Kimsingi mi si mchangiaji wajukwaa hili lakini kwa kuwa nimekutana na uzi unaomhusu mtu ambaye kwa namna moja ama nyingine ninadhani aweza kuwa msaada kwa Taifa langu na ikibidi kwa Ulimwengu mzima sioni kama kuna ubaya nami kutia neno langu japo sitaki kuamini kuwa neno hili ni lazima limfae Esther Wassira.
Kwanza nakiri kuwa Esther ana kipaji ama vipaji vingi na kwa upekee vipaji hivyo vyaweza kuwa na nguvu sawa ama kipo chenye nguvu zaidi kuliko vingine,lakini mimi naamini mtu hawezi kuwa na vipaji vyote vyenye usawa.Vipaji vya Esther ni Kuimba labda na utunzi wa nyimbo,Yawezekana akipewa nafasi ya kuigiza aweza kuwa mzuri pia kwa kuwa kuigiza kwa namana fulani kuna mahusiano na mambo ya muziki,ana karama ya uongozi,ana karama ya siasa na pia yeye ni mwanasheria kitaaluma na kama sikosei yeye ni mkurugenzi sehemu fulani,kwa hakika huyu ni mtu muhimu na mwenye kustahili pongezi ambapo yeye atamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia karama lukuki zinazokwenda na bahati.
Esther Wassira,mimi nadhani kuwa na vipaji vingi ni jambo la kheri na ukifanikiwa kuvitumia vema kwa manufaa yako binafsi,familia yako na hata Taifa lako.Ukivitumia vipawa hivi si tu vitakuondoa ktk maisha ya utegemezi lakini pia kuyaishi maisha uyapendayo.Na ukweli ni kwamba uko huru sana kutumia vipaji vyako kukufikisha utakapo na ktk matarajio ya juu sana ili kujiridhisha upendavyo.
Karama hizo kwa jinsi zilivyo zinaweza kukinzana wakati fulani,nafahamu na ninaamini kuwa unafahamu kuwa shabiki wako wa maigizo si lazima akukubali kwenye uimbaji,shabiki wako wa siasa si lazima awe shabiki wako wa maisha yako binafsi na kuna uwezekano mashabiki wa maeneo niliyoyataja asiwe shabiki wa uongozi wako eneo fulani.Na mimi naamini kuwa wewe unauwezo wa kufanya mambo makubwa kwenye lile unalolipenda zaidi na nina uhakika utapendwa sana,ili usipotee wala kupotea kwenye njia inayokufaa,Tafadhali simama vema,kaa chini,Tafakari sana,pembua in three-dimension kuwa wewe sasa maisha yako yanatuhusu watanzani japo ktk chama wewe ni mwanachama wa kawaida lakini tunayoimani kuwa utakuja kuwa mtu fulani ktk chama na baadae ktk Taifa.
Siamini mtu akiwa multi-talented basi atumie kila kipaji chake kwa saababu tu ana kipaji hicho,kuna uwekano wa kuyumba na kupoteza muelekeo kwakuwa niaminivyo mimi hakuna anayefit kila pahala on the same.Esther Watz wamekupokea kwa kuamini wewe ni kijana mwenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja,unaejiamini na ambaye uko tayari kuyafia mabadiliko kwa nchi yako.Sasa kama wewe ni mvuta sigara basi usishauriwe kutovuta sigara?Je,kama wewe najiuza basi tukuache utumie kipaji chako cha kupenda kujiuza basi usishauriwe?Kuna wezi na wanjua kuwa wizi ni kosa kisheria lakini watu hawaachi kwa kuwa ni karama zao,je tusiwashauri?Sitaki kusema kusema kuwa una vipaji vibaya hapana,kuna watu wanajua kuwa wewe ni mwanasheria lakini hawazidi idadi ya watu wanaojua kuwa wewe ni mwanamabadiilko(mwasiasa),Tunaiheshimu sana career yako ya sheria na tunajua ktk siasa waweza kutumia sheria kutulinda na kutuongoza kisiasa,hii ni taaluma ambayo umeisotea kuipata na labda pia imesaida kukjenga kimwonekano na kifikra,Unaimba ni sawa,wewe ni mkurugenzi sehemu fulani ni sawa na pengine una karama yako ya uigizaji ni sawa.
