Eti Hakuna Anayejali kama Simba ni Bingwa wa Mapinduzi!

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Posts
1,544
Reaction score
943
Mwandishi Mohamed Kuyunga wa gazeti la Michezo la Mwanaspoti la leo tarehe 16 Januari 2015 anadai 'eti pamoja na kuibuka kidedea na ubingwa wa kombe la Mapinduzi, Simba yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi bado ina kazi kubwa ya kufanya ili kuweza kuwapa imani mashabiki wake kutokana na kuboronga kwake katika michezo iliyopita ya ligi. Kwa mtazamo wa kila mshabiki wa Simba na wanamichezo wote kwa ujumla hii ni kweli tupu na hata kocha wa Simba Goran Kapunovic ameweka wazi tamaa yake kuona timu inahamishia makali ktk ligi ambako kunatarajiwa kuwa na upinzani mkali zaidi.

Lakini pamoja na kuandika tahadhari hii, ukisoma makala yake huhitaji kuwa mchambuzi uliyobobea kung'amua kuwa hoja zake zimekaa kishabiki na kinazi zaidi kitu mabacho sio sawa kwa mwandishi wa aina yake anayepaswa kuchambua kitu objectively.

Ukianza na kichwa cha makala yake kinajieleza wazi pale mwandishi huyu anaposema 'Hakuna Anayejali kama Simba Ni Bingwa wa Mapinduzi' ambapo kwa mtazamo wangu amekusudia kubeza waziwazi ubingwa wa Simba katika kombe la Mapinduzi. Ni vigumu kuamini kama ingekuwa ni timu nyingine imeshinda kombe hili kama angeweza kupata ''guts' za kuandika kichwa cha namna hii. Hapa mwandishi kwa kujua au kutokujua anaonekana kuwa alikuwa na mabingwa wake wateule kichwani ambapo Simba haikuwa mojawapo. Hili si kosa, lakini kubeza mafanikio ya timu kwa kuwa tu hukuitarajia hakukupi sababu ya kubeza ushindi huu. Hata hivyo kusema 'hakuna anayejali...' amekosea sana. Huu ni ushabiki wake tu kwa kuwa mashabiki wapenzi wa Simba wanajali ndio maana walikesha wakifurahia ushindi.Wachezaji pamoja na benchi la ufundi wote wanajali kiasi cha kudai kuwa ushindi umewapa morali ya kupambana katika michezo ya Ligi. Huyu anayesema hakuna anayejali ni nani?

Ndani ya mada ndio kuna hoja za kishabiki zaidi ambazo ni aibu kwa mwandishi kuonyesha mwelekeo wako wa chuki waziwazi wakati unafanya kazi ya umma. Mwandishi Kuyunga kuna sehemu anasema ''ushindi wa Simba katika kombe la mapinduzi si wa kujivunia sana kwani haikuweza kukutana na timu nyingi zinazocheza Ligi Kuu Bara kama vile Azam, Yanga na KCCA ya Uganda ambazo zingekuwa kipimo tosha kwa kikosi chao.'' Hoja hii inaficha kilichomo katika akili ya kinazi ya mwandishi kuwa Simba haina cha kujisifu sana kwa kuwa imekutana na timu za Zanzibar, kwa maana kama ingekutana na timu nyingine isingeshinda! Huu si uanamichezo. Mwandishi anasahau kuwa timu hizi anazozitaja zilikuwa zimeshatolewa katika hatua za Robo fainali na Nusu Fainali na kwamba Simba ililazimika kuzifunga timu zilizozishinda timu anazojua yeye ni bora kama vile POLISI waliokuwa wababe wa KCCA, JKU waliokuwa wababe wa YANGA na MTIBWA waliokuwa wababe wa AZAM. Mantiki inakataa kuwa Mtibwa, Polisi na JKU zilibahatisha zote kufuzu nusu fainali na fainali yenyewe. Come on mwandishi give credit where it deserves hasa ukizingatia kuwa Mtibwa ndio kiongozi wa Ligi ya Bara, mwandishi unataka ukumbushwe hilo kuwa hakuna timu bora Tanzania Bara kwa sasa zaidi ya Mtibwa kama unazungumzia kiufundi na kimantiki?

