Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Asante sana Mkuu Nanye Go , ni faraja sana kwa jf kuwa na watu wenye objectivity ya kiwango chako, watu wengi humu ambao ni mashabiki wa Chadema, wako very negative kwa kila anayeikosoa Chadema, wanamuona ana chuki na Chadema, hivyo mtu hata ukitoa ushauri mzuri kwa Chadema, unapokelewa negatively, mfano mzuri ni ushauri huu Elections 2015 - Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ... hivyo kwenye hii issue ya hawa wabunge, ushauri wangu ni huu Wana macho lakini hawaoni, wana masikio lakini hawasikii. CHADEMA wana macho? Je, wawasamehe Wabunge 19 wabarikiwe, au wakomae nao walaaniwe?Kaka najua una nia nzuri, lakini hili swala lao mi naliona ni zaidi ya hiyo nia nzuri uipendayo.
Hapa ndipo mzizi wa fitna ulipolalia, kuna vitu 5, katiba, sheria, taratibu, kanuni na haki.Swala hili liko kisheria na kanuni zaidi.
- Katiba- ili mtu uwe Mbunge ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa. Baada ya CC ya Chadema kuwavua uanachama, from that moment, kikatiba wanapoteza sifa za kuwa wabunge. Hili halikufanyika kwasababu kwasababu wabunge wale wametimuliwa Chadema kinyume cha katiba ya Chadema!.
- Kisheria- Unapofutwa uanachama na chama chako, automatically unakuwa sio mwanachama halali kisheria, hivyo wabunge wale wanaendelea kupeta bungeni kinyume cha katiba na kinyume cha sheria za nchi, kwasababu Chadema hawakufuata mkondo wa sheria kuwashughulikia.
- Taratibu za kuwatimua kwa mujibu wa katiba ya Chadema, hazikufuatwa.
- Kanuni za haki za no one is condemned unheard, haikufuata.
- Hivyo uamuzi wa CC ya Chadema kuwatimua sio uamuzi haki, NEC, Bunge limeamua kuwakingia kifua ili haki yao ipatikane, hata kama wanamakosa ya Kughushi, kosa lithibitishwe, wahukumiwe kwa haki, hata kama ni kufukuzwa, then wafukuzwe kwa haki, kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni. Sheria na Haki ni vitu viwili tofauti kabisa!.
Hili kosa la kujipeleka, lithibitishwe!. NEC wana barua ya uteuzi kutoka Chadema, it's legit bonafide genuine ndio maana Chadema hawajaripoti jinai ya forgeryHawa wadada wanafahamu walikosea, kukaidi maamuzi ya chama chao na kujipeleka bungeni.
Rushwa pia ni kosa la jinai, if they can proof this,it's a crime, this is criminal, hivyo there is criminal liabilities that needs evidence to be proved sheria ifuate mkondo wake.Ofa ya ccm kuwapeleka bungeni was too good for them to refuse. Walipokea rushwa kwa shingo upande,
Hili nakubaliana na wewe, kwasababu hawa ni wabunge wa viti maalum, wangekuwa ni wabunge wa kuchaguliwa, baada ya kuchaguliwa na wananchi, wanakuwa ni wakubwa kuliko chama, wanakuwa ni watumishi wa wananchi The Doctrine ya Mwanasiasa Kuwa Maarufu Kuliko Chama!-Ni "Utumishi wa Watu VS Utumishi wa Chamalakini walipokea ubunge bila ridhaa ya chama, na bila chama wasinge ingia bungeni. Kwa maana nyingine wao sio wakubwa kuliko chama chao.
Nakubaliana na weweSasa kesi zile ni kutaka muafaka kisheria na sio swala la nia nzuri, na wewe ni mtaalam wa sheria. Kesi siyo ugomvi, ila ni njiaau utaratibu mzuri tuliojiwekea kupata haki. Kwa mantiki hiyo sioni ugomvi kati ya Halima na wenzake dhidi ya Viongozi wa chama, naamini wana mahusiano mazuri ila kuna taratibu lazima zifuatwe ili waweze kurejea kwenye chama chao, hili siyo swala la Mbowe au Lisu bali ni swala la kisheria na kanuni za taasisi ya chadema, siyo HURUMA au mapenzi ya mtu.
Taratibu za kisheria zimekamilika kwa hukumu ile ya mahakama Kuu, imebariki kufukuzwa kwao na CC ya Chadema, ila rufaa ndio isikilizwe upya, hivyo kesi imekwisha.Watasamehewa lakini baada ya taratibu za kisheria kwisha.
Nimewaombea msamaha kwasababu kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mwanachama akifungua kesi mahakamani dhidi ya chama, kesi ikiisha, akishindwa anakuwa amejifukuzisha uanachama wake kwa mtindo wa final and conclusive.
Happy New Year
P