Sijaoa na sina mke wala mpenzi ila nimeshajisemea Mahari ya mwanamke nitakayotoa si chini ya 3m.
Wakitaja 11m nitatoa 3m wakitaja 20m nitatoa 3m wakijichanganya waseme mahari 3m basi nitakua muoaji wa kwanza Kumaliza mahari.
Ki ufupi mahari nmepanga ni 3m tu yani hiyo ipo mfuko wa shati kwa mwanamke yeyote nitakae piga hodi kwao.
Sio zaidi ya hapo wala chini ya hapo. Kwahyo Mkuu wewe 1.5m unaiona Kubwa sikulaumu yawezekana level yako hujafikia huko na naamini pia Hata muda wako wa kuoa haujafika.
MUDA ukifika naamini utapandisha dau mwenyewe hata bila kuambiwa kutokana na maana ya mahari kwa definition utayokua nayo kichwani.
Kwasasa baki tu level za dem wangu,baby wangu,manzi angu,pisi yangu level ya Mke Wangu Bado hujaifikia Boss.