Esther Matiko: Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa "unakaguliwa na hata kama ni Mama utaruka kichurachura"

Esther Matiko: Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa "unakaguliwa na hata kama ni Mama utaruka kichurachura"

Solution inayohitajika hapa ni ileeee ya KUWABAMIZA hao wahalifu wenzio ili wakitoka wawe na stori ya kukusimulieni nyie wahujumu wa taifa, walarushwa, mafisadi, wapiga dili na wachochezi na wavuruga-amani ya nchi. Umeelewa, umelewa, ama umeelemewa?
Hakuna mwenye guarantee ya kutokwenda jela either kwa kutenda au kusingiziwa. Hivyo usijione upo salama.

BTW, siku ukiingia halafu wakakutia vidole na wakuchungulie kwenye tundu lako la haja kubwa ndio utajua umuhimu wa hili linalozungumzwa.
 
Mimi mwenyewe niliacha jeshi kwa sababu kama hizo eti siku ya interview unavua nguo zote unainamishwa unakaguliwa kwenye makalio kama nywele za makalio zipo.

Tanzania bado baadhi ya taasisi zina mifumo ya ajabu sana.
 
Mbunge huyu ana hoja ya maana hata kama ni wa chadema.Imagine mama yako mzazi,dada yako,mkeo,mwanao wa kike yupo kwenye siku zake anabaki uchi anaruka kichura chura ili akaguliwe.Nimejiskia vibaya sana kwa kitendo hiki kufanyiwa mtu.Lakini ewe Binti Matiko sherua si zinatungwa huko Bungeni?wekeni sheria sawa sio kula posho na kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.Pia msisahau kurekebisha fao la kujitoa ni ukoloni mambo leo.Nchi a wenzetu zilizoendelea unaweza kukopeshwa hata kama huna dhamana ukiwapa business proposal wakiichambua unakopa,sisi tumekazania vitu vya kikoloni.Shangaeni kwa wenzetu mtu ana miaka 18 amemaliza chuo kikuu sisi tunaingia madarasa na madarasa bila kujua tulifanyiwa vile ili kucheleweshwa.
Bora uingie kaburini lakini siyo haya magereza ya kibongo
 
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Matiko, ameitaka Serikali kufunga mashine maalum kwenye Magereza ili kuondoa malalamiko ya Wafungwa kukaguliwa wakiwa uchi wa mnyama jambo ambalo ni kinyume na Haki za Binadamu.

“Unapoingia Segerea unavuliwa nguo zote, unaambiwa unakaguliwa na hata kama ni mama upo kwenye siku zako utaruka kichurachura ili waone kama kuna kitu umeficha huku chini"- Ameeleza Esther Matiko.

Tuwe na vifaa vya kisasa vya ukaguzi, kama kuna kitu ameweka tumboni kitaonekana kuliko wanavyofanya sasa hivi, ni udhalilishaji

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema ukaguzi wa namna hiyo ni mapokeo ya kikoloni na yanaondoa Utu wa Mtu kwasababu sio sawa kwa Wanawake na hata Wanaume kukaguliwa kwa hali ya udhalilishaji.

Aidha, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemtaka Mbunge kuweka wazi ni wapi matukio kama hayo yanafanyika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua.
Hiyo ni sehemu ndogo sana ya ukiukwaji wa haki za binadamu maeneo ya magereza na zile mahabusu za police ingawa kasheshe za magereza ni maradufu kwa ukiukwaji wa haki za binadamu. Tena wao ni vile wanakuwa na chambichambi za rushwa kuwahonga nyapara na askari magereza.

Kuna mateso na utesi wa kila aina ni vile tu hakuna taarifa za wazi

Kwa kifupi usiwe sababu ya mwingine kuingia kule hasa kwa uonezi.

.
 
Mimi mwenyewe niliacha jeshi kwa sababu kama hizo eti siku ya interview unavua nguo zote unainamishwa unakaguliwa kwenye makalio kama nywele za makalio zipo.

Tanzania bado baadhi ya taasisi zina mifumo ya ajabu sana.
Tetetete, sheria za serikali ya CCM
 
Gereza ni dunia nyingine kabisa!

Ova
 
Hakuna mwenye guarantee ya kutokwenda jela either kwa kutenda au kusingiziwa. Hivyo usijione upo salama.

BTW, siku ukiingia halafu wakakutia vidole na wakuchungulie kwenye tundu lako la haja kubwa ndio utajua umuhimu wa hili linalozungumzwa.

Wewe ni mshamba kama washamba wengine. Mhalifu hana haki; aliipoteza baada ya kuamua kuvunja sheria za nchi. Sasa unataka useless people kama hao wawe treated kama watalii kuleee kwenye hoteli za mbuga ya Serengeti na Mlima Kilimanjaro!???
 
