DA naomba nikunyooshee kuwa tamaa tu ndiyo inayowasumbua watu wa dizaini hiyo. Hivi ukimtongoza mtu mpaka umdanganye ndiyo akukubali? Inaeleweka kuwa inaweza kutokea kutokuelewana ndani ya nyumba lakini siyo kufikia kusema ulikosea kufanya uchaguzi. Mimi nadhani kama unataka kazi za nje fanya lakini siyo kwa kumkandia mkeo/girl friend wako vinginevyo muache umuoe huyo unayeona anakuvutia kwa kipindi hicho.
ukisikia mwanaume au mwanamke anatoa kauli kama hiyo na yuko kwenye ndoa ujue kuna shida.....hapo juu post # 41 nimesema wengi wamefika hapo walipo si kwa hiari yao...unaingia kwenye ndoa then kile ulichokitarajia toka kwa mtu huyo hukipati...anageuka kabisa ndoa inakuwa ndoano inafika mahali mtu anafikia hatua anasema huyu hakuwa chaguo langu niliingia kichwa kichwa ...ni kama ule wimbo wa lucky dube...it is no easy... so ukikutana na mtu wa namna hiyo na ukamdadisi na akiwa muwazi lazima afunguke na atakwambia kuwa huko kwenye ndoa yake kuna jambo
lakini pia kauli kama hii wengi huitoa kama utani vile na pia kama mtego flani hivi lakini deep down huwa kuna kitu kimejificha....anyway ndoa bana ina mambo mengi kweli tena sana sana......
Yani DA wananikera sn hawa viumbe wa aina hii maneno mengi kumbe tamaa tu hana lolote tena wengine utakuta wanawekwa mjin na wake zao,nishasema OLE WAKE,kwanza hii ni kushushiana hadhi tu kwan mie sistahili kuwa na wangu mpaka watake kunifanya nyumba ndogo!Ebo
oh pole sana DA. mungu akujalie afya yako iwe imara mapema
Ni tamaa tuu za mwili na hila za machoni.....hakuna cha zaidi,
kuna wimbo fulan wa zamani...
Sikinde - ngoma ya ukae, -
Mtu chake upendacho,
hakina hila moyoni,
huridhika kuwa nacho,
japo hakina thamani.............
Habari zenu wapendwa wote wa jukwaa letu pendwa la MMU.
Natumaini wote muwazima kabisa na ni buheri wa afya japokuwa ya kwangu si njema sana ila nashukuru nimeweza hata kuandika haya.
Nimekuwa nikisikia nikikutana na watu mbalimbali wakisema " Ningekuwa sijaoa ningekuoa wewe"
AU "Ningekuwa sijaolewa ningeolewa na wewe" Nimejaribu kuzitafakari hizi kauli nimekosa majibu hebu waungwana na wataalamu hebu nisaidieni?
Unaoa au kuolewa kwa lazima mpaka ufikie kusema maneno kama hayo???
Au nitamaa tu ndo zinasumbua? Ama ni nini hasa?? Hebu nisaidieni
Nawatakia maandalizi mema ya weekend.
DA
Ha ha we unavonijua mie ni wa kuingia chaka kama hilo kweli?
Duuuuh wanawake kama wewe wapo wachache sana hapa duniani na si JF tu! Lakini tutoke hapo, hebu tujiulize kati ya wanaume na wanawake ni wepi walio wengi na kama unajua kwa ratio ipi? Ukinijibu nitajenga hoja shosti kama nitakuwa sikubowi lakini.Yani haijalishi amekuja na gia gani,ile kujua tu ni mume wa mtu naomba asithubutu kbs kwan hakubaliki kwangu,hiyo ni ishara tosha ya unafiki,km ameweza kuwa mnafiki kwa mkewe aliempenda na kumuoa itakuwaje kwangu mm anayetaka kunidhalilisha kwa kutaka niwe nyumba ndogo yake?
Hakuna mapnz ya kweli kutoka kwa mume wa mtu ni kudanganyana tu na kujijazia mizambi tu na malaana kutoka kwa mkewe mwisho wa siku kupata malaana na mikosi maishani.
Hakujui huyo, najua hung'oleki kwa katapila wala shoka. Jamani msiniulize nimejuaje tehe tehe tehe tehe tehe.Ha ha we unavonijua mie ni wa kuingia chaka kama hilo kweli?
Utapropose kwa kibibi kizee km mie utanipeleka wapi?
Nazidi kusisitiza wanawake wa namna hii wapo wachache sana!Yani DA wananikera sn hawa viumbe wa aina hii maneno mengi kumbe tamaa tu hana lolote tena wengine utakuta wanawekwa mjin na wake zao,nishasema OLE WAKE,kwanza hii ni kushushiana hadhi tu kwan mie sistahili kuwa na wangu mpaka watake kunifanya nyumba ndogo!Ebo