Ethiopia: Updates on war against TPLF

Ethiopia: Updates on war against TPLF

Wapiganaji wa Serikali na Afar wakipokelewa na Wananchi baada ya ukombozi. Miji imebomolewa vibaya na Watigray TDF. Mauaji ni makubwa sana.

IMG_20211129_061533.jpg
IMG_20211129_061527.jpg
IMG_20211129_061522.jpg

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Wapiganaji wa Serikali na Afar wakipokelewa na Wananchi baada ya ukombozi. Miji imebomolewa vibaya na Watigray TDF. Mauaji ni makubwa sana.View attachment 2026710View attachment 2026711View attachment 2026712

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
Jana nimelala vizuri kabisa kwa furaha maana nilikuwa nachukia sana kuona awa jamaa wanaoleta ukabila wanaendelea tu kusonga mbele.

Hakika marafiki wa kweli hapa Duniani ni Iran,Warusi na UAE + Waturuki.msaada wenu umekuwa nguzo muhimu sana kwa Watu wa Ethiopia,naimani Wa Ethiopia watawashkuru sana.pongezi zingine ziende kwa Eritrea kwa kusaidia mpaka kutoa wanajeshi japo kuna watu waliamua mpaka kukuwekea vikwazo.

Misri tulikuwa pamoja Libya ila safari hii umeniangusha sana. ujatumia akili na busara.
 
Hii Vita Eritria wamechangia sana Ushindi. Naweza sana Bila Eritria vita ingewawia ugumu sana serikali. Pia UAE wamesaidia sana kwa anga.

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Salaam,

Kwa mahaba yangu Nitakua naweka updates za mapigano yanayoendelea huko Ethiopia Kati ya Jeshi la Serikali na Waasi wa TPLF na Jeshi lao liitwalo TDF.

Kwanza Kuna vitu vya kuweka sawa
1. Vita siyo Kati ya Ethiopia na Jimbo la Tigray. Bali ni Vita ni Kati ya Ethiopia na Chama Cha TPLF. Chama hicho ndiyo kina Jeshi lake liloitwa TDF (Tigray Defence Force). Chama hiki wafuasi wake wengi ni watu wa Jimbo la Tigray ila siyo wote. Takwimu zinataja Chama kinaungwa mkono huko Tigray kwa wasitani wa asilimia 70. Hivyo kama 30 ya Watigray hawakikubali.

Chama hiki ndiyo kiliongoza mapigano ya kumpindua Waziri mkuu wa Zamani Mangisu Haille Mariam mwaka 1991. Baada ya kufanikiwa Mtigray wa kwanza akaongoza nchi hiyo Bw Melez Zenawi.

Melez ndiye alirudisha utawala wa majimbo uliokua umetokomezwa tangu 1975 baada ya mapinduzi ya mfalme Haile Selassie.

Aidha katika utawala wa Melez ndiyo Watigray walikamata fursa zote za taifa.

Baada ya kifo cha Melez na maandamano ya Waoromo na Wahmara ulifanyika uchaguzi mkuu akashinda Bw Ali Ahmed Ali mwaka 2018.

Bw Abiy kwa kabila ni Muoromo. Abiy akaanza mikakati ya kuweka usawa jeshini na kwenye taasisi nyingi nyeti za taifa. Jambo ambalo liliwaudhi Watigray.

Chuki hii ndo imefikisha taifa katika vita.

2. Napenda niweke sawa wiano wa watu Ethiopia. Nchi hiyo inamakabila mengi zaidi ya 20 ila Makabila makubwa ni matatu. La kwanza ni Oromo 34% la pili Ahmara 27%, na la tatu ni TIGRAY 06%.

3. Historia utawala wa Ethiopia ni Kati ya Wa Ahmara na Tigray. Wa Oromo hawajajaliwa kutwaa kiti mara nyingi.

4. Wa Tigray na Ahmara ni Wahabeshi wakati Waoromo ni Wakush.

Mwisho wa UTANGULIZI.

Vita.
TPLF ni rafiki wa Magharib hasa US. Wakati Abiy ni rafiki wa nchi majirani hasa Eritria, Somali hadi UAE. Sababu ya hili ni moja, Watigray huwa ni vibaraka wa US, kusimamia maslahi ya US katika pembe ya AFRICA. Utakumbuka enzi za PM Melez Zenawi akiwa Waziri Mkuu wa Ethiopia. US walikua wanatumia Jeshi la Ethiopia kuwachapa Wasomali na Wa Eritria.

Sasa Waeritria hawataki Watigray watawale Ethiopia kwa hofu zama za Marekani kuwapiganisha zitarudi.
Marekebisho kidogo.
1: Kabila la tatu kwa ukubwa ni Somali halafu ndiyo Tigray.

2: Hili kabila la mama na mke wa Abbiy ni AMHARA sio Ahmara.

3: Abbiy alichaguliwa na bunge kama kiongozi wa mpito baada ya PM Haile Mariam Desalegn kujiuzuru kufuatia machafuko ya mauaji ya maelfu wa Oromo kabila la Abbiy. Hivyo hakuchaguliwa kwa uchaguzi mkuu.

La ziada ni kuwa japokuwa ni mahasimu wa kutupwa (Eritrea na TPLF) lakini chakustaajabisha ni kuwa Kabila kubwa Eritrea ni Tigray. Inasemekana Esayas Afwerk (Rais wa Eritrea) alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa waasi waliomuweka Zenawi madarakani lakini baadae wakahitilafiana ndiyo Afwerk akataka amegewe eneo lake na kuiasisi Eritrea.
 
