Yamenikuta! Naambiwa fimbo yangu iko mbali nikubali yaishe!
Matatizo ya maisha yametufanya mimi na mke wangu tukubali ushauri wa rafiki yangu wa kumruhusu mke wangu akatafute kibaruwa umangani. Rafiki yangu huyo yuko huko kwa kitambo akiwa dereva wa magari makubwa na huja nyumbani kila baada ya miaka miwili.
Anapokuja pesa hujionyesha hivyo alipotushauri tulikubaliana na mama watoto aende akatafute kibaruwa huko kama mtumishi wa nyumbani.
Mama watoto alienda huko akiniwachia ulezi tukitegemea mabadiliko ya maisha. Miezi michache mke wangu akituma pesa kidogo zilizosaidia maisha huku. Mara mambo yalibadilika, mama watoto aliniletea habari kuwa sasa yuko kwenye mateso na hata mshahara wake halipwi. Tatizo ni kuwa mama mwenye nyumba amebaini kuwa baba mwenye nyumba anapiga malaini kwa mke wangu, hivyo kaamuwa kumuonyesha na Baba mwenye nyumba nae baada ya kuvumilia muda mrefu na msimamo wa mke wangu wa kumtolea nje nae kaamuwa atumie mateso na vitisho ili apate mradi wake.
Niliwasiliana na yule rafiki yangu alietushawishi juu ya hali hii nae akashauri mke wangu akimbie kwa mwajiri wake nae atamficha ndani ya gari lake ili kumvusha sehemu alioko ili afike kwenye mji wenye ubalozi wetu. Mke wangu amefanya hivyo na baada ya siku moja tangu atoroke amenitumia ujumbe huu wa simu;
' Tumeshapoteza siku nzima tukiwa njiani na imefika usiku rafiki yako amekodi chumba lakini anachoniambia mimi sikielewi. Ananitaka kimapenzi na nilipomkumbusha kuwa wewe ni rafiki yake alinijibu kuwa fimbo ya mbali haiuwi nyoka!
Amenikumbusha tu kuwa mimi sina ninapopajuwa na ni mkimbizi. Sijui kama ni kweli lakini amenambia kuwa nikikamatwa na maaskari basi watanifanyia vibaya kwanza kabla ya kunipeleka gerezani. Hadi sasa nimejaribu kukutunzia heshima yako na kwa vile hili la kuja huku tuliliamuwa pamoja naomba ushauri wako lipi la kulifanya?'
Baada ya kuisoma msg hiyo nimechanganhikiwa. Wenzangu nakuombeni ushauri nini cha kufanya katika tatizo hili?