Hoja kwamba safu ya ushambuliaji ya Simba ni butu kwa kushindwa kupachika mabao ya kutosha nayo imekaa kishabiki zaidi hasa ukizingatia kuwa ni Yanga pekee ndio timu iliyofunga magoli mengi zaidi kuliko Simba! Tofauti pia ni goli 1 pekee! Hapa kuna mambo mawili ambayo ni ama timu nyingi zilijaandaa kiasi cha kufanya mashindano kuwa makali, au, timu zote ikiwemo hizo Yanga, Azam na KCCA zilikuwa na safu mbovu za ushambuliaji! Wakati anajadili hili mwandishi angepaswa kuzingatia kuwa kundi alilotokea Simba lilikuwa 'gumu' zaidi kuliko makundi mengine ambako timu zilikuwa zinapigwa magoli anayoyaita ya kutosha. Ikumbukwe kundi la Simba liliingiza timu 3 nusu fainali labda kwa faida ya mwandishi, timu zilizotoka kundi la Simba hazijafungwa na timu yoyote kutoka kundi tofauti na la Simba katika mashindano haya. Kwa mantiki hii mwandishi angejenga hoja kuwa timu zote zilizoshoriki katika mashindano haya hazikuwa ktk ubra wao angeeleweka kuliko kudai kuwa timu zilitolewa mapema zilikuwa bora kuliko zilizofika nusu fainali na fainali! Mwandishi anaweza kutoa ushihidi upi ukakubalika katika hili zaidi ya ushabiki?

Hoja kuwa safu ya ulinzi ya Simba bado haijathibitisha uimara wake na yenyewe ni ya kishabiki zaidi kwa kuwa Simba ingefanya nini kuthibitisha hili? Kuruhusu bao 1 pekee ktk mechi 6 ni ushahidi ambao haujavunjwa na timu yoyote ktk michezo hii. Mtibwa, Yanga na Azam zote zimeruhusu idadi hii au zaidi so huwezi ukatofautisha beki hzi zinazoonekana kuwa bora na ile ya Simba.

Mwisho ningeweza kuendelea zaidi na zaidi kuelezea 'ushabiki' wa waziwazi wa mwandishi lakini bora niishie hapa. Niseme tu sitaki kuaminisha jamii kuwa Simba iko kamili kabisa lakini si vizuri pia kubeza mafanikio yao hata kama ni kidogo kwa hadhi ya Simba. Ni jambo baya mwandishi kuchukua hoja za mashabiki mtaani kisha unakuja kujaza gazeti bila kufanya due diligence ya kutosha. Uchambuzi unaofaa ni ule unaoelezea ubora na ubovu wa timu fairly bila mwelekeo wa chuki au husuda.

Ni vizuri waandishi wetu kujua kuwa manpoandika maandishi yenu yanasomwa na wengi, na wengine wetu tunapenda sana mtu afanye critique iliyojaa hoja, mifano, takwimu na facts nyinginezo na sio criticism ya kishabiki kwa kujenga hoja zilezile ambazo Yanga Azam au Mtibwa wanahukumiwa nazo lakini zinatumika kubeza timu moja pekee? Ni nini hiki zaidi ya ushabiki?
 
Hongera Baba Kiki kwa uchambuzi safi.. Huyo mwandishi ni kanjanja.
 
Last edited by a moderator:

Uchambuzi wako ni mzuri sana. Nakushauri uupeleke kwa gazeti hilo hilo ili kurudisha hadhi ya Simba na kombe lake la mapinduzi iliyovurugwa.
 
Simba wenyewe tunajali ndio maana uongozi umewapa pesa zote za ushindi wa kwanza wachezaji wagawane. Kanjanja huyu hana haki ya kutuambia sisi ushindi huo sio wa kujali. Wangeshinda hao anaowataka tusingesikia kauli hizo. Ni maoni ya poor losers wanazotumia kujifariji.
 
mmeambiwa ukweli mnaanza kuzonza mikia bwana kwahiyo mmeridhika na nafasi mliyopo kwenye msimamo wa ligi kuu bara
 
wivu ni kidonda wanaoshiriki waugue pole...
 
mmeambiwa ukweli mnaanza kuzonza mikia bwana kwahiyo mmeridhika na nafasi mliyopo kwenye msimamo wa ligi kuu bara

Watu wengine bwana. Nani kakuambia tumeridhika na nafasi tuliyopo? Tungeridhika Phiri angekuwa bado kocha wetu. Fikra zako kama za kocha wa Taifa Stars kumchagua Msuva kwenye timu ya maboresho wakati kwa sasa hakuna winga wa kiwango chake Tanzania.
 
Tunajibishana na Yanga tu.Wauza sembe hawa deserve attention yetu. Mtani wetu Dar Young Africans wengine kwetu ni kama Arusha Meat au Mbagala Rangers. Sasa wewe upo wapi? Tukufahamu.
 
Hoja zako zina mantiki Mkuu,nafikiri asiyekuelewa atakuwa na MTINDIO WA UBONGO bila kujali anashabikia timu gani.

