hii shillingi huonekana kuwa ni ndogo kwa mtazamo, ila zinakuwa na katundu kadogo kadogo ambacho hakaonekani kirahisi, ambacho ukichukua pini na kuipenyeza kwenye ako katundu basi shillingi hiyoinajifungua kati kati au nusu kwa nusu. Katikati unaweza tunza micro chips au memory cards ambayo inaweza kua na taarifa yenye hata kurasa 50 au zaidi.

· Kwa kutumia karatasi maalumu

Hii ni karatasi ambayo, kwa mtazamo inakua tupu yaani haina maandishi kwaiyo sio rahisi kwa mtu kuishuku. Ila ukweli ni kuwa, karatasi hii inakuwa imebeba ujumbe ndani yake. Ujumbe huu huweza kuonekana kwa kuchemsha iyo karatasi kwenye vimiminika vya kemikali sahihi, au maji nk

· Kwa kutumia dead drop

Hapa taarifa hufichwa kwenye eneo ambalo linajulikana kabla au mapema, na baada ya muda mfupi, mtu mwingine anaenda kuzichukua. Njia hii ni maarafu sana na inatumika sana, ni kama zile the most celebrated kamasutra positions hahaha. Faida yake ni kuwa, inazuia nafasi za yule anayeficha taarifa na mpokeaji kukutana uso kwa uso au kuwa wote pamoja kwa wakati mmoja katika eneo husika. Hivyo basi, hata ikitokea muhusika anafuatilia (kama ni double agent ) anaweza akajitetea, na hasa kama eneo lenyewe ni kama kwenye garden, anaweza sema kuwa ameenda kupunga upepo nk.

Taarifa inaweza wekwa kwenye mfuko wa takataka, kinyesi cha ng’ombe au sehemu yeyote ile ambayo itamfanya mpita njia akiona asiweze kupata kishawishi cha kutaka kuchukua au kudadisi hizo taarifa.

· Kwa kutumia mizoga ya wanyama

Mnyama ( panya, paka, sungura nk ) mwenye umbo dogo, ambae yupo hai, anauawa, kisha taarifa za siri zinawekwa ndani yake, anashonwa kwa operation. Baada ya hapo hatua inayofutia ndo muhimu zaidi na ndiyo inayoleta tofauti ( usiri ).

Mnyama huyo hunyunyuziwa vimiminika vya kemikali ambavyo hufanya aoze na kutoa harufu mbaya ambayo ni kero kwa watu na hata wanyama ambao katika hali ya kawaida huwa wanakula jamii iyo ya wanyama (mzoga) kuchukizwa na hyo harufu na kupuuzia huo mzoga, kisha hutupwa kwenye eneo husika au lililokusudiwa ili muhuika wa upande mwingine aweze kuona na kuchukua taarifa hizo.

Kama unafahamu njia zingine, pls share..

Link iyo hapo chini, BBC waki-report maisha ya double agent wao toka anajua recruited mpaka ana deflect. Ni Tanzania tu ambapo inaonekana sio sahihi ila sio uko walipoendelea
Kim Philby, British double agent, reveals all in secret video - BBC News
Espionage kama taaluma kuna mambo chungu zima.
--- kukamata majaususi wa adui wanao operate ndani ya nchi na Ku intercept mipango yao.
--- kuna kufuatilia mienendo ya viongozi wa serikali wa ngazi za juu pamoja na watumishi wa idara husika ya ujasusi kama wanaenenda na viapo vyao ( oath of office )
--- kulinda miundo mbinu muhimu kwa nchi kama petroleum pamoja na food reserves dhidi ya mashambulizi ya adui.
--- majasusi wa kijeshi (military intelligence) wao wanafanya tathmini ya hatari ya uvamizi wa kijeshi kutoka nchi yoyote ya jirani pamoja na ku verify military readiness ya jeshi kwenye kujibu mashambulizi ya ghafla ya adui.
--- intelligence inawezesha kupatikana kwa taarifa zitazowezesha policy makers kuunda sera za mahusiano ya nchi za nje pamoja na namna nzima ya kuendesha serikali.

Ujasusi ni somo moja refu sana wadogo zangu.
 
Back
Top Bottom