Eti haya maswali majibu yake ni nini?

weng wamefika hapo walipo si kwa hiari yao......na ndio maana kauli kama hizi unazisikia
 
kama alivyosema ADII...inawezekana wengine kwa kumhitaji mtu anasema hayo baada ya hapo anapotezea na wengine ni maisha waliyonayo ndani ya nyumba yanapelekea kusema hayo.

Si umwambie mwenzio kama anakukeraaaa kwani ndo ukaseme nje ndo solution???
 
Uko sahihi kbs mamito,mie huwa nawaulizaga ulilazimishiwa ndoa?yani ni unafiki usiokuwa na kipimo na kutuona hatujawashtukia jaman nasema kbs ole wake mtu ameoa alafu anijie na hii gia atajuta kunifahamu!

Ha ha ha ha Cantalisia wewe mkali aisee atajuta kukufahamu tunatakiwa kuwa kama wewe ndo watu watapunguza huu usaniii
 
DA naomba nikunyooshee kuwa tamaa tu ndiyo inayowasumbua watu wa dizaini hiyo. Hivi ukimtongoza mtu mpaka umdanganye ndiyo akukubali? Inaeleweka kuwa inaweza kutokea kutokuelewana ndani ya nyumba lakini siyo kufikia kusema ulikosea kufanya uchaguzi. Mimi nadhani kama unataka kazi za nje fanya lakini siyo kwa kumkandia mkeo/girl friend wako vinginevyo muache umuoe huyo unayeona anakuvutia kwa kipindi hicho.
 
ukisikia mwanaume au mwanamke anatoa kauli kama hiyo na yuko kwenye ndoa ujue kuna shida.....hapo juu post # 41 nimesema wengi wamefika hapo walipo si kwa hiari yao...unaingia kwenye ndoa then kile ulichokitarajia toka kwa mtu huyo hukipati...anageuka kabisa ndoa inakuwa ndoano inafika mahali mtu anafikia hatua anasema huyu hakuwa chaguo langu niliingia kichwa kichwa ...ni kama ule wimbo wa lucky dube...it is no easy... so ukikutana na mtu wa namna hiyo na ukamdadisi na akiwa muwazi lazima afunguke na atakwambia kuwa huko kwenye ndoa yake kuna jambo

lakini pia kauli kama hii wengi huitoa kama utani vile na pia kama mtego flani hivi lakini deep down huwa kuna kitu kimejificha....anyway ndoa bana ina mambo mengi kweli tena sana sana......
 
Edson kwani ulilazimishwa jamani


kuna mazingira hupelekea kauli kama hiyo mtu kuitoa .......hasa mambo yanapobadilika ndani ya ndoa..huwa nawambia walioko kwenye ndoa mwili mmoja huwa hauji mkisimama mbele ya padre/shehe au mchungaji....kuufikia mwili mmoja ni process ndefu sana nje ya hapo lazima kauli kama hizi utazisikia tu
 
Ha ha ha ha Cantalisia wewe mkali aisee atajuta kukufahamu tunatakiwa kuwa kama wewe ndo watu watapunguza huu usaniii
Yani DA wananikera sn hawa viumbe wa aina hii maneno mengi kumbe tamaa tu hana lolote tena wengine utakuta wanawekwa mjin na wake zao,nishasema OLE WAKE,kwanza hii ni kushushiana hadhi tu kwan mie sistahili kuwa na wangu mpaka watake kunifanya nyumba ndogo!Ebo
 
Kwa Wanandoa Wengi. Miezi inapita. Miaka Inapita, Uhakika kwamba NDOA Hii itadumu unakuwa nusu kwa nusu.
Mtavumiliana wee !!
Wakati mwingine hata WAKWE nao huchangia kwanini msiachane kama ndiyo hivyo !!!
Wasiwasi huo utaisha pale Ndoa itapofika mwaka wa 40. Watoto mliozaa Wamejukuu.
Hapo kila mmoja anabaki anashangaa HAA KUMBE HAYA NDIO MAISHA YETU YA KUDUMU !!!
MUHIMU KATIKA NDOA NI UVUMILIVU, KUONEANA HURUMA NA KUSAMEHEANA.
HAKUNA MWANADAMU ALIEKAMILIKA !!
LABDA UENDE MAENEO YA BAHARINI UKASUBIRI MAJINI !!!
 
Hii ndio sababu kubwa watu wengi wanapenda kutoa/kutamka hiyo kauli, naona hata AshaDii kailezea mwishoni kabisa:

 
hizo ni lugha tu za kimihemko dada
watu wakiwa kwenye mihemko akili na mdomo havifanyi kazi kwa ushirikiano

yaani wewe............. sijui umeingia kwenye kichwa changu....................
 
Uko sahihi kbs mamito,mie huwa nawaulizaga ulilazimishiwa ndoa?yani ni unafiki usiokuwa na kipimo na kutuona hatujawashtukia jaman nasema kbs ole wake mtu ameoa alafu anijie na hii gia atajuta kunifahamu!
Ila mkwara uliopiga haki ya nani hakuna mume wa mtu JF atayetia pua kwako! Lakini nina ka swali ka uchokozi, rejea bold yangu ina maana mtu akiwa ameoa akija na gia tofauti na hiyo labda akawa mkweli katika mambo yake yote ila tu imetokea amekupenda siyo kwa kukuoa wala nini vipi anaweza kuchukua ikulu?
 
Ushauri wangu tu kwa jinsia zote....mkubaliane au la, msiache kutumia hii kitu!!
 
Tamaa tu hizo,unajua mtu huwa ana tabia ya asili ya kutoridhika.Na ndio maana hata ukiwa na mali kiasi gani bado unatafuta na kujilimbikizia.
 
Yani haijalishi amekuja na gia gani,ile kujua tu ni mume wa mtu naomba asithubutu kbs kwan hakubaliki kwangu,hiyo ni ishara tosha ya unafiki,km ameweza kuwa mnafiki kwa mkewe aliempenda na kumuoa itakuwaje kwangu mm anayetaka kunidhalilisha kwa kutaka niwe nyumba ndogo yake?
Hakuna mapnz ya kweli kutoka kwa mume wa mtu ni kudanganyana tu na kujijazia mizambi tu na malaana kutoka kwa mkewe mwisho wa siku kupata malaana na mikosi maishani.
 
oh pole sana DA. mungu akujalie afya yako iwe imara mapema

Ni tamaa tuu za mwili na hila za machoni.....hakuna cha zaidi,

kuna wimbo fulan wa zamani...
Sikinde - ngoma ya ukae, -
Mtu chake upendacho,
hakina hila moyoni,
huridhika kuwa nacho,
japo hakina thamani.............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…