Ethiopia: Updates on war against TPLF

Mkuu unaonekana ni mkabila sana , hatuezi ongoza nchi kwa misingi ya ukabila , kwann upaone maeneo ya waoromo ni muhimu kuliko kwa wa amhara au tigray ?
 
Mkuu unaonekana ni mkabila sana , hatuezi ongoza nchi kwa misingi ya ukabila , kwann upaone maeneo ya waoromo ni muhimu kuliko kwa wa amhara au tigray ?
Mkuu mimi sio mkabila hata kidogo, lakini unapozungumzia Ethiopia basi jua kuwa unazungumzia ukabila. Yaani ukabila Ethiopia ndiyo kila kitu. Hupati huduma nzuri ila ni kabila lako kwanza ndiyo litakaloamua na ninaongea hivyo kwa kuyaona sio kuhadithiwa. Nimeishi ethiopia kwa miaka mitatu. Yaani si maofisini wala mitaani ni ukabila tu, hadi maeneo ya kuishi kwenye miji mikubwa kama Addis na Hawasa watu wanaishi kimakabila tu.

Yaani ni vigumu kupata picha halisi ukiichukulia Ethiopia kuifananisha na muingiliano wa kimakabila kama Tz
 
Lakini hata Tanzania ilikuwa ya kikabila until someone rolled the sleeves and decided to do something. Don't you think Ethiopia need someone to do something about it? Au ndio inabidi iwe fate yao, unavyoona wewe? Just askin'
 
Ahsante sana huu ndio ukweli nashangaa kuna watu huwa wanawaunga mkono hawa wa Tigray bila kujuwa kuwa wametawala nchi kwa miaka mingi na hawataki wengine watawale pamoja na uchache wao wanadhani nchi ni kwao na kutawala haki yao. waziri mkuu kutaka kuleta usawa ikawa nongwa kwao maana mpaka jeshini wao walishika kila kitu. Kuna mtu kama Zitto Kabwe anawaunga hawa waasi hakuna nchi inaweza kuvumilia waasi hata hao USA vita walipigana vya ndani sababu kuna watu walitaka kujitenga na Ethiopia wana haki ya kuwapiga watu wanaotaka kujitenga.
 
Lakini hata Tanzania ilikuwa ya kikabila until someone rolled the sleeves and decided to do something. Don't you think Ethiopia need someone to do something about it? Au ndio inabidi iwe fate yao, unavyoona wewe? Just askin'

Lakini hata Tanzania ilikuwa ya kikabila until someone rolled the sleeves and decided to do something. Don't you think Ethiopia need someone to do something about it? Au ndio inabidi iwe fate yao, unavyoona wewe? Just askin'
Naiombea kilasiku Ethiopia iachane na huu mfumo wake wa ukabila na umajimbo watoke kwenye federal state kwenda kwenye united republic. Lakini kwasasa huenda ikawa too late au ikahitaji miaka kadhaa kui-implement yaani hiki kizazi ki-phase out then the coming generation iachane na ukabila. Kwasasa ni ngumu sana maana miongoni mwa waethiopia kuna wenye dhana ya kudhulumiwa na kuna wenye kujiona wapo superior yaani first class citizens. Hapo ni vigumu sana kuwafanya wawe wamoja watu wa muundo huu.

Wanachoweza kufanya ni serikali ijitahidi kuea fair kwa jamii zote ili kuweka usawa. Abbiy aliharibu hivyo mwanzoni lakini kuwaondoa watigray waliojazana serikalini wakahisi wanahujumiwa na ndiyo wakaifikisha ethiopia hapo walipo sasa.
 
Sasa ili kutokomeza ukabila hupaswi na ww kuvaa uhusika wao bali jikite kwenye uhalisia sio kumlaumu Abey kwa kumfunga mtu anaetaka kuleta ukabila
 
Watigray hawajaipeleka sehem yyte Ethiopia zaid ya kuwa chanzo cha ukabila kurudi tena Ethiopia
 
Update.

Mapigano yamekoma majimbo ya Afar na Amhara. Yanaendelea majimbo ya Oromia na Tigray hasa Magharibi.

Hivyo Waasi wa TPLF wamepoteza Nusu ya maeneo yao kwa siku kumi za mapigano sasa

Kwa Kasi hii kufika tarehe 15 December vita Baki yankuviziana hasa maeneo ya Tigray ila miji yote itakua kichibya Jeshi la Serikali

PM Abiy anawajibu mmoja mkubwa sana wa kuhakikisha wapiganaji wa Afar na Amhara hawalipizi kisasi.

Maana inaonekana wa Tigray wamefanya maauji makubwa Afar na Amhara.

Sent from my Lenovo L38111 using JamiiForums mobile app
 
Endelea na maombi, ipo siku mambo yatabadilika. Ila United Republic haitawezekana. Kwa maoni yangu naona Pure federalism ndio itawafaa, ikiyapa majimbo uhuru fulani limited kwa mambo yao ya ndani. Hii itawezesha Watu kuhamia majimbo ambayo yanaendeshwa vyema na kuongeza muingiliano. Katiba ilinde tu uhuru na fairness kwenye majimbo kusiwe na kubaguana. Kubagua iwe serious criminal offense.

United republic itasumbua kama Zenji na Tanganyika zinavyosumbua mpaka leo!

Wanachoweza kufanya ni serikali ijitahidi kuea fair kwa jamii zote ili kuweka usawa. Abbiy aliharibu hivyo mwanzoni lakini kuwaondoa watigray waliojazana serikalini wakahisi wanahujumiwa na ndiyo wakaifikisha ethiopia hapo walipo sasa.
Sidhani kama aliharibu. Ilikuwa ni sahihi kuelekea Ethiopia ambayo huwa unaiombea. Ilikuwa ni an unavoidable pain. Else angekuwa kinyago chao pale Abeba. Nadhani akishinda hii vita itampa leverage ya kutengeneza Ethiopia tofauti walau na aliyoikuta. Ila itategemeana kama atashinda na hatua atakazofuata baada ya hapo.

Kutawala nchi kama Ethiopia sio kazi rahisi. Naona wengi wanaandika as if Ethiopia ni Bongo!
 
Unataka kutuambia tiba ya ukabila ni kuunga mkono ukabila!?
Ndio tuseme Watusi walikuwa sahihi kuwauwa wahutu kisa tu wao ni waumini wa ukabila?
 
Ahsante kwa taarifa.
Tafadhali weka chanzo cha taarifa kama haupo Tigray!

Joke. Zamani JF kutoa habari ilikuwa lazima uweke source!
 
Pia ukiacha Somali region,wengi wao ni Waislam
 
Federalism yenye mfumo wa kikabila mara nyingi ni shida sana Afrika haswa kuhusiana na tofauti za ki tamaduni,raslimali na kadhalika.Angalia Nigeri(Biafra),Cameroun(English Speaking region),Senegal,Angola etc.Kunahitajika ukomavu sana kuweza kufanikiwa under federalism.
 
Watigray hawajaipeleka sehem yyte Ethiopia zaid ya kuwa chanzo cha ukabila kurudi tena Ethiopia
Hujanielewa mkuu! Kusema kuifikisha ethiopia ilipofikia sasa nilimaanisha hii vita inayoendelea sasa hivi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…