tindikalikali
JF-Expert Member
- Jan 14, 2011
- 4,854
- 1,129
Nilipomfata mwanzo hakutaka hata kunisikiliza, nilipozid kumfatilia akanambia "sikupendi", "nina mpenzi wangu na ninampenda sana",, niliukubali ukweli na kuamua kukaa pembeni, siku, miez hatimaye miaka kama mi3 ikapita, hapo ndipo akaanzisha ukaribu tena na mimi, akawa haishi kupiga simu na kuandika text, akajitahidi akaonana na mimi, safari hii "sikupendi" ikawa "nakupenda", huku akiwa na lundo la matumaini. Sikumficha, nilimweleza kwamba sina muda naye tena, na nilishamtoa akilini siku nyingi. Alilia sana siku hiyo na kulalamika kwanini namfanyia hivyo, alinibembeleza lakin hakufua dafu, ikabidi akubali kile nilichomuambia. Sasa anachowaambia rafiki zangu ni kwamba mimi nitakuwa wake tu! Sijajua huu ujasiri anakoupata, wakati mimi sina mpango naye hata kidogo