Watanzania bado tina fikra za ujamaa na kila wakati tunahisi muwekezaji ni mwizi.
Kama sio Samia kuwa bold, uwekezaji bandarini usingefanyika. Bado Bagamoyo, kidogo watu watoane roho kwa ten pasent, msukuma kachukua hela kaenda kujenga bandari Nyamirembe,Chato, na hakuna meli iliyowahi kufika tangu bandari iishe.
Morogoro ilitajwa kama moja ya mikoa inayoweza kulisha taifa, who cares kuja na mkakati maalum?
Karafuu inalimika baadhi ya mikoa ya nchi yetu huku bara, walio serious ni zanzibar tu!
Parachichi biashara kubwa sana, lakini huoni commitment ya serikali hata kuweka miundombinu ya maghala yenye mafriji maalum ya kuyatunza.
Tanga wana machungwa na machenza, who cares?
Kagera, Mbeya, Kilomanjaro wana ndizi, who cares to make the business go international?
Zabibu Dodoma? Mahindi tele Katavi na Rukwa