Eti asijue................How??

MwanajamiiOne

Platinum Member
Joined
Jul 24, 2008
Posts
10,470
Reaction score
6,580
Wanajamii
Natumaini wote wazima.........................

Ni mara nyingi nimekuwa nikisikie kuwa ..Kama unataka mwanaume/mwanamke wako kimapenzi asikuchoke basi usimwonyeshe kuwa kwake umefika............yaani hata kama unampenda sana basi unatakiwa usionyeshe!!!

How do people do that?? Mapenzi si wanasema ni kikohozi, hayajifichi?? sasa hapa inakuwaje au inakuwagaje?
 
mh mh! Dearest MJ1 kwanza nikusalimu........pili hivi mapenzi yanafichika kweli?lkn nahs inawezekana kukontrol lol!nimekuwa nikiskia sana hii kitu lkn cjui kama ina uhalisia! Wacha nione wengine watasemaje.....
 
Sidhani kama inawezekana ikiwa mtu amependa kwa moyo....yanayokontroliwa ni yale yanayotumia akili zaidi!

Besides ni ubinafsi kuacha kumjali na kumpenda mwenzako ipasavyo kisa hutaki ajue kwake umefika!
 
Hicho ndo wengi wanajidanganya, too much kushindana katika mapenzi...
Nyie kama mnapendana kweli na kila mmoja kumpenda mwenzi wake ipasavyo
naamini inatosha... kinacho fanya watu wachokane katika mapenzi ni failure katika
tendo la sex... na sex si tu lile tendo ni attitude yenu towards sex na jinsi gani
mnaichukulia priority...

Pamoja na kusema sex si pekee... naamimi if you really love a person you do
anything for her/him... sasa kama hio sector ya loving each other mumemudu
inayobaki ni SEX...
 
Sasa usipomuonyesha kuwa kwake umefika si atadhania kweli hujafika. Mantiki zingine bana….taabu kweli kweli.

Na akishadhania kuwa kwake hujafika na akatafuta mwingine utafanya nini? Utamlaumu? Utambembeleza na kumwambia umefika?
 
nafikiri waga wanamaanisha usimuonyesha mtu uko desperate sana,kwamba kama ye hayupo basi na maisha nayo basi....mpende,mheshimu,mtunze,mshauri lakini kamwe usimfanya binadamu mwenzio kuwa kama mbadala wa maisha yako.....binadamu hubweteka na kujisahau wakati mwingine na kuona wao ndo kila kitu,as in kama wao hawapo basi tena....lakini hiyo sentensi haina maana unampenda mtu umuonyeshe unamchukia...la hasha,kuwepo na kiasi,na reasoning kwenye decision....nenda kwa akili na moyo wako pia,kuwe na kiasi!!
 
yap..hii idea ipo hasa ktk yale mapenzi ya kuzuga! Lakini mara nyingi huwa haifanyi kazi coz mwisho wa siku utajionesha tu! Hili wazo limekuja kutokana na kuwa na mahusiano yasiyo na uhakika!
 
Sasa usipomuonyesha kuwa kwake umefika si atadhania kweli hujafika. Mantiki zingine bana….taabu kweli kweli.

Na akishadhania kuwa kwake hujafika na akatafuta mwingine utafanya nini? Utamlaumu? Utambembeleza na kumwambia umefika?

Unamwambia nimefika tafadhali badili mawazo...muda huo nae anakua kafika kwingine na kafikiwa basi inakula kwako!!!
 
in an intimate relationship the power lies whith who cares less. unampenda,be kind,play ur part.bt signs of desperation nadhani zinamfanya mwenza akimbie.nadhani nimeona hii,unapompenda mwanaume hadi unaskia kama unapata kichaa,anaanza kuleta maringo.when u almost give up,ana-notice na kuanza kukufukuzia tena.i guess chilling out and take life as it is ndo unaambiwa usimuoneshe.dont go over the roof over petty stuff.what am i saying again,sorry im half asleep,lol!
 
Unamwambia nimefika tafadhali badili mawazo...muda huo nae anakua kafika kwingine na kafikiwa basi inakula kwako!!!

