Ethiopia: Updates on war against TPLF

Hiyo yenye nyota ya Daudi ya blue ndiyo Bendera ya Taifa hii ina lbebwa na Jeshi la taifa. Huyu mdada kwenye picha amejitwalia umaarufu sana kwenye Jeshi la taifa. Amekua frontline KIKAMILIFU. Vijana wengi wa Ethiopia wanatumia picha yake kujenga morali kwa mabinti kwenda vitani

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli gani huo ili nianze kuswali kwenye dini inayotumia lugha moja?
Nitasali kwenye dini ambayo inatumia lugha zote kumuabudu huyo Mungu. Ninaweza kusali hata kwa kimakua huyo Mungu akanisikia.
we jamaa stick kwenye mada hapa tunaongelea updates za vita huko ethiopia..
 
Ila ukweli ni Kwamba Labda waafrika hatujakomaa.Nchi nyingi za Ulaya mipaka yake ni ya kikabila zaidi.Nchi chache sana zina makabila zaidi ya moja na hapo utakuta ndani kuna majimbo yenye mipaka ya kikabila Mfano Switzerland yenye canton za wajerumani,Wafaransa na Waingereza.Hata Yugoslavia na Czechoslovakia ziliposambaratika nchi zilizozaliwa ilikuwa za kikabila zaidi.Tatizo Africa kabla ya ukoloni himaya zilikuwa kiasi kikubwa zipo kikabila lakini mipaka ikawekwa na wakoloni bila kuzingatia ethnicities.Tulipopata uhuru iliagizwa Kila nchi iheshimu mipaka iliyoachwa na Wakoloni.Hiki tunachokitetea sio asili yetu bali ni legacy za ukoloni.Kama dunia iliruhusu Yugoslavia kugawanyika na kuzaa nchi nyingi why not Africa?.
 
Wahutu waliwaua watusi na sio watusi waliwaua wahutu, unakijua unachoandika kweli?
Sio kweli.kuna Genocide mbili.Ya kwanza against Tusis ambapo interahamwe walitekeleza ila ya pili ambayo ilikuwa ndani ya Rwanda na Kwenye makambi ya wakimbizi Wahutu Kongo mashariki dhidi ya Wahutu iliyotekelezwa na RPF.Walivamia hadi Kongo wakidai kuwatafuta FDLR lakini walichofanya ni kuwachinja wahutu.Mpaka leo Kagame anaendelea kuwachinja kwa visingizio mbalimbali.
 
Vita iko ukingoni. Dalili zinaonesha TPLf imeshindwa vita. Wapiganaji wengi wanasalimu amri kwa Sasa. Aidha njia ya kuretreat hakuna wapiganaji wengi wamejikuta wazingirwa.

Pia makamanda wanaona ni Bora kusalimu amri kuliko kumpeleka vita Tigray. Wanaogopanmakabila mengine yataharibu na kuua watu wao vita ikipiganwa Tigray hasa katika mji Mekele.


Baadhi ya picha za wapiganaji waliojisalimisha

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Hadi akaita hivo ana uhakika 100%
 
Weka basi chanzo, hata kama ni wewe unaripoti toka uwanja wa vita 😉
 
Demographical data zinakataa kabisa hiyo hesabu ya watusi laki nane kuuliwa.
 
Safi,wanawake wa kitanzania wajifunze hapa,hii ndiyo ile asilimia 50 inayotakiwa, sio viti maalumu.
 
Mwenyekiti wa TPLF amesema kuwa,kuna sababu nyingi zilizosababisha wao kupoteza maeneo mengi.sababu izo ni -

(1)makamanda wengi wamehasi jeshi lao kwa iyo imepelekea vikosi vyao vingi kugawanyika
(2)Baada ya Abby kuja front,alikuja akiwa na wapiganaji kutoka nnje na silaha nzito

(3)kuingilia kati kwa mataifa ya nnje kwa kumsaidia bwana Abby kumpa ndege vita
(4) wapiganaji wetu wametelekeza silaha zetu nyingi kubwa kubwa kwa ofu ya mashambulizi makali kutoka kwa Abby
 
Wekeni Source bandugu. Hii ni kanuni ya uandishi kama unachukua second hand information lazima uoneshe chanzo cha taarifa yako.

Hii inaongeza credibility ya taarifa pia kutoa rejea kwa anayetaka.

Hata kama wewe ni body guard wa Abiy!
 
Kuongoza taifa la Ethiopia kazi Sana, vikundi vya kijeshi vingi mno na kuvidhibiti kazi mno!
 
Nyie mlikatazwa kuwaambia wanaume wenu wawape ndege na silaha nzito?

Visingizio vya kichapo 😄😄
 
The end justifies the means.
Ushindi ni ushindi tu. Mbona Marekani akitaka kupigana vita kwanza nakuwekea vikwazo, pili anakufungia anga lako ndege zisiruke, tatu anatafuta collabo la washirika wake, halafu mwisho inasemekana kashinda vita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…