carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Zaidi ya watu 60 wameuawa katika mfululizo wa mashambulizi dhidi ya Wakristo katika Mkoa wa Oromia nchini Ethiopia, kwa mujibu wa Kanisa la Orthodox la nchi hiyo.
Mkazi mmoja aliyempoteza baba yake mwenye umri wa miaka 75 alisema washambuliaji waliwazunguka kutoka pande zote nne bila wao kuwa na taarifa ya awali. Mashambulizi hayo yanaripotiwa kuathiri maeneo matatu katika Wilaya ya Shirka, huku nyumba 20 zikichomwa moto na watoto watano wakiwa miongoni mwa waliouawa.
Kanisa la Orthodox limelaani mashambulizi hayo, likiyataja kuwa mauaji ya kinyama na kusema vitendo hivyo vinadhoofisha misingi ya kuheshimiana na kuishi kwa amani nchini humo. Pia limedai kuwa limekuwa likizifikisha kwa mamlaka malalamiko kuhusu ukosefu wa usalama bila kupata suluhisho.
Kwa upande wake, kiongozi mmoja wa eneo hilo amelituhumu muungano mpya wa waasi unaojulikana kama Alliance for Survival, unaojumuisha Jeshi la Ukombozi wa Oromo (OLA), kuhusika na mashambulizi hayo. Hata hivyo, OLA haijatoa maoni kuhusu tukio hilo na imekanusha kuhusika na mashambulizi kama hayo yaliyotokea awali.
Ripoti ya Baraza la Haki za Binadamu la Ethiopia iliyotolewa Julai 2026 ilieleza kuwa watu 458 wameuawa katika mashambulizi katika eneo hilo ndani ya miaka minne iliyopita.
Chanzo : BBC News