Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Ethiopia inafanya Uchaguzi Mkuu hii leo baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na mlipuko wa virusi vya corona na kutoa nafasi ya kukamilisha maandalizi.
Huu ni uchaguzi wa kwanza unaompa changamoto Waziri Mkuu na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Abiy Ahmed aliyeingia madarakani mwaka 2018, ukitajwa kuwa wenye ushindani mkubwa zaidi katika historia ya taifa hilo la pili barani Afrika kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu.
Abiy aliandika kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akiwatakia wananchi wote kila la heri katika uchaguzi huo.
Wananchi wanatarajiwa kuwachagua Wawakilishi wa Mikoa na Taifa, ambapo Wawakilishi wa Taifa watamchagua Waziri Mkuu na Rais - ambaye hushika nafasi isiyo ya kiutendaji.
Chama cha Abiy Ahmed cha Prosperity Party kimetoa Wagombea wengi zaidi wa nafasi ya Uwakilishi wa Kitaifa, hatua inayotarajiwa kumpa ushindi wa mtelezo Abiy katika kuunda serikali ijayo.
Zaidi ya Waethiopia milioni 38 wamejiandikisha kupiga kura Juni 21, lakini wengi hawatashiriki kupiga kura katika majimbo yote 547 nchini humo. Maeneo mengine yametajwa kutokuwa na usalama wa kutosha kushiriki katika uchaguzi huu huku katika maeneo mengine changamoto ya ufikishaji vitendeakazi vya uchaguzi kwa wakati vikisababisha wananchi kushindwa kupiga kura.
Awamu nyingine ya uchaguzi inatarajiwa kufanyika Septemba 6 ili kutoa nafasi kwa maeneo yaliyoshindwa kupiga kura hii leo. Hata hivyo, Ethiopia haijaweka tarehe rasmi ya kupiga kura kwa Jimbo la Tigray lenye uwakilishi wa viti 38 katika Bunge la Taifa ambapo zaidi ya watu 350,000 wanahitaji msaada wa kibinadamu kutokana na mzozo wa Mwezi Novemba mwaka 2020.
Waangalizi wa Uchaguzi wanaonya kuhusu uhalali wa uchaguzi huu kutokana na maeneo mengi kushindwa kukamilisha taratibu za uchaguzi kwa wakati. Katika siku za kawaida, Jeshi la nchi hiyo hutumika kuongeza nguvukazi ya kusambaza vifaa, lakini sehemu kubwa ya Jeshi lipo katika eneo la mapigano katika Jimbo la Tigray.
Baadhi ya vituo vya uchaguzi havikuwa na karatasi za kupigia kura kufikia siku ya Jumapili. Tayari kura zimeshaanza kupigwa katika baadhi ya maeneo siku ya Jumatatu, katika uchaguzi unaohusisha zaidi ya vyama 40 na wagombea 9,500.
Chanzo: AFP