LGE2024 Ester Thomas (ACT Wazalendo): Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Watiania Msikubali Kutishwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Bara, Ester Thomas amesema ACT Wazalendo imejipanga vyema kuhakikisha wanachama wake waliotia nia kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wanapata msaada wa kisheria katika kipindi cha uhitaji. Amesema maneno hayo leo Oktoba 23 Jijini Mwanza wakati akizungumza na watia nia wa Mitaa ya majimbo ya Nyamagana na Ilemela.

"Madhali umetia nia kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Naomba simama imara, usitetereke, usiwe na hofu na wala usikubali kutishwa. Chama kiko pamoja na wewe. Pia tuna Wanasheria; ambao wako tayari kukusaidia wakati wowote." amesema Ester Thomas.

Aidha, Bi. Ester Thomas amewakumbusha watia nia hao dhima na wajibu wa Mwenyekiti wa Mtaa kwenye maendeleo ya mtaa. Amesema kwenye mitaa na vijiji ndiko wanakoishi wananchi na huko ndiko inapopita na kufanyika miradi ya maendeleo.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji utafanyika Novemba 27, 2024 na ACT Wazalendo ni miongoni mwa vyama vinavyokwenda kushiriki uchaguzi huo.
 
 

Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
    420.8 KB · Views: 3
kwani wanatishwa na nani wagombea uongozi wa ACT?🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…