Eritrea yenyewe Ina historia tofauti kidogo sababu ilitawaliwa na Italy japo briefly wakati Menelik alizuia kutwaliwa na hatimaye kura wakiwa kwa sehemu nyingine za Ethiopia.Vita dhidi ya waitalia ilipiganwa zaidi na Wa Tigray na hata majeshi ya Italia yalisambaratishwa kwa kichapo walichopata katika mji wa Adowa ambao upo jimbo la Tigray kwa sasa.Hilo na historia ya Malkia wa Sheba kuzaa na Nabii Suleiman kumewafanya Watigray kujiona watu maalum wanaostahili kuongoza wengine tu huko Ethiopia .Wanajiona ni Wateule fulani kama vile Waisrael .Ndio maana hata kama wangefanikiwa kuuteka Addis Ababa bado wangepata shida sana kutawala hiyo nchi maana hawakubaliki makabila mengine makubwa.Wangeishia udikteta tu kama wa Mengistu Haile Mariam na Meles Zenawi
 
Mchambuzi usiwe na upande..acha sisi wapenzi wasomaji tuchague nani yuko sawa...
 
Eritrea yenyewe Ina historia tofauti kidogo sababu ilitawaliwa na Italy japo briefly wakati Menelik alizuia kutwaliwa na hatimaye kura wakiwa kwa sehemu nyingine za Ethiopia.Vita dhidi ya waitalia ilipiganwa zaidi na Wa Tigray na hata majeshi ya Italia yalisambaratishwa kwa kichapo walichopata katika mji wa Adowa ambao upo jimbo la Tigray kwa sasa.Hilo na historia ya Malkia wa Sheba kuzaa na Nabii Suleiman kumewafanya Watigray kujiona watu maalum wanaostahili kuongoza wengine tu huko Ethiopia .Wanajiona ni Wateule fulani kama vile Waisrael .Ndio maana hata kama wangefanikiwa kuuteka Addis Ababa bado wangepata shida sana kutawala hiyo nchi maana hawakubaliki makabila mengine makubwa.Wangeishia udikteta tu kama wa Mengistu Haile Mariam na Meles Zenawi
Sorry ya Adwa ni tofauti sana. Ijapokua Adwa ni Tigray ila aliongoza vita na kushinda ni Menelik II. Waitaly walifanikiwa kuangusha utawala ya Watigray na mfalme wao Yohane vi alikua kaangushwa ndipo Jeshi la Menelik mfalme wa Waahmara alipkuja na Jeshi lake kufanikiwa kuwapiga Waitaly kwa pigano kubwa la Adwa.

Na kuanzia hapo ndipo Menelik akawa mfalme wa Ethiopia yote na Makabila yote.

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Tatzo kubwa apa ni kwamba ndugu mwandishi wa habari ama mchambuzi wa habari yuko bias yaani ana upande na uoande wake ni wa majeshi ya serikali iko ndo tatzo vinginevyo jamaa umejitahidi ila ukiacha kuwa mfuasi wa upande fulani basi story yako itanoga zaidi
 
Hizi Habari siyo njema kwa Zitto, zitto alikuwa anawaunga mkono wa Tigray kwenye uchambuzi wa DW
Nadhani alikurupuka.TPLF baada ya kumshinda Mengistu hakikuwa chama cha kimapinduzi tena.Ndio maana baada ya muda mfupi uasi ulianza tena kutoka kwa makabila mengine kama Oromo,Somali,Afar .Walikuwa na upendeleo wa makusudi wa kabila na eneo lao.Hata mafanikio makubwa ya kijeshi waliyopata ni kutokana na Silaha nyingi na miundombinu mingi ya kijeshi kubakia Tigray baada ya vita iliyokuwa na umwagikaji mkubwa wa damu baina ya Ethiopia na Eritrea ikizingatia Tigray ndio ilikuwa battlefront kwa upande wa Ethiopia.TPLF ilianzisha vita kwa kuwaua au kuwateka askari wa serikali ya muungano waliokuwa Tigray na kuchukua silaha zote za kimkakati na kuzitumia dhidi ya Jeshi la Serikali.Walikimbia mji wa Mekele kimkakati kwenda Milimani ambako inadaiwa ni ngumu sana kuwaondoa kutokana na jiografia yake.Hata sasa nadhani endapo watashindwa bado wataenda huko kujichimbia na kujipanga upya.Wao lengo ni Uhuru wa Tigray wala sio kuitawala Ethiopia yote kwa sasa wakati Abiy anataka Ethiopia japo ya shirikisho iliyo moja.
 
Eritrea yenyewe Ina historia tofauti kidogo sababu ilitawaliwa na Italy japo briefly wakati Menelik alizuia kutwaliwa na hatimaye kura wakiwa kwa sehemu nyingine za Ethiopia.Vita dhidi ya waitalia ilipiganwa zaidi na Wa Tigray na hata majeshi ya Italia yalisambaratishwa kwa kichapo walichopata katika mji wa Adowa ambao upo jimbo la Tigray kwa sasa.Hilo na historia ya Malkia wa Sheba kuzaa na Nabii Suleiman kumewafanya Watigray kujiona watu maalum wanaostahili kuongoza wengine tu huko Ethiopia .Wanajiona ni Wateule fulani kama vile Waisrael .Ndio maana hata kama wangefanikiwa kuuteka Addis Ababa bado wangepata shida sana kutawala hiyo nchi maana hawakubaliki makabila mengine makubwa.Wangeishia udikteta tu kama wa Mengistu Haile Mariam na Meles Zenawi
Ahaa nimeanza kuwaelewa sasa watigray inamaana wanatabia kama za watusi walivyo.
 
Back
Top Bottom