Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Sikubaliani na kauli zako. Hii ni nchi ya kidemokrasia, udikteta wa Magufuli ulikuwa hauna nafasi na ndiyo maana alikufa mapema kwa uwongo aliokuwa anawalisha, kuwapeleka rumande wale aliokuwa hawapendi, kunyang'anya fedha za wafanya biashara na kuua wakosoaji.JPM hakuwa perfect, lakini amefanya mambo mengi ya msingi kulisaidia taifa, vitu ambavyo watu walifikiri haviwezekana. Angalia nchi ilipokuwa 2015.
Alifanya vitu kama :-Umeme wa uhakika, maji, tunapata share yetu kwenye madini, Elimu bure, kukamilisha Terminal three, vituo vya afya nchi nzima, SGR, Bwala la Nyerere, barabara ya Kimara, barabara nchi nzima. Nidhamu serikalini, kupunguza ukiritimba rushwa, upigaji wa miradi,Madaraja nchi nzima, ukarabati wa meli na kununua meli mpya katika maziwa mbalimbali.
Alijaribu kuhimiza uchapakazi, kukemea rushwa, wizi, ufisadi, udini. Mafisadi wengi aliwabana ila ni kweli hakuwamaliza wote.
Alijaribu kuhimiza nchi kuwa na mentality na attitude ya kujitegemea badala ya kuombaomba. Aliwahimiza Watanzania wajiamini na kutembea kifua mbele. Aliweka misingi thabiti ili kujenga nchi imara.
Kama alikuwa anataka kututawalq KIDIKTETA basi alipaswa awe amepindua nchi kama akina Kagame na Museveni, lakini yeye alikuja kwa sanduku la kura.
Huwezi kuja kwa sanduku la kura halafu ukataka kutawala KIDIKTETA NO, lazima na wewe ufe