Tetesi: ESTIM kujenga barabara Kimara - Kibaha

Mhindi hua yuko vzr kwenye kukata hela/kishika uchumba pale anaposaka madili
 
Wakina Jeetu Patel,Manji,yule mhindi Shivacom/Rada scandal wote ni wazalendo na wanapenda Reputation kuliko pesa.
Yeah ndio kinachowatofautisha wao na wachina, wahindi tunaishi nao hapa nchi na wengi tu walishapata uraia na kuishi hapahapa bongo ila mchina ni watu wa kuchukua na kuondoka tu, ukiona mchina anaishi sana bongo basi huyo ana sababu zake ila sio kuwa mkazi rasmi wa hapa bongo, tofauti na wahindi
 
Ata bakhresa walimjengea nyumba yake anayoishi hadi hii leo masaki, ni muhindi mmoja anaitwa giri, anakaa mikocheni b.
Huyu mzee yupo simple sana, mkiwa naye site unaweza kumuita foreman tu..... muda mwingi kajiinamia
 
Una wasiwasi na Estim ama hutaki kwa vile ni ya kitanzania. Huoni miradi iliyofanya ama, Bagamoyo Msata kajenga nani? Massana Mbezi, Kinyrezi Kifurj, na zingine nyingi.
Lakini pia hela itabaki hapa Tanzania.
Kwa kuongezea Mbezi... Goba.. Tangibovu
 
Unajua kazi ya Bank ya Baroda na Bank of India hapa Tanzania?Chunguza hapo ndio utajua kama hela za wahindi zinabaki nchini au zinarudi India.

Au wao kua na makazi Bongo inakudatisha saaaana?
 
Estim kazi yake kujenga mkuu, anafuata mchoro wa consultant unasemaje..... hapo shida ipo kwa huyo mwenye kudesign
 
Unajua kazi ya Bank ya Baroda na Bank of India hapa Tanzania?Chunguza hapo ndio utajua kama hela za wahindi zinabaki nchini au zinarudi India.

Au wao kua na makazi Bongo inakudatisha saaaana?
Duuuuhh sio hivyo sikujua mkuu, ila issue ni kwamba hiyo ni kawaida tu kwa watu husika kutaka kufanya jambo lenye manufaa zaidi kwao, ila still kwani uwepo wa hizo bank hapa nchini zimekiuka sheria yoyote ile ya kiuchumi?, kwann na Tanzania wasipeleke BOT branch nyingine kule India na nchi zinginezo kadhaa?, sema tu wahindi wamejiongeza na wabongo tumezidi kulalalala tu mwishowe kulalamika mno, uwepo wa hizo banks hapa bongo sidhani kama ni kigezo tosha kuwafanya wahindi wawe watu wabaya, maana k7na marekani tuliokuwa tukipokea misaada yao na kufanya nchi ijae madeni kwa mikopo.
 


Lakini nakumbuka kuna uzi uliletwa hapa ukionesha barabara imepasuka, (sina uhakika kama ilikuwa kwa lengo la kuichafua kampuni au vinginevyo) kwa mtazamo wangu naona barabara iliyojengwa kwa kiwango kizuri ni ile inaanzia daraja mbili kwenda Iringa japo sijui ni kampuni gani iliijenga
 
Inakusaidia nini kuwa na njia sita kuanzia kimara-kibaha wakati huohuo kuingia mjini kuna barabara moja zinakuja 6 inatoka 1 msongamao hautapungua hapo ni matumizi mabaya ya fedha za mikopo
So?
 
Barabara toka daraja mbili pale msitu wa Simba mpaka Mafinga - Iringa urefu wa km 230 imejengwa na kampuni ya intaberton kutoka Denmark.

Pia ndo kampuni iliyojenga barabara ya Tunduma - Sumbawanga urefu wa km 215.

Barabara ya Iringa - Dodoma urefu wa km 260 imejengwa na kampuni ya kichina baada ya intaberton kukataa tenda kutokana na ufinyu wa bajeti.
 
Iyovi - mafinga ndio barabara bora Tanzania.
 


Unaweza kuhisi tofauti ya ladha ya barabara ukiingia kwenye hiyo njia, hata kama ulisinzia utagundua tofauti ni kubwa kabisa
 
Aliyejenga hiyo barabara kajenga katika ubora mzuri, angepewa tenda ya kujenga barabara nyingine nadhani zitakuwa zaidi.
Ile barabara hata dereva unajihisi hupo tz, barabara inaongea, usiku ndio usiseme, kitu kinaongea balaa
 
Unaweza kuhisi tofauti ya ladha ya barabara ukiingia kwenye hiyo njia, hata kama ulisinzia utagundua tofauti ni kubwa kabisa
Tatizo ni gharama Mkuu, intaberton wanapo Bid tender wanakuja na estimation cost kubwa kuliko hata bajeti..... Lakini mkiwapa kazi mtafurahi.

Kikawaida highways life span yake ni at least miaka 15 lakini hii ya Iyovi - Iringa - Mafinga inaweza kudumu hata miaka 22.
Hivi sasa ina miaka 10 lkn bado ipo Safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…