Eti ghetto kwako umeweka sheria gani kwa wageni wako?

Eti ghetto kwako umeweka sheria gani kwa wageni wako?

Katika miezi hii na tunakoelekea naona , minyuzi ya wagombea na wagombaniwa imeshika hatamu kila pembe ni uchaguzi na wachaguliwa ila sio dhambi tukijipa break kidogo.

Maisha yana mambo mengi sana ya kuyajadili.

Leo naomba tujadilia hili hasa kwa wale waliopanga kama mimi.

Eti ghetto kwako umeweka sheria gani kwa wageni na washkaji zako?
Getho kwangu kuna pea kadhaa za mabuti ya kupigia mafala mitama, ukiingia uruhusiwi kuyagusa hata kwa bahati mbaya.
 
Mgeni karibu gheto, viatu usivue hata kama ni mpoto.../

Sipendi ubosi, na ndio maana geto sijaweka kochi.../

Usijilete ukiwa soft, ukiweka channel za sultan mi nanyang'anya remote.../

Si unajua hili Gheto la muhuni, basi ukisikia muasho kausha hao ni kunguni.../

Kama unataka kuoga nenda bafuni, kumbuka sina demu kwaiyo usimalize sabuni.../
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Sio la kishua, ila mademu wa masaki nadhani wanalijua.../

Limetamba sana huko insta, ma modo wengi wamepigia nalo picha.../

Hizi ndio Ilani za geto kwa mgeni, kama ni demu ingia chumbani usikae subuleni.../

Wali wa jana mwiko kuita kiporo, ukija asubuhi utanikuta nje naanika godoro.../

Ratiba ya usafi wa ndani ni moja tu kwa wiki, kama mashuka siku niliyofua hata sikumbuki.../

Jiji la mabaharia linakosaje bahari, na ndio maana geto sina kitasa natumia komeo ya msumari.../

Karibu geto jiskie uko kwenu bibie, unatumia kinywaji gani nipe hela nikakununulie.../

Si unajua sijapata deal tangu magu aingie, umeoga ila gheto sina losheni vipi nikupe korie?.../
 
Back
Top Bottom