Solution inayohitajika hapa ni ileeee ya KUWABAMIZA hao wahalifu wenzio ili wakitoka wawe na stori ya kukusimulieni nyie wahujumu wa taifa, walarushwa, mafisadi, wapiga dili na wachochezi na wavuruga-amani ya nchi. Umeelewa, umelewa, ama umeelemewa?
Ungejua kuwa sio wote wanaoingia magereza wanakuwa na hatia usingeandika huo upuuzi!
 
OK nyumba ya wote ile mkuu acha kashifa sio vizuri

Unamjua mhalifu wewe, au unasimuliwa tu!??? Imagine yule kijana A Town aliyembaka mbibi, then akamnyonga. Be serious sometimes, sawa!??? Tena nasema sheria hukoooo ziwekwe kando watu waminywe haswa hadi akili ziwakae kumkichwa.
 
Ungejua kuwa sio wote wanaoingia magereza wanakuwa na hatia usingeandika huo upuuzi!

Sasa hapo ni kosa la gereza au wanasheria wako!??? Peleka ushahidi mahakamani ili hao watu wako wasiokuwa na hatia waachiwe huru, sawa!??? Acha kupika uongo kwa kusudi tu la kupiga kelele za bure.

Lipi la maana --- usidhani kuna muwali wowote kwamba sheria ivunjwe ili kuacha kuwapatia wahalifu halali stahiki zao za mikikimikiki gerezani kwa kuhofia eti kwamba kuna wafungwa hewa miongoni mwao ambao, allegedly, wamo humo kimakosa, umeelewa!???
 
Prison is not home! ndio maana kunatisha ili watu wasitende makosa!!!!ndio maana ni laaana ya vizazi na vizazi kwa mtu anayemsingizia mtu kosa ili ampeleke pasipo hatia.

Kuna wahalifu hasa wanawake wanaweza kuingia na vitu vya hatari kwa usalama wa wanaowalinda au watuhumiwa wengine.

Yeye kama mbunge ambaye ni muhimili wa dola angetoa njia sahihi ya kupekua na siyo kulalamika.
Watu wanabambikwa kesi za uhujumu uchumi, mara pembe za ndovu n.k acha kutetea ujinga nchi yetu imejaa uonevu, kuna mwanafunzi Hai amefungwa miaka 3 kwa kuonewa, demu kaibuka kwenye vyombo vya habari kasema ukweli tena mwaka huu, wengi wamefungwa kwa uonevu. kufungwa ni kufungwa tu hata ukifungiwa Impala hotel pazuri kuliko hata kwako lakini uhuru wa mtu ni kitu kingine kabisa.
 
Huyo Ndugai hajui kama CCM ni mkoloni mweusi, mambo tunayofanyiana ni ya kijinga hata mkoloni mweupe akituona atatucheka, waliondoka wakoloni weupe physically but mentally wametuachia urithi.
Bora wakoloni yaani tumeachiwa mashetani kabisa
 
Prison is not home! ndio maana kunatisha ili watu wasitende makosa!!!!ndio maana ni laaana ya vizazi na vizazi kwa mtu anayemsingizia mtu kosa ili ampeleke pasipo hatia.

Kuna wahalifu hasa wanawake wanaweza kuingia na vitu vya hatari kwa usalama wa wanaowalinda au watuhumiwa wengine.

Yeye kama mbunge ambaye ni muhimili wa dola angetoa njia sahihi ya kupekua na siyo kulalamika.
aisee muwe mnasoma thread mpaka mwisho kabla hamjatoa maoni yenu.
 
Kama nchi tuna mifumo ya hovyo sana sana hivi kweli Karne ya 21 Bado huo upuuzi unaendelea ni aibu kubwa sana yaani daaaaa
Hivi mbaka hua najiuliza sie waafrika hatuna akili za kujiongeza au tunasubiri mbaka mabeberu yatoe order kwamba hebu achaneni na kicho fanyeni hivi!
Ndio sisi Kama makondoo tuwafuate
Maana Kuna vitu Kama binadamu tuliokamilika hatuhitaji kujifikiria mara mbili kuvifanyia marekebisho!
Hatari sn na nusu mkuu
 
Yaan magereza yote tz lazima uvue nguo zote halafu unaweka mikono nyuma kama watumwa harafu unalazimshwa unye kwenye "MTONDOO" ndoo zile bati usipokunya kesho unakunywa bakuli la uji wamoto halafu kunya kuna kuhusu sio mchezo[emoji35][emoji35]
 
Back
Top Bottom