Tunapenda kuona Esther wassira mwenye uchaguzi sahihi kwa wakati sahihi,wewe sasa maisha yako si mali yako peke yako,watz nao wanafuatilia kwa ukaribu na wangependa kujifunza toka kwako.Ni kweli hauna nafasi nyeti ktk chama na pia serikalini lakini ushaaminiwa so si vizuri kuonesha kuwa wewe hujui kuchagua mambo sahihi kwa wakati sahihi.Tungependa tukuone ukiwa kiongozi wa mfano na kama kijana chagua yale yanayopendwa na watu na kama mwanamke onyesha kuwa wewe ni wa tofauti wajua nini na na namna ya kufanya kiwe nini.Kuchanyanya mambo kuna punguz aimani kwako na hili nilisema the day ulipokaribishwa jukwaani(Jukwaa la siasa).
Esther Ukitambua kuwa kama kijana lazima ukubali kulelewa kiuongozi na kimikakati,kisiasa na kimaadili ili uweze kuwa kiongozi wa mfano na kuleta maendeleo kwa Taifa lako.Kazi ulonayo mbele yako ni kuwa makini na kila unalotaka kulifanya na kwa kweli sintofurahi hata kidogo pale nitakaapoona umeishia kuwa mpambaji wa magazeti ya udaku kwa mambo yanayokupunguzia heshima kama si kuiondoa kabisa ktk jamii.Tuishi ktk misingi ya uchaguzi wa nini kinafaa wakati gani ili tudumu.Ili Kudumu Esther kuna vitu inabidi umezee kidogo(kuwa mvumilivu ) ht kama mzuka umekupanda kiasi gani.Jaribu kuwa na control ya hisia na kile unachoamini kuwa unaliweza vinginevyo utapotea kwenye ramani ya siasa mara moja.Binafsi ningependa kuendelea kukuona ukiwa kwenye ulingo wa siasa kwa muda mrefu na kwa hadhi inayopanda na si kupungua ili kujenga historia nzuri kwa na mdogo wako Lilian na wengine weye nia hiyo huko mbeleni.
Mwisho napenda kukukumbusha kuwa nature ya siasa ni kuviziana,kufitiniana na kudhalilishana ili kupata nafasi kama si ridhaa ya kuongoza,ni vizuri kwa ushauri(Sheria ni career yako ishikilie kwa nguvu zote ili uweze kushauri na kujenga Taifa lisilo na uonezi),Kipawa chako cha siasa kitumie vizuri ili usijejutia siasa na ukiweza Musiki kuwa nao kama shabiki tu wala haito kugharimu na kama utaweza basi ukipandwa na mzuka jifungie chumbani imba sana mpaka mzuka uishe then ukitoka nje uko vizuri,Kuchanganya musiki na siasa kwa mara moja itakuondolea imani na ule upendo wa wananchi kwako japo nafahamu si wote.Simama kama mwanasiasa kijana mwenye maono na mwenye uwezo wa kupembua mambo ya kufanya na kusimamia unachokiamini ili kuondokana na dhana ya kuwa unaganga njaa,au kutafuta cheap popularity kwa nia fulani fulani.Kumbuka nilisema sehemu fulani kuwa watu ambao wanahistoria ya kupokelewa kwa nguvu mwanzoni hupotea haraka sana kwenye jambo lolote mifano ipo mingi naamini hata wewe unayo.Tumia karama zako vizuri na ujue kuchagua nini kinafaa wakati gani ili usijepoteza mwelekeo hata ndoto zako hazijatimia.
Nakutakia kila jema ktk ujenzi wa Taifa hili
IT CAN BE DONE,TAKE YOUR PART...!!