Mzee wa kupambania
JF-Expert Member
- Aug 14, 2022
- 21,111
- 53,092
PoaSawa. Ukileta unitag nije kusoma madini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
PoaSawa. Ukileta unitag nije kusoma madini
Katikati ya jiji la Madrid, kuna hekalu la soka linalo vutia na kuakisi historia tajiri isiyolinganishwa popote kwenye mchezo huu mzuri wa soka.
Estadio Santiago de Bernabéu, ni maskani ya klabu ya Real Madrid,
hauna haja ya kufafanuliwa sana kuhusu hekalu huli.
Kwa hadithi zake za kuvutia, usanifu wa wa kipekee, na uwezo wa kuchukua maelfu ya mashabiki,
uwanja huu ni moja kati ya alama zenye ishara ya utukufu wachezo wa soka.
Mizizi ya Estadio Santiago Bernabéu inarudi nyuma hadi mwaka 1944 ambapo ujenzi wake ulianza chini ya uongozi wa Rais wa kipekee wa Real Madrid kwa wakati huo, Santiago Bernabéu Yeste.
Siku za awali, uwanja huu ulikuwa mdogo, ukiweza kuchukua watazamaji 75,000 tu, baada ya Kupita miaka, uwanja ulifanyiwa ukarabati mara kadhaa, hadi kufikia hapa ulipo sasa.
Muundo wa uwanja huu ume sanifiwa vema sana hada sana ya muonekana wake na eneo la kucheza soka, siti zake kwa mtindo wa kisasa na wa kihistoria.
Umbo lake la duara limehakikisha kila kiti kinapata mtazamo mzuri wa uwanjani, hivyo kuwawezesha mashabiki wote kushudia vyema kabisa mchezo kila wanapoingia kwenye lango lake takatifu.
Moja ya sifa nyingine kipekee ya uwanja huu ni paa lake linaloweza kufunguka na kufunga.
Paa hili la kutumia teknolojia ya kufunguka na kufunga kwa mitambo ni alama ya ubunufu na umaridadi wa Santiago Bernabeu
Hata hivyo, kivutio kikuu ni ukuta wake wa nje wenye madirisha ya skriniwe uwezo wa kuufanya uwanja huu kunadirika rangi au kuonesha vicha za video mbali mbali.
Skrini hizi kubwa zenye kuonesha matukio mbalimbali wakati wa mechi, na kumfanya hata alie nje ya uwanja kuenjoy soka kama alie ndani.
Estadio Santiago de Bernabéu umeshuhudia nyakati nyingi bora za kihistoria katika soka.
Kutoka kwa wachezaji maarufu na wakubwa, walio vuja jasho uwanjani wakati wa mapambano ya mechi za kukata na shoka,
uwanja huu umeshuhudia ushindi na kushindwa kwa wachezaji bora wa soka.
Ni hapa ambapo Real Madrid imebeba vikombe vingi vya ndani na kimataifa, ikijiweka katika rekodi kuwa klabu klabu iliyo fanikiwa zaidi kwenye soka.
Upepo wa uwanja huu unapo vuma unawapa wachezaji wa timu ya nyumbani hisia za ushindi na kuufanya uwanja kuwa moja ya uwanja mgumu kwa wapinzani kupata matokeo.
Mpira wa miguu hauna maana bila mashabiki na Estadio Santiago de Bernabéu ina mashabiki walio pagawa na wenye shangwe zaidi ulimwenguni wanajulikana kama THE WHITES ama Los Brancos .
Siku za mechi, uwanja huu hujaa full haouse tena bila hamasa za kwenye mwendo kasi na mashabiki hushangilia na kupiga kelele kwa timu yao pendwa muda wote na uwiano usiobadilika bila kujali matokeo!
Kipindi cha "Galácticos" cha Real Madrid ili jizolea umaarufu na uwanja huu ulivutia mashabiki na wapenzi kutoka kila kona ya dunia.
Mkusanyiko wa jezi za rangi nyeupe na bendera zinazorushwa kwa pamoja huleta hisia murua sana wakati wa mechi na kufanya kutembelea uwanja huu kuwa jambo la kusosimua mnoo lisioweza kusahaulika.
Estadio Santiago de Bernabéu ni zaidi ya uwanja tu, ni ishara ya urithi wa Real Madrid na mchezo wa soka kwa ujumla kutoka kwa kizazi na kizazi.
Unasimama kama ishara ya umoja, undugu, na ubora na tumaini,
ukivutia mamilioni kwa utukufu wake.
Kama wewe ni shabiki wa soka au mtazamaji wa basi kutembelea hekalu hili la soka ni moja ya ndoto yako.
Hapo ndio Estadio Santiago dé Bernabeu ukifika jiji la Madrid Hispanja iliza yoyote atakuelekeza.
Camp nou haifiki hata kwa WandaMetrapolitanoUsifananishe hekalu la soka na upuuzi.
Camp Nou uwanja mkubwa ila limekaa kishamba, hata paa halina.
Ni kama timu zao tu. Madrid imekaa kishua, barca ipo ki local sana. Madrid wana noti hawalii njaa, barca kila wakati mayowe ya ukata hadi wakamuuza Messi ghafla kipindi kile.
Ngoja waje waswahili wenye barca yao na utimu kwenye kila jambo, hawatokuelewaCamp now haifiki hata kwa WandaMetrapolitano
Ukikutana na watu wa aina hiyo una achana bao sio kila mtu aelewe,Ngoja waje waswahili wenye barca yao na utimu kwenye kila jambo, hawatokuelewa
Camp now ndio nini?Camp now haifiki hata kwa WandaMetrapolitano
Sahihi mkuuUkikutana na watu wa aina hiyo una achana bao sio kila mtu aelewe,
Kwenye sekta ipi ukiachana na idadi ya viti/siti?Haijafikia Camp Nou
Santiago bernabeu ndio best veue kwa sasa DunianiMkuu umuelezea vizuri kabisa uwanja huu, ambao ni kivutio kikubwa hapa Earth-ni.
Kingine umesahau kukiweka, ni ile technology ya best RETRACTABLE PITCH in the GALAXY.
Hiyo pitch iiyo juu, inaweza kurudishwa chini, af kuna pich iliyo chini ikapanda juu. Kiwanja kimoja, kina viwanja kibao ndani yake, kwa ajili ya michezo mbalimbali.
Sawa,anachokosea mwana Barcelona mwenzangu ni kuwa uzi unazungumzia uwanja wa jamaa zetu,ata yeye afungue tu uzi unaozungumzia La Masia haina shida.naitwa Masanja Mayunga natokea Mwanza.nimefika Darasalama juzi usiku.
nilikua naomba mwenye fesi buku na wasapu aniuzie niweke kwenye simu yangu ni mpya mjomba kaninunulia, au munielekeze duka wanalouza huko kalaakoo.
wabheja sana nkoi.
OHata ziwe siku mbili, imeshakamilika, na mtoa mada kaizungumzia EdSB na historia yake tangu mwaka 1944.
Wewe upo hapo na stori za asilimia, stuka ohooo!