Mkuu, hili sulala uliloliwasilisha ndilo linaloua kwa kiasi kikubwa SOKA la nchi yetu. Waandishi wetu wengi wa habari za michezo ni washabiki zaidi wa hizi timu na hawaandiki habari zao kiutaalaam,husukumwa zaidi na ushabiki na ndio maana unakuta hizi timu kubwa hasa za SIMBA na YANGA magazeti huzipamba sana lakini kiuhalisia hazina uwezo huo wanaousema. Na ndio maana ktk mashindano ya Afrika ngazi za vilabu wakikutana na timu za ukweli hazifanyi lolote lile la msingi
 
nikupongeze kwa kuona na ugonjwa wa JICHO LA TATU ambao mim pia naumwa.
kwanza hatustahl kuldharau kombe la mapnduz ndio kombe lenye mvuto zenj.
Simba pamoja na kushnda kombe la mapnduz kuna ya kufanya.
washambuliaj wa simba si wabovu sema bado hawjawa na chemstry nzur.
kama mwanzon DANY serunkuma alikuwa anasmama kat sana lakn dany ili apafomu kwa mfumo wa SIMBA.Inapasa acheze kama 10 lie.awe anashambulia pande zote mbl kwan ana uwezo wa kuptsha mipra pemben ya box.
Pia simon serunkuma inapaswa aaminiwe zaid ana ktu tofaut hana uwezo mkubwa wa kufunga kama mawnga wengne lakn ana uwezo wa kupga pas za hatar. OKWI apgwe bench au ashndanshwe na mshambuliaj wa kat lakn s nafas ya simon yuko poa sana wakat huu.
Pia kat mtu kama mkude apunguze pas za kurud nyuma na pemben ajarbu kuwa na ujanja mwngne wa kushambulia kat pale wapnzan wanapogundua powa ya simba ni winga.
afkshe kwa dan 10 lie yeye anauwezo wa kwenda popote.
 
Aah uchambuzi mrefu ila nimesoma nusu, mimi namuunga mkono mwandishi wa habari wa Mwanaspoti.
Simba imechukua kombe la mapinduzi, lakini ni kama vile haikushiri kabisa.

Mikia msitokwe povu, timu yenu ishachokwa, halafu muwe na kumbukumbu, hamkucheza na Yanga bali mlicheza na Mtibwa Sugar.
Acheni kutoa maneno ya dhihaka kwa Yanga, ushindi wenu hautupi presha, karibuni VPL.
 
Bibie sisi tulikuwa tunajua tunacheza na nani.Wewe ndio ilikuwa una kiwewe kiasi cha kusema wakati wa penalti kwamba unajisikia vibaya na unaomba Mungu asaidie. Ni tabia ya ajabu kupatwa na hali hiyo na timu yako imeshatolewa. Mengine ni just bullshit za kawaida.
 
Bullshit?? Mkiona hivyo mjipange, hamkubaliki nyie size yenu vibonanza. Hata timu za mchangani zinashinda vibonanza.

Kuhusu kushangilia timu ni mikia mlianzisha. Kuna wakati tulikuwa tunacheza Yanga na Azam, nikashangaa kuona simba kibao na wanashangilia, Azam washangiliaji ni wa kuwahesabu tu.

Mtendwa akitendewa........ tulieni tu mimi nasema hivi wazee wa sare karibuni VPL.
 
Huyu Mwandishi na "Kanjanja" Bin Zubeiry Dugu moja.
 
Watu wengine bwana. Nani kakuambia tumeridhika na nafasi tuliyopo? Tungeridhika Phiri angekuwa bado kocha wetu. Fikra zako kama za kocha wa Taifa Stars kumchagua Msuva kwenye timu ya maboresho wakati kwa sasa hakuna winga wa kiwango chake Tanzania.

Ngarna ukiona kocha kamwita Msuva maboresho jua sio bure kuna kitu anataka amwelekeze katika mfumo anaoutumia Taifa stars.
 
Last edited by a moderator:
Bullshit?? Mkiona hivyo mjipange, hamkubaliki nyie size yenu vibonanza. Hata timu za mchangani zinashinda vibonanza.

Kuhusu kushangilia timu ni mikia mlianzisha. Kuna wakati tulikuwa tunacheza Yanga na Azam, nikashangaa kuona simba kibao na wanashangilia, Azam washangiliaji ni wa kuwahesabu tu.

Mtendwa akitendewa........ tulieni tu mimi nasema hivi wazee wa sare karibuni VPL.

Naweza kushangilia timu za mkopo lakini sijisikii vibaya inapofungwa wala siombi Mungu hiyo timu ya mkopo ishinde. Siichukii Yanga ila naipenda Simba. Sitaki Yanga ikosekane kwani bila Yanga Simba haipo na vice versa.Hoja ya kukubalika sijui tukubalike na nani au tusikubalike na nani?
 
Back
Top Bottom