Lizzy Licious,

Hapo kweli inakuwa imekula kwako mazima bila kubakisha.
 
Inategemea, kwa wengine inafanya kazi na kuna wengine haifanyi kazi. Kutaka kujua kwako inafanya kazi wewe binafsi unatakiwa uweze kumchunguza mpenzi wako na kufuata kile ambacho kitasaidia kudumisha penzi lenu.

Na kuna wale ambao hawawezi kujizuia kuonesha mapenzi yao na ukweli ni kwamba hakuna sababu ya kujizuia; lakini pia unaweza kumpata mtu ambae akachukulia advantage (wako wenye tabia hii) kwa wewe kuonesha mapenzi yako na kuanzakukufanyia vituko kwa vile anaamini kwamba umefika kwake.
 
Hivi wifi ni mambo gani haswa yanaonyesha mtu yuko desperate?!Amka unawe uso kisha unijibu tafadhali....Binafsi nashindwa kutambua maana hata sijali wala sioni tatizo mtu akinipenda kama vile nimebaki duniani mwanamke mwenyewe....ila malalamiko ndo huwa siwezi kuvumilia!!
 
Lizzy Licious,

Hapo kweli inakuwa imekula kwako mazima bila kubakisha.
Nyaniizzo nafurahi kuona unajua kwamba ukimpenda mtu unatakiwa umwache ajue kwamba umempenda haswa usije ukaibiwa na wataalamu wa kujali na kubembeleza!!
 
Nyaniizzo nafurahi kuona unajua kwamba ukimpenda mtu unatakiwa umwache ajue kwamba umempenda haswa usije ukaibiwa na wataalamu wa kujali na kubembeleza!!

Lol @ Nyaniizzo.....

N to the Izzo....I to Izze
Foshizzle ma nizzle I used to dribble down in GA

N to the Izzo....I to the Izee
Fo' sheezy my neezy keep my arms so freezy

Haaaaaaa ningechana mistari hapa sema staki tu kumharibia sisteri Mj1
 

Mistari yenyewe ina
kwashakoo!!Lolzzzz!!

Backt to topic..MJ mpenzi kwenye mapenzi ya kweli hamna haja ya kuogopa kuonyesha mapenzi yako kwa mwenzio yako deep kiasi gani...ila haya ya kiusanii yaliyosambaa siku hizi inabidi maana mtu akiona/gundua unampenda sana anaona kama utajamganda na kumng‘ang‘ania siku akikwambia bye bye .
 
hivi mmeiona avata ya joelincoln sawasawa au mnajadili tu mambo ya kusadikika hapa?
 


yes, kwa namna fulani nakubaliana na wazo lako lakini,
sio mara zote wazo lako hili linaweza kuwa la kweli?

wakati mwingine kwenye mapenzi watu wanapenda kuweka reserve
ya mapenzi yao kwa kutarajia kuwa huko mbeleni kama mambo yanaweza kubadilika,
na ikafikia mpaka kuachana basi asiumie sana,
lakini kama waungwana wanavyosema, penzi ni kikohozi,
kulificha asilani huliwezi,
mi nadhani ni kujifaragua tu na wala haina uhalisia wowote!!!!!!
Hizi huwa ni kauli za kujitengenezea mazingira ya kujilinda tu hapo mbeleni,
pindi mambo yanapoenda kombo!
 
mh mh! Dearest MJ1 kwanza nikusalimu........pili hivi mapenzi yanafichika kweli?lkn nahs inawezekana kukontrol lol!nimekuwa nikiskia sana hii kitu lkn cjui kama ina uhalisia! Wacha nione wengine watasemaje.....

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, WL mydia am fyne darling hope uko poa. Nimekumisije?

Yaani hii kitu iko serious mydia more than we think................kina kaka wanadai kuwa ili mwanamke asikusumbue mwonyeshe mapenzi 'nusu' loh sijui ndo aje eti wanadai mwanamke akijua 'kwake hupindui' i.e. unampenda sana atakusumbua ....na sie kina dada huwa tunaamini kuwa mwanaume akijua kwake 'umefika' utabana ngenge......sasa sijui ni aje hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…